Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-16 21:22:56    
Mradi wa "kutozaa watoto wengi ili kupunguza umasikini na kutajirika haraka" waanzishwa Magharibi ya mkoa wa Ningxia.

cri
    Mwandishi wetu wa habari hivi karibuni alifahamishwa kwenye Mkutano wa kazi ya kwamba, Kamati ya idadi ya watu na uzazi wa mpango ya China na idara nyingine husika zinapanga kueneza uzoelfu wa kazi ya majaribio ya Mradi wa "kutozaa watoto wengi ili kupunguza umaskini na kutajirika haraka", na sasa Mkoa wa Yunnan na Mkoa wa Qinghai umeingizwa kwenye majaribio ya utekelezaji wa mradi huo.

    Mradi huo ni mageuzi yanayofanyika katika kazi ya uzazi wa mpango vijijini nchini China, ambao pia ni kazi mpya ya kusaidia kupunguza umasikini vijijini. katika hali ya kuendelea kutekeleza sera ya uzazi wa mpango wa hivi sasa, watu wanaofuata sera ya uzazi wa mpango wanapewa tuzo na serikali, na kwa wazazi wenye mtoto mmoja ambao pia wamekuchukua hatua ya kuwepa mimba wanapewa tuzo kubwa mara moja, Mbali na hayo idara husika zinazisaidia familia hizo kutumia fedha za tuzo katika kazi za kuendeleza kilimo ili kuwasaidia waweze kutarajika haraka iwezekanavyo.

    Lakini hali ya kijioglafia ya vijiji vilivyoko Magharibi ya China ni mbaya, na maliasili za sehemu hiyo haziwezi kuwatosheleza watu wanaoishi katika vijiji vingi vya sehemu hiyo. Lakini wakati huo huo, kutokana na kiwango cha chini cha uzalishaji mali na uwezo mdogo wa huduma za jamii katika sehemu hiyo, watu wa sehemu hiyo bado wantegemea kuzaa watoto wengi ili kupata nguvu ya kubadilisha hali ilivyo, hivyo watu wengi walizaa watoto wengi lakini wanakumbwa na shida kubwa zaidi maishani.

    Ili kubadilisha hali ya umaskini, mwaka 2000, mkoa wa Ningxia ulianza kuufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mradi wa "kutozaa watoto wengi ili kutajirika haraka" katika wilaya 6 na vijiji 6 mkoani humo. Mpaka sasa, kazi hiyo imeeneza katika vijiji 521 na wilaya 77, Zaidi ya wanandoa 7000 walichukua hatua ya kukwepa mimba, na walipewa tuzo ya Yuan kati ya elfu 3-5. Miongoni mwao zaidi ya 80% walitumia fedha za tuzo kama mtaji wa shughuli za ufugaji, kilimo, usafirishaji, na huduma n.k. kila mwaka mapato ya familia moja ilifikia Yuan elfu 4. Katika mwaka 2002-2003 kiasi cha watu waliofuata uzazi wa mpango katika wilaya 8 za Kusini ya mkoa wa Ningxia kilifikia 71.23% kutoka 66.78%.

    Katika miaka 4 iliyopita, mafanikio makubwa yalipatikana katika Mradi wa "kutozaa watoto wengi ili kupunguza umasikini na kutajirika haraka" mkoani Ningxia, Mradi hu ulihimiza maendeleo ya uchumi, jamii, maliasiri na mazingira ya sehemu hizo. Mwaka huu, shirika la idadi ya watu na uzazi wa mpango ya China, Wizara ya fedha ya China, Ofisi ya baraza la serikali ya kusaidia watu masikini wa China kujiendeleza na idara husika nyingine ziliamua kueneza uzoefu wa mkoa wa Ningxia nchini kote China na kuongeza sehemu za kufanya majaribio ya Mradi wa "kutozaa watoto wengi ili kutajirika haraka" katika eneo la magharibi ya China, ili kupunguza umasikini katika eneo hilo.

Idhaa ya kiswahili 2004-06-16