Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-06 22:24:02    
Wanyama-Pori

cri
    China ina ardhi kubwa sana na hali ya hewa ni tofauti katika sehemu mbali mbali. Kwenye ardhi hiyo kuna idadi kubwa ya milima mirefu, mito mikubwa, nyanda za juu, tambarate kubwa, majangwa, nyika na misitu minene. Na mazingira ya kimaumbile kama hayo yameifanya nchi hii iwe ni mahali pazuri sana kwa wanyama-pori ambao baadhi yao ni adimu sana.

    Kwa mujibu wa hesabu, China ina aina 1166 za ndege na zaidi ya aina 420 za wanyama. Kwa maneno mengine, inachukua asilimia 13.4 na 11 ya idadi ya jumla ya ndege na wanyama hapo duniani. Nchi hii ina aina 200 za wanyama wanaoweza kuishi katika nchi kavu na majini pia, na karibu aina 300 za wanyama watambaao. Wanyama-pori hawa si kama wanaweza kuonyeshwa kwenye bustani za wanyama tu, bali pia wanaweza kutupatia manyoya, ngozi, nyama, mafuta na madawa. Baadhi yao wanatumika katika masomo ya kisayansi, katika majaribio ya utibabu, au kwa ajili ya kufugwa. Kwa mujibu wa thamani yao ya kiuchumi, wanyama wa China wanaweza kugawanya katika wanyama wanaotoa manyoya, nyama, mafuta na madawa. Baadhi yao wanatumika katika masomo ya kisayansi, katika majaribio ya utibabu, au kwa ajili ya kufugwa.

    Kwa mujibu wa thamani yao ya kiuchumi, wanyama wa China wanaweza kugawanywa katika wanyama wanaotoa manyoya, nyama, dawa na wanyama kwa ajili ya maonyesho kwenye bustani za wanyama. China ina aina 70 na kitu za wanyama wanaotoa manyoya kama vile gray squrrel, marmot, yellow weasel, alpine weasel na lynx katika kaskazini ya China; kindi, bamboo rat, weasel na masked civet katika kusini ya China; mbweha, mbwa-mwitu, badger, chui, paka-shume na sungura wanaoonekana nchini kote. Lakini sable na fisi maji ni wenye thamani kubwa kabisa.

    Wanyama wa China ambao hutupatia nyama ni kama yak-mwitu, punda-mwitu, nguruwe-mwitu, paa, vinokera wa Kimongolia, kondoo, kulungu, argali sheep, takin, serow, reindeer na paa wenye vishungi. Licha ya kutoa nyama, wanyama wa namna hii pia wana ngozi ambazo zinaweza kutengenezwa na kuwa ngozi zisizooza, na manyoya yanaweza kutumika katika ufumaji wa nguo.

    Wanyama wanaotumika zaidi kwa kutengeneza madawa ni kama wafuatao: paa wa sika, paa wekundu, sambar, elk, paa wenye midomo meupe, swala, paa-miski, chui na dubu. Wanaweza kutoa vitu vyenye thamani vya madawa kama vile pilose antler, foetuse na penise ya paa, pembe za swala, miski; mifupa, mafuta na damu ya chui; na mafuta na nyongo za dubu.

    Kuna wanyama wengine ambao si kama wanaweza kutoa manyoya, nyama na kutumika kama dawa tu, bali pia ni muhimu katika uchunguzi wa kisayansi na kwa ajili ya madhumuni ya maonyesho. Wanyama hao ni kama nyani wasio mkia, kima wenye manyoya ya dhahabu, slender loris, panda wakubwa, panda wekundu, farasi-mwitu, ngamia-mwitu, takin, tembo wa Asia na chui wa mashariki ya kaskazini ya China.

    Wanyama-pori wengi wanapatikana nchini China tu na wengine ni maarufu duniani kote.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-06