Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-15 18:53:34    
Malimbikizo makubwa ya mafuta barani Afrika yafuatiliwa na wafanyabiashara ulimwenguni

cri
    Afrika ina maliasili nyingi ya mafuta,ambapo malimbikizo yake ya mafuta yanachukua nafasi ya tatu duniani kufuata sehemu ya mashariki ya kati na Latin Amerika. Kutokana na hali ya wasiwasi ya sehemu ya mashariki ya kati, bei ya mafuta imekuwa kubwa, wafanyabiashara wa mafuta wanafuatilia zaidi siku hadi siku mafuta barani Afrika yenye mustakabala mzuri.

    Kutokana na takwimu za OPEC, mwaka 2002, malimbikizo ya mafuta barani Afrika yalifikia mapipa bilioni 93.5, ambayo inachukua asilimia 8.8 ya malimbikizo ya mafuta ulimwenguni. Maliasili nyingi mafuta barani Afrika inatoa fursa nyingi za biashara na kuvutia kampuni nyingi za nchi za magharibi kwenda Afrika kuanzisha shughuli za uchimbaji mafuta. Sehemu iliyo karibu na Ghuba ya Guinea barani Afrika ni mojawapo kati ya sehemu zilizopata maendeleo makubwa katika utafutaji na uendelezaji wa mafuta ulimwenguni katika miaka 10 iliyopita. Inakadiriwa kuwa, uwekezaji wa vitega uchumi wa kampuni za mafuta za nchi za nje katika mafuta na gesi kwenye eneo la Afrika magharibi utazidi dola za kimarekani bilioni 10 kwa mwaka katika miaka 5 ijayo.

    Barani Afrika, licha ya nchi wanachama wa OPEC Nigeria, Libya na Algeria, nchi nyingine kama vile Angola, Misri, Gabon na Congo Brazzaville vilevile zina uwezo mkubwa wa kuendeleza mafuta. Libya ina maliasili nyingi ya mafuta, lakini hivi sasa, uzalishaji wake kwa siku bado ni nusu tu ya uwezo wake wa juu kabisa. Kufuatana na kupunguzwa hali wa wasiwasi ya uhusiano kati ya Libya na nchi za magharibi, kampuni za mafuta za nchi za magharibi zinafuatilia nchi hiyo yenye maliasili nyingi ya mafuta. Waziri wa nishati wa Libya Bw. Fathi Omar Bin Shatwan mwezi Aprili alisema kuwa, Libya inakaribisha kampuni za nchi za nje kuwekeza katika miradi ya mafuta ya nchi hiyo. Alisema, Libya inapanga kuinua uzalishaji wa mafuta hadi mapipa milioni 3 kwa siku katika miaka 7 hadi 10 ijayo. Anakadiria kuwa, wakati wa utekelezaji wa mipango hiyo, kazi ya mafuta ya nchi hiyo itahitaji uwekezaji wa dola za kimarekani bilioni 30.

    Aidha, nchi nyingine zinazoendeleza kazi ya mafuta katika miaka ya hivi karibuni pia zinavutia sana wawekezaji wa nchi za magharibi. Mafuta mengi yaliyogunduliwa hivi karibuni katika sehemu ya pwani ya kusini nchini Cote d'Ivoire, yanafuatiliwa sana na kampuni za Marekani, Canada, Ufaransa na Ireland. Cote d'Ivoire imetia saini mkataba wa uendelezaji wa mafuta na kampuni za mafuta za Marekani na Ireland. Chad imekuwa nchi mpya ya mafuta baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoendelea kwa miaka 30. Kundi la fedha la kimataifa likiwemo kampuni maarufu ya Marekani ExxonMobil limewekeza vitega uchumi vyenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.7, na kuanzisha njia ya mabomba yenye urefu wa kilomia 1000 chini ya ardhi, na kusafirisha mafuta ya nchi hiyo hadi kwenye vituo vya mafuta baharini. Mbali na hayo, Guinea Ikweta pia ni sehemu muhimu kwa kampuni za nchi za magharibi kuwekezavitega uchumi. Hivi sasa, uzalishaji wa mafuta wa kila mtu wa nchi hiyo umezidi ule wa Saudi Arabia. Wakati huo huo, mradi wa mafuta baharini pia unavutia sana wawekezaji vitega uchumi wa nchi za magharibi. Hivi sasa, kazi ya zabuni kuhusu mradi huo inafanyika.

    Licha ya malimbikizo makubwa, sifa ya mafuta barani Afrika ni nzuri. Mafuta hayo yana kiasi kidogo cha Salfa, ambayo yanafaa kutengenezwa kuwa mafuta ya magari.

    Hivi sasa, uzalishaji wa mafuta ya nchi za Afrika kwa siku umefikia mapipa milioni 7.814, na kuchukua asilimia 10.3 ya uzalishaji wa jumla wa mafuta duniani kwa siku. Ili kuziwezesha maliasili ya mafuta kutoa huduma kwa uendelezaji uchumi, nchi mbalimbali zinazozalisha mafuta barani Afrika zimerekebisha sera za mafuta, na kuingiza utaratibu wa ushindani, na kampuni za taifa za mafuta hazitaweza kuhodhi soko la mafuta tena. Wataalamu wanakadiria kuwa, uzalishaji wa mafuta wa nchi za Afrika utachukua asilimia 20 ya uzalishaji wa jumla wa mafuta duniani ifikapo mwaka 2010.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-15