|

Shanga za kifalme ni mapambo yaliyovaliwa shingoni na wafalme, wake, masuria na wana wa wafalme, mawaziri, maofisa na makamanda wakati walipovaa mavazi yao rasmi na waliposhiriki katika sherehe mbalimbali. Shanga hizo zilikuwa zinaning'inia vifuani mwao. Shanga hizo zilitengenezwa kwa kutumia shanga za Mashariki, lapis lazuli, ambari, matumbawe, feruzi, jadeite, agate, jasper, fuwele, rubi, johari ya samawati na jade.
Shanga za kifalme zilitengenezwa kwa kutunga pamoja shanga 108, kila ushanga uligawenyika katika sehemu nne, na kati ya kila sehemu ilitiwa ushanga mmoja mkubwa wa mviringo ambao unaitwa "kichwa cha Buddha". Ushanga mmoja miongoni mwao uliunganishwa na "pagoda ya Buddha" yenye umbo la mung'nye. Aidha, unaunganishwa na "wingu la mgongo" kwa kutumia utepe wa hariri ambao unaning'inia kuliunganishwa mitungo mitatu midogo ya shanga, kushoto miwili na kulia mmoja, na mitungo hiyo ilitungwa kwa kutumia shanga 10, jina lake ni "jinianer". Wingu la mgongoni na jinianer ziliunganishwa na jebu.
Aina za kofia na mavazi ya wafalme, wake, masuria, watoto wao, maofisa na makamanda, zilitengenezwa kwa kufuata kanuni tofauti. Mavazi, kofia, tepe za hariri na shanga vilevile zilitofautiana kufuatana na tofauti za vyeo, hadhi matumizi na majira.
Wakati wa sherehe muhimu, wafalme walikuwa wanavaa majoho, kofia, tepe za hariri na shanga za kifalme. Wakati huo wafalme walivaa shanga zilizotengenezwa kwa shanga za Mashariki. Wakati wa kutoa dhabihu kwa jua, walivaa shanga za matumbawe; wakati walipotoa dhabihu kwa mwezi, walivaa shanga zilizotengenezwa kwa feruzi; wakati walipotoa dhabihu kwa mbingu, walivaa shanga zilizotengenezwa kwa lapis lazuli na wakati walipotoa dhabihu kwa ardhi, walivaa majoho ya kifalme na wakati huo walikuwa wakivaa shanga zozote kwa hiari yao.
Shanga za Mashariki ziliruhusiwa kuvaliwa na wafalme, mama na wake zao tu. Shanga za kifalme na tepe za hariri za watoto wa wafalme na jamaa zao wa karibu ni za rangi ya dhahabu; na shanga na tepe za hariri za maofisa wengine ni za rangi nyeusi.
Urefu wa ushanga wa kifalme wa kyanite unaoonekana katika picha ni sentimita 160, ilitungwa kwa kutumia shanga 108; kichwa chake cha Budda na pagoda yake ya Buddha vilitengenezwa kwa jasper; utepe wa hariri wa rangi ya manjano unaunganisha wingu la mgongoni lililotomewa rubi na jasper ya manjano. Jebu yake ilitomewa rubi; ina shanga tatu za jinianer za matumbawe ambazo chini ya ke zinaning'inia jebu za rubi. Malighafi za kutengeneza ushanga huu wa kifalme ni bora na ufundi wa kuutengeneza ni wa hali ya juu. Mfalme wa Enzi ya Qing na mkewe waliwahi kuuvaa ushanga huo siku za kawaida.
Idhaa ya Kiswahili 2004-05-21
|