Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-03 20:46:53    
China kujitahidi kuboresha huduma za maji vijijini

cri
    Kutokana na hali ya upungufu wa uwezo wa miundo mbinu ya utoaji wa huduma za maji katika vijiji vya China, hivi karibuni serikali ya China imefanya mpango na itafanya juhudi za kuboresha miundo mbinu ya kutoa huduma za maji vijijini, kuinua kiwango cha ubora wa maji na kueneza huduma hizo kutoka mijini hadi vijijini.

    Kumbukumbu za Wizara ya Ujenzi ya China zinaonesha kuwa hivi sasa miji mikubwa na ya kiasi nchini China imetatua kimsingi tatizo la upungufu wa miundombinu ya utoaji huduma za maji, lakini ujenzi wa miundombinu vijijini unaendelea polepole. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2002, matumizi ya maji ya bomba mijini yalifikia 77.85, lakini matumizi ya maji ya bomba vijijini yalifikia 48.81 % tu, na vijiji vilivyotumia maji ya bomba vilikuwa 19.63% ya vijiji vyote nchini China, na vijiji vilivyojengewa miundombinu ya huduma za maji vilikuwa 16.79 % ya vijiji vyote vya China.

    Ili kutatua tatizo hilo, baadhi ya sehemu zimeanza kujaribu kutekeleza utaratibu wa kutoa huduma za maji kutoka mijini hadi vijijini. Kuanzia mwaka 2000, katika mkoa wa Jiangsu, mahariki ya China, miji ya Suzhou, Wuxi na Changzhou ilianza mradi wa kufikisha huduma za maji vijijini kwa kufanya mageuzi ya ujenzi wa mabomba ya maji mijini na kuanzisha mitambo ya maji vijijini na kudhibiti matumizi ya maji yaliyoko chini ya ardhi, na ilihakikisha kila kijiji na kila familia inapata maji ya bomba.

    Baada ya kufanya juhudi za miaka mitatu, eneo la miji hiyo mitatu limeinua kiwango cha utoaji huduma za maji ya bomba katika vijiji vilivyopo katika eneo hilo. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2003, miji hiyo mitatu imefikisha maji yanayotumiwa na wakazi wa mijini kwenye vijiji 211 vyenye familia 2379, na wakulima milioni 5.6 ambao ni asilimia 69.8 wa wakulima wote waliopo katika sehemu za miji hiyo wamepata manufaa.

    Afisa wa Wizara ya Ujenzi ya China alisema kuwa mradi wa kueneza huduma za maji kutoka mijini hadi vijijini hivi sasa uko katika kipindi cha mwanzo kabisa, na umeanza kutekelezwa katika mikoa ya Jiangsu, Zhejiang na Guangdong, Mikoa ambayo inaendelea kiuchumi, kwani mikoa hiyo licha ya kuwa na hali nzuri ya miundombinu ya maji, pia ina utajiri mkubwa wa maji. Siku za baadaye mradi huo utaenezwa kwenye sehemu nyingine zenye hali mwafaka nchini China.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-03