Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-07 21:09:20    
"Njia ya hariri ya zamani" na mpya

cri

    "Njia ya Hariri" ya zamani ya kibiashara iliyopitia Asia na kuungana na Ulaya imekuwa na historia ya miaka zaidi ya elfu mbili.

    Njia hiyo ilianzia China, ilikuwa mchango mkubwa wa utamaduni wa China kwa ustaarabu wa dunia. Njia hiyo ilianzia mji wa Changan yaani mji wa Xi An wa leo, ilikuwa na urefu wa kilomita zaidi ya elfu 4 ya China, upande wake wa magharibi unafikia India, Iran na ukingo wa mashariki wa Bahari ya Mediterranean na kufikia Rome Italia, urefu wake ulikuwa kilomita 7000. Hii ilikuwa ni njia ya mawasiliano ya utamaduni na uchumi kati ya Mashariki na Magharibi, ambayo iliunganisha utamaduni wa Kichina, Kiindia, Kiuajemi, Kiarabia, Kiugiriki na Rome ya kikale, ilitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya maingiliano ya utamaduni .

    Ili kuridhisha mahitaji ya kibiashara kati ya Ulaya na Asia, Umoja wa Barabara wa Kimataifa ulitoa ushauri wa "kufufua njia ya hariri". "Njia mpya ya hariri" inaanzia mji wa Lianyugang wa China uliopo kwenye ukingo wa magharibi wa Pasifiki ikifuata "njia ya hariri ya zamani" kupitia nchi za Asia na Ulaya mpaka Bahari ya Atlantiki, ikawa kama daraja la kuunganisha bara la Asia na Ulaya na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya ustawi wa biashara katika mabara hayo mawili.

    Pande mbili za "njia mpya ya hariri" za mashariki na magahribi zinaungana na sehemu kubwa za maendeleo ya uchumi za pasifiki na Atlantiki, na sehemu kubwa ya katikati yaani bara la Asia na Ulaya ni sehemu zilizo nyuma katika uchumi kwa nchi chache tu. Hivi sasa njia ya kuanzia Uturuki kupitia Iran, Turkmenistan, Uzbekistan, Kazakstan, Kirghizstan hadi China haiwezi kutosheleza mahitaji ya mawasiliano ya barabara. Lakini sehemu hizo zina mahitaji makubwa ya kutegemeana na kusaidiana katika uchumi, ushirikiano unaonufaishana kati ya pande zote utakukwa mkubwa. Pendekezo la kufufua njia ya hariri lililotolewa na Umoja wa Barabara wa Kimataifa linaambatana na mahitaji ya nchi zilizopo kwenye njia hiyo katika ujenzi wa miundombinu, kuendeleza uchukuzi wa kimataifa wa barabara, kwa hiyo linaungwa mkono na nchi hizo.

    "Njia Mpya ya Hariri" ina urefu wa kilomita 4395 ikipitia sehemu za mashariki, katikati, na magharibi nchini China penye mikoa ya Jiangsu, Shandong, Anhui, Henan, Shanxi, Shan'xi, Ningxia, Qinghai, Gansu, Xinjiang, mikoa kumi, na itaathiri mikoa ya Hubei, Sichuan, Hebei, na Mongolia ya Ndani. Watu walioko kwenye sehemu hizo wanakaribia milioni 400 ambao ni asilimia 30 ya watu wote wa China na ardhi ya sehemu hizo zinachukua 37% ya ardhi yote ya China. Hivi sasa barabara ndani ya China zimekuwa zikijengwa.

 Idhaa ya Kiswahili 2004-05-07