Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-19 20:10:33    
China yajitahidi kutumia nishati bila ubadhirifu

cri

    Wakazi wengi wa Beijing bado wanakumbuka, jinsi jengo la Apartment building ya kimataifa ya Fengshang ilivyouzwa kwa haraka katika mwaka 2001. Ingawa nyumba ya jengo hilo iliuzwa hadi Yuan elfu 13 kwa mita, kiasi hiki ni sawa na dola za kimarekani 1585 kwa mita, tena jengo hilo haliko katika sehemu iliyo nzuri sana, lakini wanunuzi walimiminikia huko kuzinunua. Mkurugenzi wa kampuni ya Fengshang Bw. Shi Yong alisema kuwa sababu moja iliyowavutia sana wanunuzi ni zana zake za kisasa zinazopunguza matumizi ya nishati.

    "Jengo hilo linatumia nishati kidogo sana likilinganishwa majengo mengine, ambalo kuta zake zinatumia teknolojia mpya ya kutunza vizuri halijoto ya nyumbani baada ya kutumia mfumo mpya, ambapo matumizi ya nishati ya bola na sentrao heating ni 20% tu yakilinganishwa na yale ya kawaida."

    Hivi sasa jengo hilo limekuwa mfano wa kuigwa katika upunguzaji wa matumizi kwa ujenziwa nyumba za kukaa. Kwa kufuata njia hiyo, matumizi ya makaa ya mawe kwa centra heating kwa mita za mraba yatapungua kutoka kilo 25 katika miaka ya 80 ya karne iliyopita hadi kilo 12.5, hatua ambayo inafanya Beijing kupunguza matumizi ya makaa ya mawe tani laki 5 kwa mwaka. Ingawa kiwango cha maendeleo katika sehmu mbalimbali ni tofauti, lakini idadi ya majengo mapya yanayopunguza matumizi ya nishati imezidi 2%, sasa teknolojia hiyo inatumika kwa kurekebisha nyumba zilizojengwa hapo awali. Teknolojia hiyo ni kupaka aina kitu cha kemikali katika vigae vinavyobandikwa kwenye upande wa nje wa kuta za nyumba ambazo zinaweza kuzuia ubaridi wa nje usiingie ndani ya nyumba.

    Kwa kuwa matumizi mengine makubwa ya nishati ni ya vyombo vya umeme majumbani kwa watu, hivi sasa China inazalisha na kutumia vyombo vya umeme vinavyotumia umemem kidogo. Kila mwaka idara za serikali zinaandaa wiki ya kuokoa asilimali za nishati, zikitoa wito wa kutaka wananchii wasitumia nishati ovyoovyo na kutumia vyombo vya umeme visivyotumia umeme mwingine. Hivi sasa idara husika zinataka watu watumia aina ya taa za umeme zinazotumia umeme kidogo na kutoa mwangaza mkali. Hivi sasa taa za aina hiyo zimetumiwa sasa na watu majumbani mwao.

    Bibi Li Aixian kutoka taasisi ya utafiti wa vigezo vya kiteknolojia ya China, alisema kuwa ili kushawishi viwanda vya uzalishaji wa vyombo vya umeme vitumie teknolojia za upunguzaji wa matumizi ya umeme, China imeweka kigezo cha matumizi ya vyombo vya umeme vinavyotumika majumbani mwa watu. Tunachukua mfano wa friji, sasa tumeweka kiwango cha matumizi ya uemem kwa masaa 24, an kuagiza viwanda visizalishe vyombo vya umeme vinavyotumia umeme zaidi ya kiwango kilichowekwa.

    "Vigezo vinavyotekelezwa hivi sasa ni aina 14 zikiwa ni za friji, TV za rangi, mashine za kufulia nguo na taa za nyumbani. Tumekadiria kwamba kutoka mwaka 2004 hadi mwaka 2010, nishati itakayookolewa kutokana na kutumika kwa vyombo hivyo vya umeme, itakuwa sawa na tani zaidi ya milioni mia 2 za makaa ya mawe."

    Alisema kuwa, ikiwa tunapiga hesabu kutoka sasa hadi mwaka 2020, nishati itakayookolewa na vyombo hivyo vya umeme ni sawa na matumizi ya nishati ya China ya mwaka mmoja mzima. Habari zinasema kuwa idara husika za China zitaweka vigezo kwa vyombo vya umeme vingi zaidi ili kupunguza matumizi ya umeme.

    Ili kupunguza matumizi ya nishati vya viwanda, serikali ya China katika miaka ya karibuni ilitenga fedha nyingi kuviunga mkono viwanda kufanya marekaebisho ya kiteknolojia. Kwa mfano, hivi sasa, makampuni mengi ya umeme yanatoa mvuke kwa viwanda vinavyoutumia ili kupunguza maboila ya viwanda, au kutoa mvuke kwa heater za majumbani mwa watu katika majira ya baridi. Kiwanda cha uzalishaji umeme cha Gaoqiao, Shanghai, hakikutupa mvuke uliotoka kiwandani bali kinapeleka mvuke kwa viwanda vilivyo karibu nacho kwenye eneo la ustawishaji wa viwanda. Naibu meneja mkuu wa kiwanda cha uzalishaji wa umeme cha Gaoqiao Bw. Xu Jian alisema,

    "Tuko karibu na eneo la ustawishaji wa viwanda ambalo kuna viwanda vingi vinavyohitaji nishati ya ujoto. Hapo awali, viwanda hivyo vilitumia mvuke kutoka katika maboila yao vyenyewe, baada ya sisi kuvipelekea mvuke, sasa viwanda hivyo havitumii tena maboila yao tena."

    China ni nchi yenye idadi kubwa ya watu, na pia ni nchi inayotumia nishati nyingi, kukuza uchumi na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi kunahitaji nishati nyingi. Sasa China inajitahidi kutumia nishati kwa mpango mzuri, jambo hili litakuwa na mchango mkubwa kwa upunguzaji wa matumizi ya nishat duniani.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-19