Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-04 21:29:35    
Kampuni ya Tiens ya China

cri
    Kampuni ya Tiens ya China ni kampuni kubwa ambayo imekuwa matawi mengi katika nchi za nje. Kampuni hiyo inashughulikia hali bidhaa zinazosaidia afya ya watu. Tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo kuanzishwa mwaka 1995, kampuni hiyo ina shughuli katika nchi na sehemu zaidi ya 170 ulimwenguni. Kati ya matawi mbalimbali, 22 yako barani Afrika. Hivi karibuni, Kampuni ya Tiens ilifanya mkutano wa 3 wa wafanyabiashara wa Afrika na sehemu ya Mashariki ya Kati, huko Nairobi Kenya. Wakati wa mkutano huo, mwandishi wetu wa habari alimhoji meneja mkuu wa Idara ya Afrika na Mashariki ya kati ya kampuni hiyo Bw. Zhao Yanming.

    Bw. Zhao Yanming ambaye ni meneja mkuu wa Idara ya Afrika na sehemu ya Mashariki ya kati katika kampuni ya Tiens ana umri wa miaka 50 na kitu. Amefanya kazi barani Afrika kwa miaka minne. Bw. Zhao alieleza kuwa, biashara muhimu ya Kampuni ya Tiens barani Afrika ni bidhaa zinazosaidia afya. Tangu kampuni hiyo kuanzisha tawi lake la kwanza nchini Afrika ya Kusini mwaka 1998, kampuni hiyo ilishinda kampuni wapinzani wake kwa ubora wa bidhaa zake, na kufanikiwa kuingia katika soko la nchi hiyo. Hivi sasa, kampuni hiyo ina wauzaji wake laki 2.7 barani Afrika, ambapo thamani ya uuzaji inafikia milioni 3.8 kila mwezi. Mafanikio hayo ni muujiza kwa kampuni mpya. Bw. Zhao anasema:

    "Kampuni ya Tiens kufuatiliwa na kukaribishwa kwenye wafanya biashara na wateja barani Afrika kutokana na sababu tatu."

    Kwanza, wananchi wa China na Afrika wana urafiki mkubwa. China na nchi za Afrika zote ni nchi zinazoendelea, pande hizo mbili zina sauti ya pmoja katika mambo mbalimbali ya kimataifa. Siku zote China inajitahidi kusaidia nchi za Afrika, wakati waafrika wana urafiki mkubwa na China. Hali hii inasaidia kampuni za China kupata maendeleo barani Afrika.

    Aidha, sifa nzuri ya bidhaa ni sababu nyingine kwa kampuni hiyo kupata mafanikio barani Afrika. Bw. Zhao alieleza kuwa, hivi sasa Kampuni ya Tiens inauza bidhaa zake bora barani Afrika, kati ya bidhaa hizo, nyingi zinaweza kusaidia watu kuongeza nguvu za kupambana na maradhi. Bidhaa hizo pia zinasaidia sana wagonjwa wa Ukimwi wa Afrika. Licha ya hayo, bidhaa za kutia elementi ya kalisi na kupunguza umeme vilevile zinakaribishwa na watu wa Afrika.

    Mbali na hayo, Kampuni ya Tiens ina wafanyakazi wenye juhudi kubwa barani Afrika. Bw. Zhao alisema kuwa, hivi sasa, kampuni hiyo ina waajiriwa wapatao 70 barani Afrika, ambao wanajitahidi kwa pamoja na wafanyakazi wenyeji, na kutoa mchango mkubwa kwa mafanikio ya Kampuni ya Tiens.

    Bw. Zhao alieleza kuwa, Kampuni ya Tiens inashikilia kanuni ya kunufanishana kwa pande zote mbili. Kwa upande mmoja, bidhaa za kampuni ya Tiens zinaleta afya njema kwa watu wa Afrika. Kwa upande mwingine, kampuni hiyo inatoa fedha nyingi za ushuru kwa serikali za nchi za Afrika. Mbali na hayo, Kampuni hiyo imewaajiri wenyeji wapatao laki 2.7 barani Afrika, imetoa mchango mkubwa kwa utatuzi wa ajira wa huko.

    Bw. Zhao alisema kuwa, Kampuni ya Tiens inazingatia sana kazi ya hisani katika sehemu hizo. Katika miaka kadhaa iliyopita, kampuni ya Tiens ilichangia na kujenga shule mbili nchini Ghana na Cote d'Ivoire, na kuzipa nchi za Afrika bidhaa zao zenye thamani ya dola za kimarekani laki kadhaa. Bidhaa hizo nyingi ziliwapa wagonjwa wa Ukimwi, wanawake na watoto wa nchi hizo. Bw. Zhao alisema kuwa, kutokana na maendeleo ya Kampuni ya Tiens barani Afrika, kampuni hiyo itajitahidi kujiunga na shughuli za hisani katika nchi hizo. Hivi sasa, makao makuu ya Kampuni ya Tiens yanaanzisha Mfuko wa hisani ya kimataifa, ili kuanzisha utaratibu kamilifu kwa vitendo hivyo vya hisani.

    Bw. Zhao alisisimka sana akizungumzia mipango ya maendeleo ya kampuni hiyo barani Afrika. Alisema, kazi muhimu zaidi kwa kampuni hiyo barani Afrika ni kuanzisha makao makuu ya kampuni hiyo katika sehemu ya Afrika Mashariki huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Hivi sasa, kampuni ya Tiens ilianzisha matawi nchini Kenya, Uganda na Tanzania, na itaanzisha matawi mapya nchini Sudan na Ethiopita hivi karibuni. Makao makuu katika sehemu ya Afrika Mashariki yatakapoanzishwa, yatashughulikia mipango ya uzalishaji na uuzaji, na mafundisho kwa wafanyakazi kwenye sehemu hiyo. Bw. Zhao anasema:

    "Mipango yetu katika muda mrefu ni kuanzisha taasisi ya utafiti barani Afrika, kufanya utafiti juu ya mitishamba ya nchi za Afrika, na kuifanya inufaishe wananchi wa Afrika."

    Alieleza kuwa, Afrika ina maliasili nyingi za mitishamba, wakati China ina uzoefu mwingi juu ya matumizi na uzalishaji wa madawa. Kampuni ya Tiens itaboresha mitishamba hiyo na kuifanya itumike katika nchi za Afrika. Kwani nia kubwa ya Kampuni ya Tiens ni kuimarisha ushirikiano na urafiki kati ya China na Afrika.

    Makamu wa rais wa Kenya Bw. Moody Awori akiwakilisha serikali ya Kenya alishiriki kwenye mkutano wa wafanyabiashara ya Afrika na sehemu ya Mashariki ya Kati ya Kampuni ya Tiens. Alitoa hotuba kwenye mkutano huo akisema:

    "Kampuni ya Tiens ni kampuni kubwa ya China ambayo ina matawi mengi katika nchi za nje. Kenya inakaribisha kampuni ya Tiens kuanzisha makao makuu yake katika sehemu ya Afrika Mashariki hapa Nairobi. Pia serikali ya Kenya inakaribisha kampuni nyingi zaidi kuwekeza barani Afrika.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-04