Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-08 21:28:47    
WHO yataka kuimarishwa kwa Mikakati ya kinga na tiba ya UKIMWI

cri
    Shirika la afya duniani WHO tarehe 11 Mei lilitoa taarifa kuhusu hali ya afya duniani mwaka 2004, taarifa hiyo ilisisitiza zaidi suala la ugonjwa wa ukimwi, na kusisitiza umuhimu wa mikakati ya kuchukua hatua za kinga, tiba, utafiti na ufuatiliaji wa muda mrefu.

    Taarifa hiyo inaona kuwa namna ya kukabiliana na ugonjwa wa UKIMWI ni kazi ya dharura kabisa katika sekta ya afya ya umma duniani kwa hivi sasa. Tangu ugonjwa wa ukimwi ugunduliwe mwanzoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, watu zaidi ya milioni 20 wamekufa kwa ugonjwa huo. Hivi sasa watu walioambukizwa virusi vya ukimwi wamefikia milioni 34 na wagonjwa wa ukimwi wamefikia milioni 46, na theluthi mbili ya watu hao wako barani Afrika, asilimia 20 ya watu hao wako barani Asia. Kwenye Bara zima la Afrika, kati ya kila watu wazima 12, mmoja ameambukizwa ugonjwa. Mwaka 2003 watu milioni 1 duniani kote walikufa kutokana ugonjwa wa ukimwi, na watu milioni 5 waliambukizwa virusi vya ukimwi. Kama watu hao walioambukizwa virusi vya ukimwi hawataweza kupata matibabu, kwa kawaida, baada ya miaka 9 hadi 11, wataonekana kuwa ni wagonjwa wa ukimwi. Hivi sasa ugonjwa wa ukimwi umekuwa chanzo kikubwa cha vifo vya watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 59 duniani. Katika miaka 20 iliyopita, watoto milioni 4 waliambukizwa virusi vya ukimwi, miongoni mwao, watoto laki 7 waliambukizwa virusi vya ukimwi mwaka 2003.

    Balaa hilo kubwa la UKIMWI limeleta changamoto kubwa kwa binadamu, matokeo mabaya ya ugonjwa wa ukimwi yameanza kuonekana tangu kugunduliwa kwa ukimwi zaidi ya miaka 20 iliyopita. Kwa nchi kadhaa zinazoendelea, ugonjwa huo umeleta balaa kwa jamii na uchumi, athari hiyo itaendelea kwa vizazi kadhaa vijavyo. Makadirio halisi yanaonesha kuwa, watu wazima wengi wa nchi kadhaa za kusini mwa Sahara wanakabiliwa na hali ya kukosa uwezo wa kufanya kazi, na wengine hata wanakabiria kufa. Kama hali hiyo haitaweza kudhibitiwa, basi uchumi wa nchi kadhaa utadidimia kabisa.,

    Taarifa ya WHO imeanisha kuwa, katika miaka 20 iliyopita, wataalamu wamepata mafanikio mengi makubwa katika utafiti wa ugonjwa wa UKIMWI. Ingawa bado hawajagundua dawa yenye mafanikio makubwa katika kutibu ugonjwa wa ukimwi, lakini wamepata dawa ya antiretroviral inayoweza kusaidia kurefusha maisha ya wagonjwa wa ukimwi kuishi maisha kwa muda mrefu zaidi na kuboresha maisha ya wagonjwa. Katika miaka ya hivi karibuni kiasi cha vifo vya wagonjwa wa UKIMWI kimepungua kwa kiasi kikubwa katika nchi zilizoendelea kwenye bara la Ulaya ya magharibi. Lakini dawa hiyo ni ghali sana kiasi cha kushindwa kununuliwa katika nchi zinazoendelea, miongoni mwa wagonjwa milioni 6 waliohitaji dawa hizo, ni laki 4 tu walioweza kupata matibabu. Shirika la WHO linaona kuwa, sasa umewadia wakati muhimu wa kuweza kudhibiti ugonjwa wa ugonjwa kwa binaadamu au la. Hivi sasa binadamu wanakabiliana na fursa ambayo haikutokea hapo awali katika kubadilisha mchakato wa maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi. Kwa maana hiyo binadamu wanaweza kubadilisha historia kutokana na vitendo vyao wenyewe.

    Hivyo Shirika la WHO, Shirika la kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa na Mfuko wa dunia nzima vilianzisha harakati za kuwapatia wagonjwa milioni 3 wa nchi zinazoendelea dawa za antiretroviral. Harakati hizo zinaeneza hatua kwa hatua uzoefu wa nchi za Botswana, Brazil, Senegal na Thailand. Katika harakati hizo, Shirika la WHO linatetea uongozi wa dunia nzima katika kinga na tiba ya ukimwi, kutetea na kuchukua hatua za pamoja, kuzitaka nchi mbalimbali zichukue hatua za dharura za kuziunga mkono kwa hatua mfululizo kazi hiyo, kutoa matibabu kwa kutumia wa dawa za antiretroviral, kuhakikisha utoaji wa dawa zinazoaminika na kutumia ujuzi mpya bila kusita, kugundua na kueneza uzoefu wenye ufanisi.

    Shirika la WHO limepanga kuwawezesha wagonjwa wengi zaidi wapatao milioni kadhaa wapate matibatu kwa dawa za antiretroviral.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-08