Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-10 21:07:41    
Jamii ya China Yafuatilia Watoto

cri
    Kutokana na kuenea kwa haraka kwa matumizi ya mtandao wa internet nchini China, mtandao wa internet umekuwa njia muhimu kwa watoto nchini China kujifunza, kubadilishana mawazo na kujiburudisha. Lakini wakati mtandao wa internet unapowasaidia kupanua upeo na kujipatia ujuzi, baadhi ya habari pia zimeleta athari mbaya kwa watoto, kiasi kwamba hata baadhi ya watoto wanashindwa kujizuia na kujikuta wakizama katika hali iliyobuniwa kwenye mtandao.

    Idara mbalimbali za jamii ya China siku zote zinafuatilia sana athari za mtandao wa internet kwa watoto , na kufanya utafiti kuhusu namna ya kutumia vizuri mtandao wa internet katika kuwahudumia na kuwaelimisha watoto . Kamati kuu ya chama cha vijana cha kikomunisti cha China inashiriki katika kujenga mtandao wa internet unaowahudumia hasa watoto na vijana. Mkuu wa kamati hiyo Bwana Yang Yue alieleza kuwa, kutokana na hali ya watoto na vijana kutoweza kujidhibiti, na baadhi ya vituo vya internet vilitoa huduma za kibiashara, vikiaribu kuwashawishi watoto kucheza michezo au kutazama picha za ngono kwenye internet ili wapate fedha nyingi, hivyo idara inayohusika ya China imetunga sheria kali za kusimamia vituo hivyo vya kibiashara, kupiga marufuku vijana watoto wasiozidi umri wa miaka 18 wasitembelee vituo hivyo. Ukiingia katika kituo kiitwacho "qingxinzhai" katika mtaa wa Xichen, Beijing, huwezi kumuona mtoto hata mmoja. Msimamizi wa kituo hicho Bwana Wu Chuanxin alisema :

    "Kutokana na kanuni zetu, kila mtu akitaka kuingia katika kituo chetu lazima aoneshe kitambulisho chake, wale wasiozidi umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kuingia. Mimi pia niliwahi kuwa mwanafunzi, niliwahi kujitumbukiza katika michezo kwenye mtandao, ambayo imeathiri masomo yangu, na nilijuta sana. Sasa nafanya kazi hiyo, najua athari zake, hivyo lazima nitilie maanani kuhusu jambo hilo."

    Jamii ya China inawafuatilia sana vijana na watoto katika sekta mbalimbali. Katika sehemu nyingi za umma, huandikwa maneno ya kuwapa kipaumbele vijana na watoto, maduka mengi hata yameweka kaunta maalum kwa watoto. Zaidi ya hayo, nchini China kuna hospitali maalum ya watoto, watoto chini ya urefu fulani wanaweza kupanda basi na kuingia bustanini bila kiingilio. Katika bustani, zana za aina mbalimbali za michezo ya watoto zinaonekana hapa na pale. Ili kuhakikisha usalama wao, idara zinazohusika za taifa la China zinachunguza kwa makini ubora wa zana hizo na kufanya ukaguzi kila baada ya muda fulani.

    Naibu mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa usalama wa zana maalum ya idara kuu ya usimamizi wa ubora wa taifa ya China Bwana Wu Junsheng alisema:

    "Baraza la serikali la China limetunga utaratibu wa usalama wa zana maalum ambao unasema kuwa, zana za aina mbalimbali zikiwemo zana za michezo bustanini lazima zikaguliwe kila baada ya muda fulani, ili kuhakikisha usalama wa zana zenyewe na watoto. Na endapo dosari zitagunduliwa, ni lazima zirekebishwe mara moja, na kama kuna matatizo makubwa, basi lazima zisiruhusiwe kutumika tena. "

    Ili kuwapatia watoto na vijana huduma bora ya kiakili baada ya masomo, China imeanzisha mashirika mengi maalum ya utamaduni yanayowahudumia watoto na vijana, kama vile shirika la uchapishaji vitabu vya fasihi kwa watoto, kiwanda cha kutengeneza filamu za watoto na kadhalika. Kituo kikuu cha televisheni cha China CCTV mwishoni mwa mwaka jana kilianzisha idhaa maalum ya watoto, vipindi vinavyooneshwa katika idhaa hiyo vinahusu mambo ya elimu, ujuzi na burudani, watoto na vijana wanaipenda sana idhaa hiyo.

