Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-26 16:08:01    
Kubana matumizi ya maji kwa njia ya kisayansi nchini China

cri
Bw. Liu Xin mwenye umri wa miaka 65, anaishi mjini Beijing. Tangu alipostaafu kazi, alianza kufanya juhudi za kubana matumizi ya maji kwa njia ya kisayansi nyumbani kwake, vyombo vyote vya maji nyumb ani kwake vilibadilishwa kuwa vyombo vya kubana matumizi ya maji katika maisha yake ya kawaida anapenda kubadilishana maarifa na jirani zake kuhusu kubana matumizi ya maji. Alisema kuwa, kubana matumizi ya maji si kama tu ni suala la kuokoa fedha, bali pia ni suala linalohusika na kuokoa mali asili ya maji. 

Hivi sasa mjini Beijing, kuna watu wengi wanafanya kama Bw LiuXin ambao wanatumia akili zao kubana matumizi ya maji. Katika maisha ya kawaida, Bw. Liu Xin hawezi kumwanga ovyoovyo maji yaliyoosha mboga, alitumia maji hayo kumwagilia maua. Baada ya kurekebishwa, matumizi ya maji chooni nyumbani kwake yalipungua kwa 30% kuliko zamani. Alisema kuwa, zamani matumizi ya maji ya nyumbani kwake yalikuwa tani 70 kwa miezi mitatu, lakini sasa Tani 50 zinatosha. Anasema:

" mali asili ya maji ni ya thamani sana, na hili siyo suala la fedha. Madhumuni ya kubana matumizi ya maji siyo kuokoa fedha tu, unuhimu wake ni kuhifhadhi mali asiri ya maji.   Maji ni hitaji la lazima kwa maisha ya watu. Watu wakitaka kuendelea kuishi duniani wanapaswa kuokoa mali asili ya maji, huo ni wajibu mkubwa kwa watu wote duniani."

    Hivi sasa Beijing inakabiliwa na suala la ukosefu mkubwa wa maji, kila mtu wa Beijing anaweza kumiliki maji mita 300 tu za ujazo. Hali hiyo inakwamisha sana maendeleo ya mji wa Beijing wenye watu milioni 13. kuhusu suala hilo, wakazi wa kawaida wa Beijing au wataalamu na wanasayansi, wote wana maoni ya pamoja kuwa, kubana matumizi ya maji kwa njia ya kisayansi ni njia lazima ya kwa kutatua suala hilo. Miaka ya hivi karibuni, serikali ya Beijing ilichukua hatua mbalimbali za kubana matumizi ya maji, ambapo iliwaelekeza wakazi wa Beijing kubana matumizi ya maji kwa njia mbalimbali za kisayansi.

    Chang Feng Holiday inn ni Hoteli ya nyota 4 mjini Beijing. Hoteli hiyo ina vyombo maalumu vya kushughulikia maji taka. Kila siku, baada ya kusafishwa kwa mashine hizo, maji kutoka vyumba mbali mbali yanarudishwa kutumiwa tena vyooni. Matokeo yalionesha kuwa, vyombo hivyo vya kushughulikia maji taka vililetea faida kubwa kwa hoteli, mwaka uliopita walitumia vyombo hivyo kusafisha maji taka tani elfu 30, inaokoa Yuan laki 2. Msimamizi mkuu wa ufundi wa kusafisha maji taka wa hoteli hiyo Bw. Li Weiping alisema kuwa, kubana matumizi ya maji si kama tu kunaleta faida kwa hoteli, bali pia kunaokoa mali asili ya maji. Anasema:

    " Hoteli hiyo ilipoanza kujengwa ilitumia Yuan milioni 1 kuweka vyombo vya kushuhulikia maji taka, ili kusafisha maji kutoka vyumba mbalimbali ya hoteli na kuyatumia tena. Kwa mfano, maji yaliyotumiwa katika vyumba vyote kwa kuoga yalishughulikiwa na kutumika tena katika vyooni.

    Ili kuimarisha zaidi kazi ya kubana matumizi ya maji, hoteli hiyo iliweka vyombo vya kuokoa maji katika kila chumba na viliweza kuokoa 70% ya maji kuliko zamani. Beijing ni mji wenye tatizo kubwa la upungufu wa maji, na hali hiyo ya upungufu wa maji iko nchini kote China. Mbali na hayo, maeneo ya ukosefu wa maji yaliongeza siku hadi siku katika miji mingi nchini China. Hali hiyo ilikwamisha sana maendeleo ya uchumi wa China. Kuhusu hali hiyo, idara husika za serikali ya China zilikuwa na mkutano wa kazi za kubana mahitaji ya maji, kuzitaka sehemu mbalimbali za China kukuza teknolojia na vyombo vya kubana matumizi ya maji. Katika majengo yote mapya kulitakiwa kuwekwa vyombo vya maji vinavyofaa vyenye kiwango cha kubana matumizi ya maji; majengo yasiyokuwa na vyombo hivyo, yalipaswa kurekebishwa kabla ya mwishoni mwa mwaka 2005. Kamati ya mageuzi ya maendeleo ya China pia ilianzisha kazi ya kubana matumizi ya maji mijini na kutumia maji ya baharini kwa njia ya kisayansi na kiteknolojia. Naibu mkuu wa idara ya mali asli ya maji katika wizara ya utumiaji wa maji ya China ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Ofisi ya kazi ya kubana matumizi ya maji za China Bw. Meng Zhuo alisema kuwa, wakati wa kueneza kazi ya kuokoa maji kwa kisayansi, pia ilianzisha mfumo wa kubana matumizi ya maji kwa njia ya kichumi. Anasema :

    " kazi muhimu kwa China ni kutatua suala la upungufu wa maji, kuokoa maji na kutumia maji kwa uangalifu. Kwa kuambatana na ongezeko la idadi ya watu na maendeleo makubwa ya uchumi na jamii ya China, na maendeleo ya kasi ya viwanda, mahitaji ya maji nchini China yameongezeka zaidi, migogoro kati ya utoaji na mahitaji ya maji na mazingira ya mali aslri ya maji imeonekana dhahiri siku hadi siku. Kutokana na hali hiyo, katika kazi za siku za usoni, tutachukua hatua zilizotofautiana na njia ya zamani, tutaongeza bei za matumizi ya maji, ili kuwawezesha watu kubana matumizi ya maji.

    Hivi sasa jamii ya China imekuwa na maoni ya pamoja kwamba, kulegeza upungufu wa maji na kuhakikisha usalama wa utoaji wa maji, njia yake yenye ufanisi mkubwa ni kubana matumizi ya maji kwa pande zote na kwa njia ya kisayansi. wakati huo huo, zilitumia sheria, uchumi, utawala na teknolojia ili kuanzisha utaratibu kamili wa kubana matumizi ya maji, kukuza vyombo vya kubana matumizi ya maji na kuanzisha mfumo halali wa bei za maji ili kusukuma mbele harakati za kubana matumizi ya maji nchini kote China.

Idhaa ya kiswahili 2004-5-26