Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-11 19:30:12    
Zao maalumu lililohamishwa kutoka kando ya Meditrenia laleta utajiri kwa mkoa wa Sichuan

cri
    Mzeituni ambao ni zao maalumu kwenye kando ya bahari ya Meditrenia, umeleta utajiri kwa wakulima wa mkoani Sichuan.

    Mji wa Guangyuan, mkoani Sichuan umejulikana kwa shamba kubwa la mizeituni hapa nchini baada ya kupanda mizeituni karibu hekta 6,700. Mfuta yanayotengenezwa kutokana na matunda ya miti hiyo yenye thamani kubwa ya kiuchumi kutoka kando ya bahari ya Meditrenia, yanahitajiwa sana katika masoko ya nchini na ya nchi za nje, na yameleta utajiri mkubwa kwa walimali wa zao hilo mkoani Sichuan.

    Hivi sasa, mafuta ya zeituni yanayohitajiwa sana katika masoko ya nchini, ambapo mafuta ya zeituni yanayohitajiwa na Beijing peke yake ni tani 16,000 kwa mwaka, na yanauzwa kwa bei ya kiasi cha Yuan 15 kwa kilo, kiasi hiki ni sawa na dola za kimarekani 18 kwa kilo. Kutokana na makadirio ya watawalamu, mizeituni iliyopandwa katika kipindi cha kwanza karibu hekta 6,700 itaanza kuzaa kwa wingi mwaka 2007, na inatarajiwa kuzaa zeitui tani elfu 60, na kuwa na pato la Yuan zaidi ya bilioni 1.6, sawa na dola za kimarekani milioni 195 kwa mwaka.

    Mafuta ya zeituni yanasifiwa na watu kuwa ni "dhabu ya mafuta inayonukia" na "malkia wa mafuta ya mimea" ambayo yanatumika sana katika utengenezaji wa vyakula, podozi, madawa pamoja na kulainisha ngozi ya uso. Maua ya mizeituni yanaweza kutumiwa na nyuki kuzalisha asali; vijiti vya mti ni vyenye proteni nyinig ambavyo vinaweza kutumiwa kama chakula kwa ng'ombe, kondoo na mifugo mingine; zeituni zilizotengenezwa kwa chumvi ni chakula kizuri kwa binadamu. Lakini siyo kwamba mitunda hiyo inaweza kupandwa kila mahali isipokuwa sehemu chache tu, ndiyo maana uzalishaji wa mafuta ya zeituni ni kati ya tani milioni 1 na milioni 1.4 kwa mwaka katika dunia nzima, na sehemu zinazofaa kwa ulimaji wa zao hilo, hususan ziko katika nchi za pwani ya bahari ya Meditrenia zikiwemo Ugiriki na Italia ambazo zinachukua 98% ya uzalishaji wa zeituni. Mafuta ya zeituni yanayopatikana katika masoko ya kimataifa ni kiasi cha tani laki moja tu ambacho ni kiasi kidogo sana kikilinganishwa na mahitaji ya watu.

    Sehemu zinazofaa kwa ulimaji wa zalo hilo za mji wa Guangyuan ni kiasi cha hekta laki 1 na elfu 33, hususan ni kwamba kulikuwa na mabwawa na maziwa makubwa baada ya kukamilishwa ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme wa Mazhusi mwaka 1977, wataalamu husika walithibitisha kuwa Guangyuan ni moja ya sehemu chache zinazofaa kwa ulimaji wa zao la zeituni nchini China. Hivi sasa, China inaweza kuzalishaji mafuta ya zeituni tani 4 hadi tani 6 ambayo kiasi cha nusu yake yanatoka mkoa wa Sichuan.

    Toka mwaka 2000, Guangyuan ilichukua mradi wa uendelezaji wa hekta 6,700 kuwa ni nguzo ya uzalishaji mali ya maendeleo ya uchumi wake inayohusisha Kampuni ya mafuta ya zeituni ya Shubei, Guangyuan na koo zaidi ya laki moja za wakulima, ambao walipata mikopo Yuan milioni 30, kiasi ambacho ni sawa na dola za kimarekani milioni 3.7.

    Aidha, mkoa wa Sichuan ulipata msaada wa fedha wa Yuan milioni 15, sawa na dola za kimarekani milioni 1.86, kutoka Ujerumani kutokana na mradi wa uendelezaji wa mashamba ya mizeituni yapatayo hekta 6,700. Serikali za mkoa wa Sichuan na mji wa Guangyuan zinauchukulia mradi huo kama ni wa kusaidiwa wa kupanda miti kwenye ardhi iliyoendelezwa kuwa mashamba na kunufaika zaidi kutokana na sera nafuu za serikali, ambapo serikali inatoa ruzuku ya Yuan 50 kwa miche ya mizeituni, sawa na dola za kimarekani 6 kwa hekta, Yuan 20 za ruzuku ya maisha na kilo 150 ya nafaka kwa mwaka katika muda wa miaka miatnao.

    Hivi leo, ujenzi wa mradi wa zeituni umekuwa nguzo ya uzalishaji mali na sekta mpya yenye ongezeko kubwa la uchumi za mji wa Guanyuan. Ujenzi wa mradi wa upandaji wa mizeituni ambao ni kupanda mizeituni milioni tatu na laki tatu katika hekta 6,700, ulikamilishwa katika mwisho wa mwaka uliopita, hivi sasa miti hiyo imekuwa na urefu wa mita tatu hivi. Licha ya kuzaa zeituni kwa wingi, miti

    hiyo inaweza kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kuendeleza uchumi katika milima pori.

    Sasa ujenzi wa kipindi cha pili wa mradi wa zeituni umeanzishwa, ambao ni kupanda mizeituni hekta elfu 13.5 katika muda wa miaka minne, na hivi sasa wameshamaliza kupanda mizeituni katika hekta 400. hivi sasa, mji wa Guanyuan una shamba la miche ya mizeituni lenye uwezo wa kutoa miche milioni moja na laki tano kwa mwaka, wakati ujenzi wa kiwanda cha ushidikaji wa mafuta ya zeituni umeingia kipindi cha pili cha kutoa zabuni duniani kwa mitambo na zana zinazohitajika kiwandani humo. Ujenzi wa kiwanda cha ushindikaji wa mafuta ya zeituni unatarajiwa kukamlishwa kabisa mwaka 2005. Kutokana na mpango, mashamba ya mizeituni ya mji wa Guanyuan yatapanuliwa hadi hekta elfu 33, baada ya mpango huo kutimizwa, kila mkazi wa mji wa Guanyuan wenye idadi ya watu milioni 3, ataweza kuwa na mizeituni 40 kwa wastani.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-11