Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-24 22:11:01    
Chakula chenye jine iliyohamishwa ni salama ?

cri
    Kamati ya Umoja wa Ulaya tarehe 19 mwezi May iliidhinisha rasmi mauzo ya mahindi yaliyoingizwa kutoka nje yenye jin (gene) iliyohamishwa aina ya Bt-11 pamoja na chakula cha makopo kilichotengenezwa kutokana na mahindi hayo. Hii ni mara kwa kwanza kwa Umoja wa Ulaya kuidhinisha nchi wanachama wake kuuza kwa watu wake chakula chenye jin iliyohamishwa baada ya mwaka 1998. Uamuzi huo umesababisha mgongano wa maoni na wasiwasi wa watu wengi wa nchi wanachama wa umoja huo. Kitu kinachofuatiliwa hasa katika mabishano hayo ni kwamba chakula chenye jin iliyohamishiwa ni salama?

    Chakula chenye jin iliyohamishwa ni chakula kilichoongezwa jin iliyohamishwa kutoka nje au kuondolewa jin yake kiliyokuwa nayo kwa teknolojia ya jin. Watu wengi wana wasiwasi kwamba baada ya kula chakula hicho jin hizo zilizohamishwa zitaweza kuingia mwilini mwa binadamu. Wazo hilo ni la kosa kutokana na kutofahamu kazi inayofanya jin. Karibu kina aina ya chakula ni chenye jin, hata jin hizo zilitoka wapi, DNA ambazo ni kitu kinachotengeneza jin, baada ya kuingia mwilini mwa binadamu zitavunjwa na enzyme kuwa chembe ndogo mno ambazo hazitaweza kufanya nguvu ya urithi iliyotoka nje kuingia katika seti za jin za binadamu. Kutokana na ukweli huo, chakula chenye jin iliyohamishwa hakuna tofauti na chakula cha kawaida.

    Mambo mengine yaliyosababisha watu kuwa na wasiwasi juu ya chakula chenye jin iliyohamishwa ni pamoja na kwamba Chakula chenye jin iliyohamishwa huenda kitaleta vitu vipya vyenye madhara au kufanya mtu kuwa na sesitivu kwa kitu fulani; Mazao yenye jin iliyohamishwa ambayo inaweza kutengeneza vitu vya kemikali vinavyoweza kuua madudu, vitu hivyo vya kemikali huenda ni vyenye madhara kwa viumbe vingine na kudhuru afya za binadamu na mifugo; Mazao ya kilimo yenye jin iliyohamishwa na mimea ya mwitu yenye uhusiano na mazao ya kilimo huenda vitazaa mazao mengine chotara, ambayo yanajulikana kwa "uchafuzi wa jin"; Mazao ya kilimo yenye jin iliyohamishwa ambayo ina uwezo wa kuua madudu, huenda yatafanya madudu kuwa na uwezo mkubwa zaidi juu ya sumu zilizotengenezwa na jin hiyo, na kuwa "super madudu" wapya.

    Kuhusu hatari hizo, baadhi yake zinaweza kuepushwa kwa usimamizi mwafaka, na baadhi ya hatari nyingine zitathibitishwa zaidi kwa utafiti wa kisayansi. Kupima kwa makini hali ya sumu na sensitivu ya chakula kunaweza kupunguza madhara ya chakula kwa afya ya binadamu. Wanasayansi hivi sasa wanafanya utafiti na majaribio juu ya athari kwa mazao ya kilimo yenye jin iliyohamishwa wakitarajia kubuni sera kutokana na takwimu sahihi ili kuzuia athari mbaya.

    Ukweli ni kwamba katika mazingira ya kiasili mabadiliko ya jin hayakusimama hata kidogo, mazao ya kilimo wanayolima siku hizi, ni matokeo ya mabadiliko ya kimaumbile na uchatuzi wa binadamu katika miaka elfu kadhaa zilizopita. Wakati tunapokula chakula, tunakula pamoja na jin za kuua madudu pamoja na jin za aina nyingine za mimea ya mwitu yenye uhusiano na mazao hayo, isipokuwa watu hawakufikiria.

    Habari zinasema kuwa aina za vyakula vieyenye jin zilizohamishwa kikiwemo chakula cha watoto wachanga, ambavyo hivi sasa zinauzwa nchini Marekani zinakaribia 4000 na kutumiwa na watu zaidi ya milioni 200, lakini katika muda wa karibu miaka 9 iliyopita, hakukuwa na habari hata moja iliyotangazwa na vyombo vya habari kuhusu tatizo la usalama wa chakula chenye jin iliyohamishwa.

   Teknolojia ya uhamishaji wa jin ni ya kwango cha juu, ambayo inaweza kuongeza uzalishaji, kupunguza matumzi ya madawa ya kilimo. Kuhusu chakula chenye jin iliyohamishwa, tunapaswa kuwa na msimamo wa kisayansi, wala siyo kukikataza kwa urahisi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-24