Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-01 19:11:52    
Wafanya biashara wa kigeni wavutiwa na Yunnan, China

cri
    Hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu, kampuni ya vifaa vya ujenzi na mapambo ya nyumba ya B&Q ya Uingereza, ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa barani Ulaya kwa mauzo ya vifaa vya ujenzi na mapambo, imefungua matawi 18 nchini China, bara.

    Super market ya Kunming iliyojegwa na kampuni hiyo mkoani Yunan, sehemu ya kusini magharibi ya China ni ya mbali zaidi na makao makuu yake yaliyoko China ikilinganishwa na matawi mengine ya super market hiyo. Meneja mkuu wa super market ya ubia ya B&Q, Kunming Bw. Hu Yuming hivi karibuni alisema kuwa sababu ya B&Q kuanzisha super market katika mji wa Kunming ni kuvutiwa na mustakabali wa maendeleo ya mji huo ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Yunnan.

    "Kustawisha mkoa wa Yunnan ni moja muhimu ya sera za serikali ya China za kustawisha sehemu ya magharibi, hivyo tumeuchagua mji wa Kunming kuwa kituo chetu cha msingi. Kunming ni mji wa utalii, ambao baadaye utaendelezwa kuwa mji wa kisasa duniani. Kabla ya kuanzisha tawi letu hapa, tulifanya uchunguzi na tuna imani kubwa na mustakabali wa Kunming."

    Yunnan ni moja ya mikoa inayonufaika kwa sera za kustawisha sehemu ya magharibi ya China. Mkoa huo una mpaka wa zaidi ya kilomita 4,000 kati yake na Vietnam, Laos na Myanmar (Burma). Mkoa huu una mimea na wanyama pori wa aina nyingi na kusifiwa na wataalamu wa mimea kuwa "bohari la gene za viumbe duniani". Ubora wa kijiografia, rasilimali pamoja na sera nzuri za ufunguaji mlango kutokana na harakati za kustawisha sehemu ya magharibi, vimefanya Yunnan kuwa soko la uwekezaji linalovutia wageni wengi.

    Tunaweza kuchulia mfano wa B&Q, ambayo tawi lake la Kunming lilifunguliwa mwezi Septemba mwaka 2002. Meneja mkuu Hu Yumin alisema kuwa katika miaka miwili iliyopita, super market yao ilipata maendeleo ya kasi, mauzo yake ya mwaka huu yamekuwa na ongezeko la zaidi ya 50% likilinganishwa na mwaka uliopita. Bw. Hu alisema kuwa mafanikio ya B&Q yanatokana na uungaji mkono wa serikali ya huko, na vile vile, bidhaa zao za aina nyingi na mfumo bora wa huduma za baada ya bidhaa kuuzwa, viliongeza sifa za super market yao na kupendwa na wakazi wa huko. Bibi Huang Li ambaye alikwenda huko kununua mbao za sakafu ya nyumba yake kwa kupanda basi kwa zaidi ya saa moja, alisema,

    "Bidhaa zinazouzwa kwenye Super market ya B&Q ni nzuri, na huduma zao pia ni nzuri. Bidhaa tunazonunua hapa B&Q, zinaweza kurudishwa ikiwa ni hafifu au zenye dosari. Mbao zilizobaki baada kazi za sakafu kukamilishwa, zinaweza kurudishwa. Sisi hatuwezi kufahamu sana vitu tunavyotumia, lakini baada ya kuwauliza wauzaji, wanaelewa vizuri vitu tunavyotaka kununua."

    Mbali na super market ya B&Q, kampuni ya bia ya Dali ya Carlsberg ni ya kampuni ya Denmark peke yake ambayo iliichukua kampuni ya bia ya Dali mkoani Yunnan Septemba mwaka uliopita ambayo ilikuwa kampuni ya kwanza kwa ukubwa miongoni mwa makampuni ya bia ya serikali. Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya zamani ya Dali, Bw. Yang Zebiao ambaye hivi sasa ni meneja mkuu wa kampuni ya bia ya Dali ya Carlsberg alisema,

    "Carlsberg ambayo imejenga viwanda katika nchi za Asia ya kusini mashariki, zikiwemo Vietnam, Laos, Brunei, Malaysia na Thailand, sasa inataka kujenga mfumo wa masoko na kufanikisha mkakati wake barani Asia, hususan nchini China. Licha ya hayo, Carlsberg inapendezwa na maji safi yasiyochafuliwa na kikemikali, ambayo ni laini na yanayofaa sana kwa utengenezaji wa bia."

    Bwana Yang alisema kuwa mawazo yetu yamebadilika sana kutoka kuwa wafanyakazi wa kawaida hadi kuwa viongozi wa menejimenti. Alisema pia kuwa Carlsberg inazingatia sana kutoa mafunzo ya kazi kwa wafanyakazi wake ambayo ni pamoja na kazi za ofisini, kompyuta, lugha ya Kiingereza na teknolojia inayotumika katika kazi zao.

    Kampuni ya Ima iliyoanzishwa katika mji wa Dali mkoani Yunnan ni ya ubia, ambayo mwekezaji kutoka nje ni kampuni ya Ima inayotengeneza viungo vya chakula vikiwa ni pamoja na Uyoga pori na mboga kavu ambazo zinauzwa zaidi nchini Ufaransa, Italia na Marekani. Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Wang Jian alisema kuwa kampuni ya Ima ilianza kujiandaa kutengeneza chakula cha Uyoga pori miaka 12 iliyopita hapa nchini, na iliwekeza na kujenga kiwanda chake cha kwanza mjini Dali miaka mitatu iliyopita. Alisema kuwa sababu ya kampuni ya Ima kuchagua mji wa Dali kuwekeza vitega uchumi, inatokana hasa na kupendezwa na rasilimali zake nzuri. Bw. Wang alisema kuwa hadi hivi sasa, kampuni yao imesafirisha nje tani 1,500 za uyoga pori ambazo zimewaletea pato la fedha za kigeni dola milioni 7 hivi. Jambo linalowafurahisha zaidi ni kwamba baada ya kampuni yao kununua uyoga pori kutoka kwa wakazi wa vijijini, kiwango cha maisha yao kimekuwa kikiinuka kwa udhahiri.

    Pamoja na maendeleo ya uchumi na kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji ya Yunnan, wafanya biashara wengi kutoka nchi za nje wanakwenda kuwekeza huko. Kutokana na takwimu, hadi kufikia mwishoni mwa mwishoni mwa mwaka uliopita, idadi ya makampuni wa kigeni yaliyowekeza mkoani Yunnan ni zaidi ya 2,400.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-01