    Zhai Yinan ni mwanafunzi wa daraja la 5 katika shule ya Beijing. Yeye si kama tu ni mtazamaji wa idhaa hiyo ya watoto, bali pia anashiriki katika baadhi ya vipindi vya idhaa hiyo. Alisema kuwa, "Naona idhaa hii ya watoto inaendeshwa vizuri sana, napenda sana kutazama vipindi vya watoto wavumbuzi, nimejifunza mambo mengi kutokana na vipindi hivyo. Zaidi ya hayo, hata mimi nimewahi kuwa mwandishi habari wa kipindi kiitwacho "Dafengche". Maarifa hayo yatanisaidia sana katika maisha yangu.

    Ili kuwasaidia vijana na watoto wakue vizuri, idara mbalimbali nchini China zimewafungulia mlango bure. Kama vile kasri ya wafalme ya kale ya Beijing (Forbidden City) ni nyumba maarufu sana ya maonyesho duniani, japokuwa gharama za kulitunza kasri hilo ni kubwa sana, lakini kuanzia tarehe mosi March mwaka huu, kasri hilo lilianza kutoa huduma bure kwa vijana na watoto katika wakati uliowekwa, ili kuwasaidia wafahamishwe ujuzi wa kihistoria kwa kuona majengo na vyombo vya kale.

    Maktaba ya taifa la China imeanza kuweka siku ya kuwapokea watoto na chumba cha kusomea kwa watoto ili kuwafundisha jinsi ya kutumia maktaba. Nyumba za maonyesho, makumbusho na za michoro katika sehemu mbalimbali nchini China pia zinafanya maonesho ya aina mbalimbali kufuatana na tabia maalum zinazo wapendeza watoto .

    Hivi sasa, japokuwa mazingira kwa watoto waishio katika sehemu maskini na za mipaka nchini China bado hayawezi kufurahisha , lakini jamii ya China haiwezi kuwasahau. Katika miradi inayoleta maslahi kwa umati wa watu nchini China, kuna miradi mingi inawahudumia watoto hao. Kama vile, mradi wa matumaini ulioanzishwa miaka 15 iliyopita na mfuko wa maendeleo ya watoto wa China, inakusudia kuwasaidia watoto maskini kupata elimu, hadi leo imepokea msaada wenye yuan za renminbi bilioni 2.2 kutoka kwa watu binafsi nchini China na nchi za nje, na kusaidia ujenzi wa shule zaidi ya elfu kumi za matumaini na kuwasaidia watoto vijana maskini laki 26 kuendelea na masomo yao.

    Kwa watoto vijana waliofanya makosa kutokana na sababu mbalimbali, jamii ya China imeanzisha mahakama maalum na kuwaokoa kwa njia za kutoa adhabu na elimu sambamba. Tangu mahakama ya kwanza ya watoto vijana kuanzishwa miaka 18 iliyopita, sasa zimekuwepo mahakama zaidi ya 2500 nchini China. Naibu mkuu wa mahakama ya watoto ya Haidian hakimu Shang Xiuyun alisema kuwa, "Watoto wanahitaji kutambuliwa, kusifiwa na kuhamasishwa, hivyo licha ya kuchunguza sababu za watoto kufanya uhalifu, tunazingatia sana kujua uhodari wao . Wakati wa kuchunguza kesi za watoto, huwa tunazungumza na wazazi wao na walimu wao ili kufahamishwa watoto hao waliwahi kusifiwa nini, wana tabia gani nzuri, na mienendo yao mizuri shuleni."

    Katika miaka 18 iliyopita, hakimu Shang Xiuyun amepata uaminifu na upendo kutoka kwa watoto walioshitakiwa kwa moyo wake mkunjufu, na kupata mafanikio mazuri. Kati ya watoto vijana 650 waliohukumiwa naye, wengi wamerekebisha tabia zao, wengine wamefaulu kuingia katika vyuo vikuu kwa masomo, wengine wanajifunza kazi kama upishi, ushonaji, udereva, na wengi wamekuwa raia wanaofuata sheria.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-10