Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-27 22:14:54    
Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Vyama vya Mwezi Mwandamo Mwekundu

cri
    Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Vyama vya Mwezi Mwandamo Mwekundu(International Federation of Red Cross and Red Crescent Societies) ni shirika la ubinadamu lililo huru na lisilo la kiserikali, na ni Shirikisho la kimataifa linaloshirikisha vyama vya msalaba mwenkundu na mwezi mwandamo mwekundu vya nchi mbalimbali. Makao makuu yake yako mjini Geneva. Zamani liliitwa Shirikisho la Vyama vya Msalaba Mwekundu. Kutokana na kujiunga kwa vyama vya mwezi mwandamo mwekundu vya nchi za kiislam na kuongezeka kwa idadi ya wanachama, mwezi Oktoba mwaka 1983,katika mkutano wa kikao cha tatu uliofanyika mjini Geneva, Shirika la Vyama vya Msalaba Mwekundu lilibadilisha jina lake kuwa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Vyama vya Mwezi Mwandamo Mwekundu.

    Madhumuni ya Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Vyama vya Mwezi Mwandamo Mwekundu ni kufanya shughuli za hisani wakati wa vita, na kulinda amani kwa kutoa huduma za ubinadamu. Shirikisho hilo huwa linafanya mkutano wa kimataifa kila baada ya miaka minne. China ilijiunga na shirikisho hilo tarehe 8 mwezi Julai mwaka 1919.

    Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (International Committee of the Red Cross) ni chama cha msalaba mwekundu kilichoasisiwa mapema kabisa duniani. Mwanzilishi wake ni Henry Dunan wa Uswiz. Mwaka 1863, Dunan na wenzake walianzisha Kamati ya kimataifa ya kuwasaidia askari waliojeruhiwa mjini Geneva mwaka 1880, kamati hiyo ilibadilishwa kwa jina la Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu.

    Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ilikuwa chama cha kiraia cha Uswiz, ilipaswa kufuata sheria za Uswiz. Wanachama wote wa kamati hiyo walikuwa watu maarufu wa Uswiz, na hawakuweza kuzidi 25.

    Madhumuni ya kamati hiyo ni kufanya shughuli za hisani wakati wa vita. Kwa mujibu wa kanuni zilizohusika za Mkataba wa Geneva, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ikiwa kundi lisilopendelea upande wowote wakati wa kutoa ulinzi na msaada kwa watu waliokumbwa na vita, ilishughulikia mashitaka yaliyokwenda kinyume na mkataba wa ubinadamu, kufanya juhudi zake katika kuboresha na kueneza mkataba wa ubinadamu, kufanya ushirikiano na vyama vya nchi mbalimbali vya msalaba mwekundu, vikosi vya matibabu vya majeshi, na mashirika mengine yaliyohusika katika kuwaandaa madaktari na wauguzi , na kuendeleza vifaa vya kimatibabu.

    Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ni shirika mwanzilishi la Chama cha Msalaba Mwekundu. Vyama vya msalaba mwekundu au vyama vya mwezi mwandamo mwekundu vilivyoanzishwa upya au kurekebishwa na nchi mbalimbali haviwezi kuwa mwanachama wa Chama cha Kimataifa cha Msalaba Mwekundu ila tu kutambuliwa rasmi na kamati hiyo.

    Shirika lenye madaraka ya juu kabisa la Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ni mkutano wa wajumbe wote uliokuwa ukifanyika kila mwaka.

    Tarehe 15 Januari mwaka 1912, chama cha msalaba mwekundu cha China kilitambuliwa rasmi na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu. Mwanzoni mwa miaka ya 1950, chama cha msalaba mwekundu cha China kilitambuliwa tena baada ya kurekebishwa.

    Harakati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwandamo Mwekundu (International Red Cross and Red Crescent Movement)

    Harakati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwandamo Mwekundu ni shirika la ubinadamu lililo huru duniani, iliundwa na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Vyama vya Mwezi Mwandamo Mwekundu, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, na vyama vya msalaba mwekundu na vyama vya mwezi mwandamo mwekundu vya nchi mbalimbali. Makao makuu yake yako Geneva.

    Mwezi Oktoba mwaka 1863, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ilifanya mkutano wa kimataifa ulioshirikisha wajumbe kutoka nchi 16 huko Geneva, kufanya uamuzi wa kuanzisha kamati ya waokoaji katika nchi mbalimbali ili kukisaidia kikosi cha tiba cha jeshi wakati wa vita, na kuvaa tepe nyeupe ya namna moja mkononi iliyochorwa msalaba mwekundu. Tarehe 22 Agosti ya mwaka 1864, Mkataba wa Geneva wa kwanza wa kuboresha hali ya majeruhi wa jeshi la nchi kavu ulitiliwa saini mjini Geneva. Harakati hizo zilitambulika rasmi na mkataba wa kimataifa. Mwaka 1928, katiba ya msalaba mwekundu wa kimataifa ilitungwa. Mwaka 1986, kwenye mkutano wake wa 25, msalaba mwekundu wa kimataifa ulibadilishwa kwa jina la sasa la Harakati za Kimataifa za Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwandamo Mwekundu.

    Madhumuni ya harakati hizo ni kuwa, shughuli zake zote zinapaswa kufuata kanuni 7 za kimsingi za msalaba mwekundu, yaani ubinadamu, haki, msimamo wa kutofungamana na upande wowote, kujitawala, kutoa huduma kwa hiari, vitendo vya pamoja na kuhamasisha watu wa dunia nzima.

    Mamlaka ya juu ya kufanya uamuzi ni mkutano mkuu wa kimataifa wa msalaba mwekundu na mwezi mwandamo mwekundu, ambao wajumbe wake rasmi walitoka vyama vya msalaba mwekundu na vyama vya mwezi mwandamo mwekundu vya nchi mbalimbali vilivyotambuliwa rasmi, wajumbe kutoka Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, wajumbe kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Vyama vya Mwezi Mwandamo Mwekundu, na wajumbe wa serikali wa nchi zilizotia saini mkataba wa Geneva.

    China ilijiunga na mkutano mkuu huo mwaka 1919.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-27