Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-11 18:49:45    
Idara ya misitu za sehemu ya kaskazini mashariki ya China zinazohifadhi rasilimali ya misitu na kukuza uchumi wa misituni

cri

    Ili kuhifadhi rasilimali ya misitu, katika miaka ya karibuni serikali ya China imeanzisha miradi ya uhifadhi wa misitu ya asili ikitaka kupiga marufuku au kudhibiti ukataji miti. Licha ya hayo inajitahidi kukuza uchumi kwa namna mbalimbali kwa kutegemea rasilimali ya misitu. Sasa wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi ya ukataji miti zamani wamebadilika kuwa wapandaji miti na walinzi wa misitu. Hivi sasa misitu inastawi na pato la wafanyakazi limeongezeka kwa kiwango kikubwa.

    Sehemu ya kaskazini mashariki ni sehemu muhimu yenye misitu na utoaji mbao nchini China. Misitun ya sehemu hiyo hasa iko katika mlima wa Changbai mkoani Jilin na milima ya Daxing'anling na Xiaoxing'anling mkoani Helongjiang kaskazini mashariki ya China ikichukua 60% ya eneo la ardhi ya mikoa hiyo miwili.

    Mzee Chen Bao-sheng amefanya kazi kwa miaka zaidi ya 30 katika idara ya misitu ya Wangqing ya mlima wa Changbai. Akiwa mhandisi wa ukataji misitu, anazingatia sana uhifadhi wa rasilimali ya misitu ya mlima wa Changbai. Ili kuhifadhi rasilimali ya misitu, kuanzia miaka ya 60 ya karne ya 20, alifanya uchunguzi kabla ya kukata miti na kukata miti huku wakipandikiza miche ya miti. Alisema, "Hapo awali, idara yetu ilikuwa inakata miti karibu hekta 1000 kwa mwaka, kwa kuona miti yote ikikatwa nilipatwa na masikitiko makubwa sana. Lakini sisi hatuwezi kuleta hasara kwa vizazi vyetu. Njia tunayofuata hivi sasa ni kukata miti ile inayokaribia kufa au miti ambayo haiwezi kukua vizuri tena, na kubakiza miti yenye thamani kubwa; pili, tunakata miti kwenye sehemu ambayo miti imeota kwa kukaribiana sana."

    Hivi sasa, njia hiyo ya kukata miti kwa uchaguzi ya mzee Chen Bao-sheng inafuatwa katika sehemu nyingine za misitu.

     Baada ya kutekelezwa mradi wa uhifadhi wa misitu, wafanyakazi wengi waliokuwa wakifanya kazi ya ukataji miti waliopunguzwa na kufanya kazi katika sekta nyingine. Katika sehemu ya misitu ya Jiujiang mkoani Helongjiang peke yake idadi ya wafanyakazi waliopunguzwa ilifikia laki 2 na elfu 20, kiasi hichi ni zaidi ya nusu ya idadi ya wafanyakazi wa misitu wa sehemu ile.

     Kutokana na hali hiyo, viongozi wa idara ya misitu ya sehemu mbalimbali nchini walitafuta njia mbalimbali za kuongeza ajira kwa kutegemea rasilimali ya misitu.

    Idara ya misitu ya Qinghe ya mlima wa Xiaoxing'anling mkoani Helongjiang ni idara moja yenye ufanisi ikijihusisha na shughuli za aina nyingi. Kiongozi wa idara hiyo Bw. Tian Xijun alisema kuwa sekta ya misitu ya China sasa imebadilisha mawazo yake ya zamani chini ya utaratibu wa uchumi wa kimpango, alisema kuwa sekta ya misitu ni sekta moja inayoweza kukuza uchumi kwa namna mbalimbali na kuleta ajira nyingi kwa wafanyakazi wa misitu.

    "Viongozi wa idara ya misitu ya Qinghe waembadilisha mawazo yao kutokana na uchumi wa soko huria, sasa hivi wanajihusisha na shughuli za aina mbalimbali za kiuchumi, njia ambayo licha ya kuweza kuleta ajira nyingi kwa wafanyakazi waliopunguzwa, pia imeweza kutuongezea pato kubwa zaidi."

    Kwa kuelekezwa na mawazo hayo, idara ya misitu ya Qinghe kwa kuambatana na hali yao halisi ilitoa kipaumbele katika ukuzaji wa uchumi wa kifamilia. Aidha, wanapanda miti inayotoa madawa ya mitishamba, mboga mwitu, uyoga, mizabibu, pamoja na kufuga kuku, nguruwe na vyura wa msituni ambao nyamba zao zinajenga sana mwili wa binadamu.

    Kengele inapolia nguruwe wengi wanaokua vizuri wanakimbia haraka zizini mwao kutoka msituni. Nguruwe hao wanaofugwa msituni wanaonekana siyo wakubwa sana, lakini wanapendwa sana na wateja.

    Shughuli hizo licha ya kuweza kuleta ajira nyingi kwa wafanyakazi waliopunguzwa kazini, pia zimeweza kuongeza pato la wafanyakazi. Habari zinasema kuwa hivi sasa wafanyakazi wote waliopunguzwa, wamepata kazi mpya. Hivi sasa wastani wa mshahara wa mfanyakazi umekaribia dola za kimarekani 2440 kwa mwaka.

    Bw. Liu Wenhe ni mfanyakazi wa miaka mingi wa misituni ya Hualin ya idara ya misitu ya Qinghe, baada ya kutekeleza mradi wa uhifadhi wa misitu, alitia saini kandarasi ya kutunza msitu ambapo akiwa na wenzake alianzisha shughuli za ufugaji msituni.

    "Nimechukua kandarasi ya kutunza msitu na kuanzisha shamba la ufugaji kwa kushirikiana na wenzangu wanne. Tumefuga mabata zaidi ya 1500 na mbuzi zaidi ya 200. Baada ya kujishughulisha na shughuli hizo, maisha yetu yameboreshwa na pato letu pia limeongezeka.

    Pamoja na kukuza uchumi wa misituni, katika miaka ya karibuni utalii wa misituni pia umeendelezwa na idara za misitu.

    Idara ya misitu ya Baihe iliyoko katika sehemu yenye mandhari nzuri ya "Ziwa la mbinguni" inajitahidi kukuza mambo ya utalii. Wamejenga bustani ya misonobali, msitu wenye zizi la tiger wa sehemu ya kaskazini mashariki ambao wamekuwa katika hatari ya kutoweka kabisa ulimwenguni, hatua ambayo licha ya kuweza kuongeza vitu vinavyoburudisha watalii, pia wanaweza kuhifadhi rasilimali ya wanyama adimu. Hivi sasa wamebadilisha jengo la ofisi kuwa hoteli ya wageni ili kukuza uwezo wa kupokea watalii na "Ziwa la mbinguni" lililoko katika mlima wa Changbai limekuwa sehemu yenye mandhari nzuri inayovutia wageni wengi kila mwaka. Mwaka jana, pato kutokana na utalii lilifikia Yuan za Renminbi milioni 2 na laki 5, na utalii umekuwa nguzo ya idara ya misitu ya Baihe.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-11