Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-09 21:01:59    
China yazingatia kulinda haki-miliki ya kielimu

cri
    Tarehe 26 mwezi Aprili mwaka huu ni "siku ya kulinda haki-miliki ya kielimu duniani" ya mwaka wa nne. "Siku ya kulinda haki-miliki ya kielimu duniani" ilithibitishwa kwa kauli moja kwenye mkutano mkuu wa 35 wa Shirika la Haki-miliki ya Kielimu Duniani kutokana na pendekezo lililotolewa kwa pamoja na China na Algeria. Lengo lake ni kuheshimu elimu, kufuatilia sayansi na kulinda haki-miliki ya kielimu ili kuwa na mazingira ya kisheria ya kuhamasisha uvumbuzi wa kielimu na kulinda haki-miliki ya kielimu. Kupendekeza kuweka "siku ya kulinda haki-miliki ya kielimu duniani", kunaonesha msimamo wazi wa serikali ya China wa kulind ahaki-miliki ya kielimu. Katika miaka ya karibuni, serikali ya China ilichukua hatua kubwa kadha wa kadha zenye ufanisi katika upande wa kulinda haki-miliki ya kielimu.

    Haki-miliki ya kielimu ni haki ambayo wafanya kazi wanastahili kuwa nayo juu ya matokeo ya kazi walizofanya kwa mujibu wa sheria. Ili kulinda matunda ya kazi za kielimu na kuhimiza uvumbuzi, jamuia ya kimataifa iliweka utaratibu wa kulinda haki-miliki ya kielimu zaidi ya miaka 100 iliyopita na kupiga hatua za maendeleo hadi kufikisha hatua ya kusainiwa "Mkataba wa Paris wa kulinda haki-miliki ya kazi za viwanda" mwaka 1883 mjini Paris. Ili kuimarisha hifadhi ya haki-miliki ya kielimu na ushirikiano kati ya nchi na asasi za haki-miliki ya kielimu duniani, mwaka 1967, jumuia ya kimataifa ilianzisha "Shirika la Haki-miliki ya Kielimu Duniani" huko Stocholm, mji mkuu wa Sweden, ambalo hapo baadaye lilikuwa moja la mashirika maalumu la Umoja wa Mataifa.

    Tangu China kujiunga na Shirika la Haki-miliki ya Kielimu Duniani mwaka 1980, China ilijenga utaratibu wa kulinda haki-miliki ya kielimu na kubuni sheri nyingi husika zikiwa ni pamoja na "sheria ya nembo ya biashara", "sheria ya hataza" na "sheria ya haki ya uandishi". Baada ya kujiunga na Shirika la Biashara Duniani,WTO, si kama tu China ilifanya marekebisho juu ya sheria za kulinda haki-miliki ya kielimu zilizotajwa hapo juu, bali ilitunga baadhi ya sheri mpya ambazo zinachangia kukamilika kwa mfumo wa sheria za kulinda haki-miliki ya kielimu.

    Katika kulinda haki-miliki za kielimu, China inafuata sanbanban njia mbili za kuwafungulia mashitaka watu wenye makosa na kutekeleza sheria za usimamizi. Mtu, mwakilishi wa kisheria wa kampuni au asasi yoyote yenye haki-miliki za kielimu, wanaweza kutoa mashitaka mahakamani wakati haki zao zinaposhambuliwa. Katika miaka ya karibuni, idadi ya kesi kuhusu haki-miliki ya kielimu zilizoshughulikiwa na mahakama ya uuma inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Habari zinasema kuwa katika mwaka 2003, mahakama ya China ilishughulikia kesi karibu 6,000 za haki-miliki za kielimu. Hivi sasa watu wengi wameanza kujua kuliinda haki-miliki zao za kielimu kwa kufuata njia ya sheria.

    Licha ya kuufuata njia ya mahakama, idara husika za serikali ya China zinalinda haki-miliki za kielimu kwa njia ya kutekeleza sheria. Katika China, kila mtu, au asasi zinaweza kutoa mashitaka kwa mahakama wakati haki-miliki zao zinapohujumiwa. Katika miaka ya karibuni, idadi ya watu waliotoa mashitaka kwa mahakama ya uuma kuhusu haki-miliki ya kielimu imeongezeka kwa kiwango kikubwa. Habari zinasema kuwa katika mwaka 2003, mahakama ya China zilishughulikia kesi karibu 6,000 kuhusu haki-miliki za kielimu, hali ambayo inaonesha kuwa watu wengi wamafahamu kulinda haki-miliki zao za kielimu kwa sheria.

    Licha ya kufuata njia ya kutoa mashitaka mahakamani, idara husika za serikali ya China pia zinalinda haki-miliki za watu kwa usimamizi wa utekelezaji wa sheria.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-09