Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-11 22:22:14    
China yajitahidi kupata mafanikio makubwa zaidi katika sekta ya sayansi na teknolojia

cri
    Mwaka 2003, China ilirusha chombo kilichobeba mwanaanga wa kwanza Bwana Yang Liwei kwenye safari ya anga ya juu, na pia ilipata mafanikio mengi katika sekta ya sayansi na teknolojia, matumizi na uenezaji wa matunda hayo ya kisayansi na kiteknolojia umesukuma mbele maendeleo ya uchumi wa China, na kuongeza zaidi nguvu halisi ya nchi ya China.

    Tarehe 15 Novemba mwaka 2003, chombo cha kwanza cha China kilichoitwa Shenzhou No.5 kilichobeba mwanaanga wa kwanza kilirushwa kwenye anga ya juu, ambapo wachina walitimiza ndoto yao ya miaka mingi ya kusafiri kwenye anga ya juu.

    Kufanikiwa kurusha chombo hicho kumeifanya China kuwa nchi ya tatu duniani kufuatia Marekani na Russia kuanzisha shughuli za kubeba binadamu kusafiri kwenye anga ya juu. Mwanaanga wa kwanza wa China Bwana Yang Liwei akawa shujaa wa taifa, na chombo cha safari ya anga ya juu ya Shenzhou No.5 pia kimekuwa alama moja ya China katika mwaka 2003, mafanikio hayo makubwa yaliwashangaza sana watu wa dunia. Mjumbe mwenye cheo cha waziri wa Idara ya utafiti wa sayansi na teknolojia mpya ya Ufaransa ambaye alikuwa mwanaanga wa kwanza Ulaya Bibi Claudie Haignere alisema kuwa, kufanikiwa kurushwa kwa chombo cha Shenzhou No.5 kumeonesha kuwa China imekuwa na nguvu halisi ya kisayansi na kitekenoloji.Alisema:

    China ilifaulu kurusha chombo cha kubeba mwanaanga kwenye anga ya juu, hii imeonesha kuwa China ina nguvu kubwa sana katika maendeleo ya sayansi na teknolojia, China ni mwezi wa ushirikiano mwenye nguvu kubwa kwa Ufaransa ama Ulaya katika sekta za sayansi na teknolojia.

    Mwaka 2003 ulikuwa kama mwaka wa safari ya anga ya juu ya China, katika mwaka huo mmoja, China ilirusha satlaiti 6 na chombo kimoja kwenye anga ya juu, na katika mwezi mmoja baada ya kurushwa kwa chombo cha Shenzhou No.5 cha safari ya anga ya juu, China ilirusha satlaiti ya maliasili ya China na Pakistan, satlaiti ya uvumbuzi wa No.1 ya China, satlaiti ya 18 itakayorudishwa na satlaiti ya mawasiliano ya No.20 ya Zhongxing kwenye anga ya juu. Shughuli hizo zilizofanyika kwa mfululizo na kwa mafanikio katika muda mfupi zimeonesha kuwa teknolojia ya safari ya anga ya juu ya China inaimarika siku hadi siku, na usimamizi wa mfumo wa uhandisi pia umekamilika siku hadi siku.

    Mafanikio hayo yalikuwa machache miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana nchini China katika sekta za sayansi na teknolojia mwaka 2003. Katika miaka ya hivi karibuni, China imetekeleza mikakati ya kusitawisha nchi kwa kutegemea sayansi na teknolojia, na matunda kemkem yalipatikana mwaka 2003. Mwishoni mwa mwaka 2003, wanasayansi walifaulu kutengeneza kompyuta ya aina ya 6800 Shenteng ya Lianxiang yenye uwezo wa juu wa hesabu, mwendo wa hesabu wa kompyuta ya aina hiyo unaweza kufikia zaidi ya bilioni 4000 kwa sekunde, mwendo huo wa hesabu ya haraka unachukua nafasi ya 14 miongoni mwa kompyuta zenye uwezo wa juu duniani, ufanisi wake wa kikazi unachukua nafasi ya pili, na uwezo wa kushughulikia mambo unachukua nafasi ya 4. Kufanikiwa kwa utafiti na utengenezaji wa kompyuta ya aina ya Shenteng 6800 kumekomesha historia ya kuhodhiwa kwa soko la China na kompyuta za nchi za nje zenye uwezo wa juu. Mtaalamu aliyeshughulikia upimaji juu ya kompyuta ya aina hiyo Profesa Qian Depei anasema:

    Kwa maoni ya upimaji, wataalamu wameona kwa kauli moja kuwa, kompyuta ya aina hiyo imefikia kiwango cha juu zaidi miongoni mwa kompyuta zenye uwezo wa juu duniani, na imeonekana uvumbuzi mkubwa wa ubora wa mtambo mkuu na shughuli za mambo.

    Na mwezi Desemba mwaka 2003, Chuo kikuu cha Beijing cha China kilitangaza kuwa micron chip zilizosanifiwa na kutengenezwa na idara husika ya chuo hicho zimeanza kuzalishwa katika kiwanda chake, sasa kompyuta zenye uwezo wa juu za China zitakuwa na chip za kichina ambazo zimesukuma mbele maendeleo ya shughuli za upashanaji habari nchini China. Na wakati huo huo, Shirika la afya duniani WHO lilitangaza kuwa, dawa ya chanjo ya ugonjwa wa SARS inayofanyiwa utafiti nchini China itafanyiwa majaribio hospitalini kwa mara ya kwanza kuanzia mwezi Januaria mwaka 2004. Hii imeonesha kuwa utafiti wa China kuhusu chanjo ya ugonjwa wa SARS umeongoza duniani.

    Mwaka 2003, mafanikio makubwa yamepatikana katika utafiti wa sayansi wa kimsingi. Majarida ya sayansi yaliyo maarufu sana duniani "Nature" na "Seience" yalichapisha makala zilizoandikwa na wanasayansi wengi wa China mwaka 2003, na kujulisha mafanikio makubwa waliyoyapata katika utafiti wa sayansi ya maisha na viumbe vya zama za kale.

    Katika miaka mfululizo ya hivi karibuni, uchumi wa China unaendelea kwa haraka, ambapo maendeleo ya sayansi na teknolojia yalitoa mchango mkubwa. Hivi sasa mwelekeo wa ongezeko la haraka unaonekana katika kazi za sayansi na teknolojia za hali ya juu kama vile shughuli za upashanaji habari, hili limekuwa ongezeko kubwa lenye uhai katika uchumi wa China. Waziri mkuu wa China Wen Jiabao alilisifu na kusema kuwa, maendeleo ya sayansi na teknolojia za China yamesukuma mbele maendeleo ya uchumi na nguvu halisi ya nchi.Akisema:

    Maendeleo ya sayansi na teknolojia ya hali ya juu ya China yameongeza nguvu halisi ya sayansi na teknolojia, nguvu halisi ya uchumi, nguvu halisi ya ulinzi wa taifa na nguvu ya mshikamano wa taifa, maendeleo hayo yana umuhimu mkubwa .

    Katika mwaka 2003, China imeanza kubuni "Mpango wa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2020, ambapo serikali ya China imeanza kutekeleza utaratibu wa kuwahamasisha umma, kuweka mkazo katika kusikiliza maoni na mpendekezo ya wanasayansi na wanateknolojia wa nchini na ng'ambo ili kuisaidia serikali ya China kutoa uamuzi wa kisayansi. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesukuma mbele zaidi maendeleo ya uchumi, elimu, utamaduni na mambo ya kijeshi nchini China na kuboresha zaidi hali ya kuzalisha mali na kuishi maisha kwa wachina .

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-11