Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-18 19:23:22    
Vituo vya kurusha vyombo vya usafiri wa anga ya juu duniani

cri

Kituo cha urushaji wa satlaiti cha Jiuquan, China

Kituo cha urushaji wa satlaiti cha Xichang, China

    Katika maendeleo ya kurusha vyombo vya kusafiri kwenye anga ya juu duniani ya zaidi ya nusu karne iliyopita, mataifa mbalimbali makubwa yenye teknolojia ya kimaenedeleo yalijenga vituo vya usafiri wa anga ya juu. Vituo vya kurusha vyombo vya usafiri wa anga ya juu vyenye zana kamili vimekuwa ishara moja ya kuwa na nguvu katika sekta ya usafiri wa anga ya juu.

    Kituo cha kurusha vyombo vya usafiri wa anga ya juu cha Beknur kilichojengwa na Urusi ya zamani mwaka 1955, kiko kwenye sehemu ya jangwa kusini mwa Kazakhstan. Kijografia, sehemu hiyo yenye eneo la karibu kilomita za mraba 100 na wakazi wachache sana, inafaa sana kutumika kwa shughuli hizo.

    Beknur ni kituo chenye uwezo kamili cha Urusi ya zamani cha kurusha vyombo vya usafiri wa anga ya juu, ambacho kinaweza kurusha chombo cha kusafiri kwenye anga ya juu chenye binadamu, setilaiti pamoja na vyombo vya uchunguzi kwenye mwezi na sayari nyingine. Kituo hicho kilijulikana sana kutokana na kwamba 80% hadi 90% ya shughuli za urushaji zilifanyika huko. Tarehe 12 mwezi Aprili waka 1961, chombo kilichomchukua mwanaanga wa kwanza duniani Bw. Gagalin kilirushwa kwenye anga ya juu kutoka kituo hicho.

Kituo cha kurusha vyombo vya anga ya juu ya Japani

    Baada ya Urusi kuvunjika, Russia iliendelea kukutumia kituo hicho kwa kukikodi kutoka Kazakhstan, isipokuwa shughuli hizo za urushaji zimepungua sana kutokana na kuzorota kwa uchumi wa Kazakhstan na Russia, na kuchakaa kwa zana nyingi za kituo hicho. Hata hivyo, vyombo vya usafiri wa anga ya juu vya aina za "Muungano" na "Maendeleo" vilevile vilirushwa angani kutoka katika kituo hicho.

    Kituo cha usafiri wa anga ya juu cha Kenedy kilichojengwa mwaka 1962 na kutumia jina la rais wa nchi, ni cha kwanza kwa ukubwa nchini Marekani. Kituo hicho chenye eneo la kilomita za mraba 280, kiko katika kisiwa cha Marid, kilichoko katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Kituo cha kurusha vyombo vya anga ya juu ya Brazil

    Lengo la kujenga kituo hicho ni kurusha vyombo vya anga ya juu vinavyozunguka karibu na dunia, na kinajulikana kwa kurusha angani maroketi yanayobebea ndege tokea miaka ya 80 ya karne iliyopita. Kituo hicho kina sehemu 14 za urushaji ambazo nyingi zake zilibomolewa, sehemu ya No. 39 pamoja na eneo la kiwanda chake vilivyojengwa mwaka 1966 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa "Apolo", baada ya kurekebishwa sasa kinatumika kwa kurusha na kufanya majaribio ya maroketi yanayobeba ndege. Vyombo vingi vya kusafiri katika anga ya juu vilirushwa kutoka katika kituo hicho.

    Licha ya kuwa na kituo hicho cha kurusha maroketi ya kubebea ndege, nchini Marekani kuna kituo kingine vya kurusha vyombo vya kusafiri katika anga ya juu, ambacho kinajulikana kwa Fandenbo, kituo hicho chenye eneo la kilomita za mreba 280, kilikuwa cha jeshi la anga la Marekani. Kituo hicho, ambacho hapo awali kilikuwa cha kurusha makombora ya masafa marefu, kiko katika sehemu ya kusini ya pwani ya Carifonia.

Kituo cha kurusha vyombo vya anga ya juu ya Ulaya

    Kituo cha kurusha vyombo vya kusafiri kwenye anga ya juu cha Ulaya kiko katika Kulu, iliyoko kwenye pwani ya bahari ya Atlantic nchini Guyana. Kituo hicho kiko chini ya kituo cha utafiti wa anga ya juu cha nchi hiyo ambacho kinashughulikia zaidi urushaji na majaribio ya setilaiti ya sayansi, setilaiti ya matumizi mbalimbali, maroketi ya uchunguzi pamoja na maroketi ya kubebea vyombo vya usafiri wa anga ya juu. Kulu iko karibu na ikweta, hivyo inafaa sana kwa urushaji wa maroketi.

    Hivi sasa kituo cha usafiri wa anga ya juu kina maeneo matatu ya kurusha maroketi ya Aliana, maroketi zaidi ya mia moja ya aina hiyo yalirushwa angani kutoka katika kituo hicho. Kulu ni kituo muhimu sana kwa Ulaya katika harakati za usafiri kwenye anga ya juu, na pia ni kituo kinachopewa kazi nyingi za kibiashara duniani. Lakini kituo hicho hadi hivi sasa bado hakijapewa kazi ya kurusha vyombo vya kusafiri kwenye anga ya juu chenye binadamu ndani yake.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-18