Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-15 19:24:54    
Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Angola unaendelea katika kipindi kipya

cri
    Ingawa uko umbali mkubwa kati ya China na Angola, lakini urafiki wa kijadi kati ya nchi hizo mbili ulioanzishwa kutokana na mapambano ya kujipatia uhuru na ukombozi wa taifa unadumu kwa muda mrefu. Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili mwaka 1983, uhusiano wa ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili unazidi kukuzwa. Angola ilikomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoendelea kwa miaka 27 mwaka 2002, ambapo ukarabati wa nchi hiyo baada ya vita ulianzishwa baada ya hapo. Hali hiyo si kama tu imewekwa mazingira mazuri kwa maendeleo ya jamii na uchumi, bali pia inahimiza uhusiano wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili kuendelea katika kipindi kipya.

    Kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika nchini Angola, baadhi ya kampuni za China ziliingia nchini humo, na kushughulikia ujenzi, uvuvi na biashara, ambapo shughuli hizo zinafanya kazi muhimu kwa kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili. Serikali ya China pia ilitoa mikopo isiyo na riba ikiwa kama misaada ya uchumi kwa Angola. Serikali ya China ilitoa mikopo ya dola za kimarekani milioni 11 kujenga makazi kwenye sehemu ya uendelezaji wa uchumi huko Luanda, mji mkuu wa Angola, ambapo makazi hayo yanakaribishwa sana na Angola. Ili kuondoa matatizo ya ukosefu wa vifaa na kuwasaidia wakimbizi na watu waliopoteza nyumba kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, serikali ya China ilitoa kiasi kikubwa cha vifaa vya misaada kwa Angola kila mwaka.

    Angola ni nchi yenye maliasili nyingi, inajulikana kama ni nchi yenye hazina kubwa barani Afrika. Ina madini za aina zaidi ya 30, zikiwemo mafuta, gesi, almasi, dhahabu, platinamu, chuma, manganizi, kwatzi, fosfati, marumaru na matale. Takwimu zinaonesha kuwa, malimbikizo ya mafuta ya nchi hiyo yanafikia mapipa bilioni 15, hivi sasa, uzalishaji wa mafuta unafikia mapipa milioni 1, kiasi cha almasi kimefikia karati milioni 200, mapato ya Angola kutokana na biashara ya almasi yanafikia dola za kimarekani milioni 600 hadi 700. Mbali na hayo, kilimo, misitu na maliasili ya samaki nchini humo pia yanashika nafasi muhimu sana barani Afrika.

    Lakini, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoendelea kwa miaka mingi nchini humo vilileta hasara kubwa kwa nchi hiyo, si kama tu vilisababisha vifo vya watu karibu milioni moja, bali pia iliharibu vibaya sana miundo mbinu za nchi hiyo, na kuweka vikwazo kwa maendeleo ya jamii na uchumi. Ili kufanya ukarabati wa nchi hiyo baada ya vita, kuvuta mitaji, na teknolojia kutoka nchi za nje, serikali ya Angola ilitekeleza sera ya diplomasia ya kiuchumi, na sheria mpya ya uwekezaji vitega uchumi, ili kuvutia nchi nyingi zaidi kuwekeza vitega uchumi nchini humo, na kuanzisha mawasiliano ya uchumi na biashara.

    Rais Dos Santos wa Angola aliwahi kusema kuwa, anatumaini kuwa, kampuni nyingi zaidi za China zitafanya biashara nchini humo, na kujiunga na ukarabati wa nchi hiyo baada ya vita. Serikali ya China pia inazingatia sana kuzidisha uhusiano wa uchumi na biashara na Angola. Katika mwaka mmoja uliopita tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Angola, mawasiliano ya uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili yanazidi kuongezeka, ambapo pande hizo mbili zinafanya ukaguzi wa biashara mara kwa mara. Hadi mwishoni mwa mwezi Septemba, mwaka huu, thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili ilifikia dola za kimarekani bilioni 1.7.

    Takwimu zilionesha kuwa, hadi mwishoni mwa mwaka 2003, thamani ya biashara ya nchi hizo mbili ilizidi dola za kimarekani bilioni 2. Ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Angola unaingia katika kipindi kipya. Hivi sasa, nchi hizo mbili zinafanya mazungumzo na kutekeleza miradi mingi zaidi ya ujenzi. China ilitenga fedha za dola za kimarekani milioni 65 na kuanzisha mradi wa uboreshaji wa waya ya mikoa ya Namibe, Huila na Lunda-Norte, ambapo ilitoa mkopo wa fedha za dola za kimarekani milioni 90 na kuanzisha mradi wa utengenezaji wa reli ncini Angola. Miradi hiyo miwili ilianzishwa mwezi Oktoba na mwezi Novemba, mwaka jana. Aidha, ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Luanda uliojengwa kwa mikopo isiyo na riba ya China utaanzishwa mapema.

    Angola ni nchi kubwa ya maliasili barani Afrika, ambapo ina mustakabali mzuri katika siku za mbele. Ukarabati wake baada ya vita unahitaji misaada kutoka nchi za nje, wakati huo huo unatoa nafasi nzuri kwa nchi za nje kufanya biashara nchini humo. China ina msingi imara wa viwanda na kilimo, baada ya sera ya mageuzi na ufunguaji wa mlango kutekelezwa nchini China, uchumi na tekenolojia za China zinazidi kupata maendeleo mapya, wakati nguvu ya taifa inazidi kuongezeka, si kama tu inahitaji kuvutia uwekezaji vitega uchumi kutoka nchi za nje, bali pia inahitaji kuanzisha shughuli katika nchi za nje. Kutokana na hayo, uhusiano wa uchumi na biashara kati ya China na Angola utanufaisha pande zote mbili, na utapata mafanikio makubwa zaidi katika siku za usoni.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-15