|
Vyombo 100 vya kulia vya kauri vya "maua ya bauhinia ya rangi" vilivyokusanywa hivi karibuni na Jumba la makumbusho ya historia ya China si vya kawaida.
Seti hii ya vyombo vya kulia inayowakilisha kiwango cha juu kabisa cha sanaa ya kauri ya leo ya China, ilitengenezwa kwa makini na wasanii, mafundi na wahandisi 100 wa Kiwanda cha Kauri ya Sanaa cha Jingdezhen. Wang Xiliang, msimamizi mkuu wa sanaa wakazi yakutengeneza seti hiyo, ni mmojawapo wa mabingwa wakuu 10 wa sanaa na kazi za mikono wa China. Mawazo ya wasanii ya kubuni seti hiyo yalitokana na maua ya bauhinia yaliyoko kwenye nembo ya Mkoa Maalumu wa Hong Kong na kusudi lao la awali lilikuwa ni zawadi yao kwa Mzee Deng Xiaoping aliyetoa mchango mkuu kwa ajili ya kuirejesha Hong Kong nchini China. Lakini kwa bahati mbaya Mzee Deng alifariki dunia wakati wasanii hawa walipokuwa bado wanaitengeneza. Kwa moyo wa kumkumbuka na bidii za miezi 8, hatimaye wasanii waliikamilisha seti hiyo ya sanaa na kuipeleka Jumba la Makumbusho ya Historia ya China liitunze.
Idhaa ya Kiswahili 2004-06-4
|