Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-08 21:34:21    
Tuifanye bahari iwe safi zaidi

cri
    Tarehe 5 mwezi Juni ni siku ya mazingira duniani. Kauli-mbiu ya mwaka huu ni "Kila mtu anawajibika kwa uhai wa bahari". Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa lilisema kuwa uchafuzi wa bahari ni moja ya balaa kubwa zinazotishia maisha ya binadamu. Kwa mujibu wa takwimu kutoka wizara ya mawasiliano, uchafuzi kwenye sehemu ambayo maji ya mto Lulu yanapoingia baharini, ni uchafuzi wa pili kwa ukubwa nchini China ukiufuatia ule wa kwenye ghuba ya bahari ya Bo hapa nchini.

    Pamoja na maendeleo ya kasi ya uchumi, China imekuwa nchi ya pili inayoagiza kwa wingi mafuta ya asili ya petroli ikiifuatia Marekani. Katika mwaka 2003 China iliagiza tani milioni 80 za mafuta kutoka nchi za nje, kiasi cha robo ya mafuta hayo yaliingia nchini kupitia bahari ya Kusini ya China, pwani ya mkoa wa Guangdong, hususan sehemu ya mwisho ya mto Lulu inayoungana na bahari ni sehemu zinazopita meli nyingi za mafuta. Habari kutoka idara ya mambo ya bahari ya wizara ya mawasiliano zinasema kuwa sehemu ya mwisho ya mto Lulu inaongoza kwa wingi wa usafirishaji wa vitu vya hatari ambavyo hufikia zaidi ya tani milioni 60 kwa mwaka yakiwemo mafuta zaidi ya tani milioni 20 na meli za mafuta laki mbili.

    Tangu kuanzishwa kwa idara ya mambo ya bahari ya mkoa wa Guangdong, idara hiyo ikifuata kanuni ya "uchukuzi salama na bahari safi" tangu ilipoanzishwa, inaimarisha usimamizi wa usalama wa usafirishaji baharini na kupunguza ipasavyo ajali za uchafuzi kwa maji ya bahari kutokana na kumwagika kwa mafuta ya petroli asili.

    Tokea mwaka 2001, idara hiyo inayoshughulikia mambo ya bahari ilipeleka meli ya upimaji kupima kina cha maji kwenye eneo la kilomita za mraba 2,087 la sehemu ya chini ya mto Lulu inapoungana na bahari. Kutokana na upimaji uliofanywa, idara hiyo ilipiga marufuku sehemu moja ya kutia nanga kwa meli, kurekebisha sehemu 19 zisizo nzuri sana za kutia nanga na kuongeza sehemu 11 za kutia nanga zikiwemo sehemu 5 kwa ajili ya meli zinazobeba vitu vya majimaji vyenye hatari, hatua ambayo imetatua vilivyo tatizo la kuzuia usafiri wa meli kwenye sehemu za kutia nanga.

    Ili kusawazisha utaratibu wa usafiri wa meli na kupunguza muda wa kupishana kwa meli, idara hiyo imeanzisha utaratibu wa kusafiri kwa njia mbalimbali kwa meli za uchukuzi na meli za uvuvi zinazopita kwenye eneo hilo zilikumbwa na ajali mara kwa mara hapo awali.

    Ongezeko kubwa la maendeleo ya uchumi wa Guangdong linaleta ustawi wa shughuli za kuongeza mafuta kwa meli zilizoko baharini. Vituo hivyo kuongeza mafuta vipatavyo 182 vimesambaa katika kandokando za mto Lulu na 80% ya vituo hivyo ni vya binafsi. Mwezi May mwaka uliopita, serikali ya Guangdong ilitoa " Agizo la muda wa kuongeza mafuta kwenye maji" na "kiwango cha teknolojia ya usalama kwa vituo vya kuongeza mafuta kwenye maji" ili kuimarisha usimamizi wa usalama na kupunguza hatari ya ajali.

    Hatua za dharura dhidi ya kuvuja mafuta kwa meli ni suala kubwa linalofautiliwa sana na nchi mbalimbali. Idara ya mambo ya baharini ya mkoa wa Guangdong ina meli moja maalumu yenye tani 800 yenye zana za kisasa ambazo zinaweza kunyonya maji yenye mafuta mita za ujazo 120 kwa saa. Mwanzoni mwa mwaka 2004, idara hiyo ilifanya marekebisho ya kukuza uwezo wa meli kubwa ya kuondoa uchafuzi pamoja na mfumo wa upashanaji habari wakati wa kutokea ajali. Licha ya hayo, idara hiyo inaunganisha vikosi vya kuondoa vitu vya uchafuzi vilivyoko katika eneo lile, na kuanzisha kundi maalumu lenye watu 120 na zana za kisasa ili kukabiliana na vitu vya uchafuzi vilivyosambaa kwenye maji ya bahari.

    Asubuhi mapema ya tarehe 29 Desemba mwaka 2003, meli ya mafuta iitwayo Xingtong iliyokuwa imebeba tani 2,000 za mafuta iligongana na meli iliyobeba makontena ijulikanayo kwa jina la Yonganzhou kwenye bahari inayoungana na sehemu ya mwisho ya mto Lulu, ambapo meli ya Xingtong iliyokuwa imebeba mafuta ya asili ya petroli ilipasuka na kusababisha tani 350 za mafuta kumwagika baharini. Idara ya mambo ya baharini ya mkoa wa Guangdong ilizindua mpango wa dharura, na katika muda wa dakika chache tu, watu husika pamoja na meli na ndege za doria walifika huko na kuanza kunyonya mafuta yaliyosambaa baharini. Katika ajali hiyo waliweza kurudisha maji yenye mafuta tani 230 na mafuta yaliyo takataka tani 25. Tarehe 30 mwezi Desemba ambayo ilikuwa ni siku ya pili baada ya kutokea ajali, wataalamu kutoka idara 7 zikiwa ni pamoja na idara za hifadhi ya mazingira za wizara ya mawasiliano, ya mkoa wa Guangdong na mji wa Guangzhou, walikwenda huko kupima maji ya bahari, waliona kuwa matokeo yake yalikuwa mazuri.

    Idara ya mambo ya baharini ya Guangdong ilitangulia kuanzisha mfumo wa utozaji wa fidia kwa ajali za meli za mafuta kuvuja hapa nchini, na kuanzisha utaratibu wa mfuko wa fedha za kuzuia uchafuzi katika sehemu ya chini ya mto Lulu, na kuwashawishi wenye meli za mafuta wakate bima ili kampuni ya bima iwalipe malipo ya fidia na kuondoa wa uchafuzi pindi itakapotokea ajali.

    "Taarifa ya ubora wa mazingira ya bahari ya China" inaonesha kuwa katika mwisho wa mwaka uliopita, sehemu ya chini ya Mtu Lulu ilichukua nafasi ya sita kwa wingi wa uchafuzi ikilinganishwa na hali ya zamani ambayo ilichukua nafasi ya pili nchini China.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-08