Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-03 21:31:19    
Marubani wa Kike wa China

cri

   Tangu kuanzishwa kwa China mpya ilianzishwa mwaka 1949, China kwa jumla imewaandaa marubani wa kike  mia kadhaa,Miongoni mwao,kuna marubani wawili waliopewa nishaniya jeshi la anga, na wengine wanne wamepewa cheo cha kanali ,kati yao asilimia 65 ni marubani wa daraja maalumu au daraja la kwanza. Marubani wa kike wamewahi kuendesha aina 13 za ndege ikiwemo ndege ya jet yenye mwendo wa kasi sana, kutekeleza majukumu ya aina
mbalimbali, kufanya majaribio ya urukaji kwa aina mpya za ndege na kutoa mchango mkubwa katika ulinzi wa taifa
na ujenzi wa jeshi la anga la watu wa China.
    Kikundi cha kwanza chenye marubani wa kike 55 kiliandaliwa mwaka 1951. Wakati huo, hali ya mafunzo ya kurusha ndege yalikuwa sio mazuri, lakini wasichana wa China waliyakabili matatizo ya aina mbalimbali kwa moyo wa ukakamavu, na walihitimu shule kwa muda usiozidi mwaka mmoja tu. Katika siku ya kimataifa ya wanawake tarehe 8 Machi mwaka 2000, sherehe ya ukaguzi wa uwezo wao wa kurusha ndege ulifanyika kwenye uwanja wa ndege wa magharibi ya Beijing, Wakewa wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali walioko nchini China na waandishi wa habari wa nchini China na
wa ng'ambo walishuhudia maonesho yao. Maonesho yao yalikuwa ya mafanikio makubwa.Katika historia ya miaka 50 hivi, marubani wa kike. Walionesha uhodari mkubwa angani, waliwahi kushiriki katika vita vya kuisaidia Korea ya Kaskazini dhidi ya Marekani mwaka 1950; wamewahi kupeleka vifaa vya msaada kwa watu waliokumbwa na maafa ya mafuriko, ukame au tetemko la ardhi; wamewahi kutekeleza majukumu ya kuangusha theluji na kutengeneza mvua ili kuondoa
ukame, kuondoa mvua na mvuke kwa lengo maalum; wamewahi kufanya majaribio ya kurusha ndege mpya za aina mbalimbali; na pia wamewahi kuwapeleka viongozi wa China na wa nchi za nje. Katika mazoezi ya kijeshi, marubani
wa kike pia walionesha uhodari na ustadi wao kama marubani wanaume walivyofanya. Zaidi ya hayo, marubani hao wa China walimudu kutekeleza kazi nzito za aina mbalimbali kama vile kurusha ndege kwa dharura, kutawanya mbegu na miti milimani, pamoja na kuzima moto kwenye misitu. Marubani wa kike wa China pia ni mama wa watoto , ni wake na ni mabinti, wanawapenda watoto, waume na familia zao, lakini wanaipenda anga zaidi, na wameweka historia nzuri katika ukurasa wa maisha yao.
      Bibi Wu Xiumei ni rubani aliyeendesha ndege kwa miaka mingi kuliko marubani wengine wa kike wa kikundi cha kwanza.Katika maisha yake ya kuruka na ndege; kwa miaka 33,ameruka kwa saa 3865 kwa usalama, umbali ambao ni sawana kuzunguka dunia mara 24.kutokana na kupenda kurusha ndege baada ya kufikia umri wa kustaafu,
hakutaka kuagana na ndege. Lakini tarehe 28 mwezi Machi mwaka 1984, alipaswa kuagana na urukaji ndege kutokana na utaratibu uliowekwa.
    Bibi Wang Yun alikuwa rubani wa kike wa kwanza nchini China kurusha kwa ndege aina ya Jet. Aliwahi kutekeleza majukumu mengi ya kuruka kwa ndege maalum ya kuwapeleka viongozi wa China na wa ng'ambo. Tarehe 18 Desemba mwaka 1974, rais wa Zaire ya zamani Mobutu alipoizuru China, alisafiri kwa ndege maalum aliyopangiwa na serikali ya China. Rais huyo aliyewahikuwa rubani wa ndege ya kudondosha mabomu alishangaa kugundua kuwa, rubani wake alikuwa mwanamke. Wakati ndege ilipotua kwa usalama kwenye uwanja wa ndege, rais Mobutu alimshika mkono Bibi Wangu Yunna kumsifukwa ustadi wake.
    Jaribio la kurusha ndege kisayansi na kiutafiti ni la hatari sana, kazi hii mara nyingi huwa inafanywa na marubani
wanaume. Bibi Zhang Yumei alikuwa rubani wa kike wa kwanza kufanya kazi hiyo. Katika kipindi cha miaka 10 toka 1984
hadi 1994, alishiriki katika majaribio ya namna hiyo zaidi ya mia moja ,na kutekeleza majaribio muhimu 15 ya urukaji wa kisayansi na kiutafiti, alijisikia vizuri sana.
    Bibi Yue Xichui alikuwa kamanda mdogo wa kwanza wa kike wa divesheni ya jeshi la anga la China. Yeye pia alipewa nishani .Katika maisha yake ya urukaji ndege, aliruka angani kwa saa 6000, yeye ni rubani wa kwanza nchini China kudondosha theluji na kuondoa mvua kwa nguvu ya binadmu. Akiwa mwakilishi wa marubani wa kike aliwahi kukutana  hayati Mao Zedong, hayati Zhou Enlai na viongozi wengineo wa China. Mwaka 1992, alichaguliwa kuwa mjumbe wa bunge laumma la 14 la China.
    Sasa marubani wa kike wa kikundi cha saba wameandaliwa, kama marubani wa kike wa kikundi cha kwanza ,wote wanapenda sana urubani. wanaandika ukurasa wao wa maisha kwa moyo wa ushujaa.

Idhaa ya kiswahili 2004-06-03