Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-07 19:46:10    
Kampuni ya jiolojia na uhandisi ya China

cri

Kampuni ya jiolojia na uhandisi ya China (China Geo-Engineering Corporation) ni kampuni kubwa iliyopata maendeleo makubwa katika nchi za Afrika. Lakini, baada ya kampuni hiyo kuanzisha tawi huko Abidjan, mji mkuu wa Cote d'Ivoire, mwezi Oktoba, mwaka 1998, vurugu na vita vilitokea mfululizo nchini humo, ambapo kampuni ya jiolojia na uhandisi ilikumbwa na hali ngumu kutokana na migogoro na vita vilivyotokea mfululizo. Tangu mwezi Septemba, mwaka jana, kampuni nyingi za miradi ya ujenzi za nchi za nje ziliondoka au zilifungwa, wakati tawi la kampuni hiyo lililoundwa na watumishi 10 tu, lilijitahidi kutafuta njia ya kujiendeleza wakati wa kukabiliwa na matatizo. Hivi sasa, kampuni hiyo inashughulikia ujenzi wa barabara, uhifadhi wa maji mashambani, utoaji wa maji mijini na vijijini badala ya kuchimba visima tu.

    Makao makuu ya Kampuni ya jiolojia na uhandisi ya China yako Beijing, kampuni hii ina matawi na ofisi mbalimbali katika nchi zaidi ya 30 barani Asia na Afrika. Pia ina matawi na ofisi zaidi ya 30 nchini China.

    Kampuni hiyo inashughulikia miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mabwawa, barabara, madaraja, uchimbaji wa visima, utoaji wa maji, utunzaji wa mazingira, umwagiliaji maji mashambani, uchunguzi wa madini, upimaji wa maliasili, jiolojia ya kikanda, utafiti wa kifizikia na kikemikali wa dunia, pia inafanya ujenzi na biashara kwa nchi za nje.

    Kati ya miradi hiyo mbalimbali, kazi muhimu kwa kampuni ya jiolojia na uhandisi ni miradi ya ujenzi. Wakati kampuni hiyo ilipoingia nchini Cote d'Ivoire, serikali ya huko haikujua sana kampuni hiyo ya China, hata idara husika ziliona kuwa, kampuni hiyo haina uzoefu wowote wa ujenzi. Lakini baada ya kufanya jitihada kubwa, kampuni ya jiolojia na uhandisi ilionesha vya kutosha uwezo wake kwa serikali ya Cote d'Ivoire, ikakubaliwa kushiriki kwenye ujenzi wa miradi baada ya kupitia ushindani wa kujipatia zabuni. 

 Hata hivyo, kampuni hiyo bado inakabiliwa na matatizo mengi makubwa katika njia yake ya kuingia katika soko la ujenzi nchini Cote d'Ivoire ambalo lilihodhiwa siku zote na makampuni ya nchi za magharibi. Ili kuingia katika soko la nchi hiyo, kampuni ya jiolojia na uhandisi ilifanya kwa makini uchunguzi wa hali ya soko, na ilishinda katika zabuni ya mradi wa uchimbaji wa visima 900 iliyotengewa fedha na Benki ya uendelezaji ya Afrika. Kutokana na sifa ya kampuni hiyo katika mradi wa uchimbaji wa visima, mradi huo ulimalizika kwa muda usiofikia mwaka mmoja kabla ya mpango uliowekwa. Zana za ujenzi na ufundi za kampuni hiyo zote zinaweza kulingana na kampuni nyingine zilizofanya ujenzi kwa miaka mingi nchini humo.

Mafanikio hayo yalibadilisha maoni na msimamo wa serikali na wananchi wa Cote d'Ivoire, pia kuiwezesha kampuni hiyo kupata nafasi kwenye soko la ujenzi la Cote d'Ivoire na kushiriki kwenye miradi mingi zaidi ya ujenzi. Mwanzoni, mkuu wa idara inayoshughulikia usimamizi wa miradi ya ujenzi alipinga kampuni za China kushiriki kwenye ujenzi wa uchimbaji wa visima, lakini baada ya kukagua sehemu ya ujenzi wa kampuni ya jiolojia na uhandisi ya China, mkuu huyo aliridhika sana, alikula kwa pamoja kwa furaha na mafundi wa China. Baada ya hapo, kampuni hiyo haikukutana tena vikwazo vilivyowekwa na idara zinazoshughulikia utoaji wa zabuni, badala yake, wakati fulani, idara husika zilialika kampuni ya jiolojia na uhandisi ya China kushiriki kwenye zabuni ya miradi mipya ya ujenzi. Kutokana na hayo, jina la kampuni ya jiolojia na uhandisi ya China linajuliakana siku hadi siku. Kampuni hiyo inapanua nafasi yake siku hadi siku kwenye soko nchini Cote d'Ivoire, bali pia inapanua soko lake nchini yake Ghana hatua kwa hatua.

    Baada ya ushindani mkali, kampuni ya jiolojia na uhandisi imeimarisha imani yake katika kupanua soko la ujenzi barani Afrika, ambapo kampuni hiyo ilipata uzoefu mwingi katika miradi mbalimbali. Hususan baada ya uasi wa kijeshi kufanyika nchini Cote d'Ivoire mwaka jana, kampuni hiyo ilijitahidi kutafuta njia ya kujiendeleza na kushika fursa mbalimbali kupata miradi ya ujenzi wakati inapokabiliwa na matatizo mbalimbali. Kampuni hiyo inaona kuwa, kufahamishwa ipasavyo miradi ya ujenzi ni njia pekee kwa kuepusha migogoro ya kibiashara. Wakati huo huo, inapaswa kutekeleza mkakati wa uendeshaji wa shughuli mbalimbali.

    Ingawa vita vya wenyewe kwa wenyewe viliendelea katika miaka ya hivi karibuni nchini Cote d'Ivoire, ambapo vurugu na migogoro ilitokea mara kwa mara katika nchi hiyo,hali ya uchumi nchini humo ni ngumu, lakini kampuni hiyo inazidi kupata maendeleo mapya. Baada ya kuchambua hali ya Cote d'Ivoire, kampuni hiyo inaona kuwa, nchi hiyo ina soko kubwa katika nyanja ya ujenzi, lakini kampuni za China bado zinaweza kujiendeleza. Na itaendelea kuchukua hatua mwafaka kwa kukabiliana na mabadiliko mbalimbali, ili kujipatia mafanikio makubwa zaidi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-07