Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-07 21:29:28    
Ushirikiano kati ya Beijing, Tianjin na Tanggu waimarishwa

cri
    Ushirikiano kati ya miji ya Beijing na Tianjin umeimarishwa kwa haraka tangu wataalamu wa mambo ya uchumi watoe wazo la "Njia kuu mpya ya sayansi na teknolojia" mwezi Septemba mwaka jana. Kutokana na mkataba wa ushirikiano wa sayansi na teknolojia uliosainiwa mjini Beijing tarehe 22 May, miji hiyo miwili mikubwa itashirikiana katika kuanzisha mfumo mpya wa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia ambao kitovu chake kitakuwa ni miji ya Beijing na Tianjing, na kuendelezwa kuwa kituo muhimu kabisa cha uzalishaji mali kwa kutumia sayansi na teknolojia za kiwango cha juu nchini China.

    Mkataba huo wa ushirikiano wa sayansi na teknolojia unahusu mambo matano muhimu yakiwa ni pamoja na kutatua kwa ushirikiano masuala makubwa ya sayansi na teknolojia yanayotokea katika maendeleo ya uchumi na jamii na kuwa na ushirikiano mkubwa katika sekta za software, rasilimali za maji, hifadhi ya mazingira, kuweka usafi katika sehemu za umma, kilimo, magari yanayoendeshwa kwa nguvu za betri. Pili, kuhimiza ujenzi wa kanda ya uzalishaji wa teknolojia mpya za kiwango cha juu ya Beijing, Tianjin na Tanggu, kuanzisha kwa pamoja mazingira ya maendeleo ya ushirikiano wa kikanda, kubuni kwa pamoja mpango wa maendeleo na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uzalishaji mali wa teknolojia mpya ya kiwango cha juu. Tatu, ni kutumia kwa pamoja mafanikio ya sayansi na teknolojia na utaalamu, kufungua maabara na taasisi za utafiti wa teknolojia ya uhandisi za ngazi za taifa na mji. Nne, ni kujenga kwa pamoja maabara, vituo vya uhandisi vyenye hisa, vituo vya utafiti na wasomi waliohitimu elimu ya shahada ya udaktari. Tano, ni kuhamasisha uhamishaji wa mafanikio ya sayansi na teknolojia, wataalamu wa sayansi na teknolojia na uwekezaji vitega-uchumi.

    Miji ya Beijing na Tianjin si kama tu ni sehemu zenye wataalamu wengi hapa nchini, bali pia ina mifumo kamili ya kisasa ya uzalishaji wa teknolojia mpya ya kiwango cha juu. Kwenye kando mbili za barabara ya kasi inayounganisha Beijing, Tianjin na Tanggu kuna maeneo nane ya uzalishaji wa mali wa teknolojia mpya ya kiwango cha juu, ambayo kwa ujumla mapato yake ni zaidi ya Yuan bilioni 200, kiasi ambacho ni sawa na dola za kimarekani bilioni 24.4. Bidhaa zinazozalishwa zaidi ni pamoja na zana za elektroniki na upashanaji wa habari, dawa, mitambo inayotumia teknolojia za mwanga na elektroniki, vifaa vya aina mpya na nishati mpya ambazo zinatumika zaidi nchini China na duniani kwa ujumla. Wataalamu wanasema makampuni yaliyoko katika maeneo hayo yana uwezo mkubwa wa kuongeza mafanikio ya utafiti wa haki-miliki katika uzalishaji, ikiwa yatashirikiana ipasavyo, na yana uwezo mkubwa kabisa wa kuwa kituo cha uchumi wa kielimu na uzalishaji wa teknolojia mpya ya kiwango cha juu nchini.

    Kutokana na kuhimizwa na serikali za miji hiyo miwili, Beijing na Tianjin zinaelekea kushirikiana vizuri na kuwa na maendeleo kwa pamoja, hali ambayo ni tofauti na hapo awali, ambapo miji hiyo iligombea raslimali na ujenzi wa miradi. Baada ya kushirikiana pamoja kwa forodha na bandari za miji hiyo miwili, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing na Tianjin vinatumika kama kitu kimoja. Kutokana na kuidhinishwa na idara husika ya serikali, miji hiyo miwili imeamua kujenga barabara ya kasi kati yao. Kutokana na takwimu, tokea mwaka 2002, mikataba ya teknolojia iliyosainiwa kati ya miji hiyo miwili imekuwa na thamani ya Yuan bilioni 1.5 ambapo Beijing iliipatia Tianjin aina 1,300 za teknolojia na kuingiza aina 1,100 za teknolojia kutoka Tianjin.

    Kutokana na mikataba iliyosainiwa kati ya idara za sayansi na teknolojia za miji hiyo miwili katika maonesho ya sayansi yaliyofanyika mjini Beijing, miji hiyo miwili itaanzisha hivi karibuni ujenzi wa baadhi ya miradi ya kunufaishana. Mkurugenzi wa kituo cha utoaji ushauri mjini Beijing Bw. Niu Deming alisema kuwa, miji ya Beijing na Tianjin ina ubora ambao haupo katika miji mingine. Miji hiyo miwili bado ina uwezo wa kufanya ushirikiano katika mambo mengi sana. Alisema kuwa sekta ya huduma ya Beijing inaongoza kwa nchi nzima, lakini Tianjin ina nguvu kubwa katika uzalishaji bidhaa, hivyo miji hiyo miwili inaweza kunufaishana, na kanda hiyo itaweza kuwa kanda iliyoendelea katika dunia yetu.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-07