Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-17 21:04:28    
Wakulima wa Mkoa wa Mongolia ya Ndani wafaidika kutokana na mifugo ya ng'ombe

cri
    Hivi karibuni, mwandishi wetu wa habari alitembelea mkoa wa Mongolia ya ndani uliopo kaskazini mwa China, ambapo alipata kuona kuwa, wakulima mkoani humo wanafurahia kujishughulikia mifugo ya ng'ombe, na wengi wao wamepata fedha kutokana nayo.

    Mkoa wa mongolia ya ndani una eneo kubwa la ukanda wa mbuga, ambao ni eneo la mifugo nchini China. Katika miaka ya karibuni, katika sehemu karibu na mji wa Huhehaote, ambao ni mji mkuu wa mkoa huo, serikali imetilia maanani sekta ya maziwa, na yameanzishwa na kuendelezwa makampuni makubwa ya mazao ya maziwa, yakiwemo makampuni ya Yili na Mengniu ambayo hujulikana sana hapa nchini. Makampuni hayo yametoa ushuru mwingi kwa serikali, pia yameleta faida kwa wakulima wa mkoani humo.

    Wilaya ya Chaosuqi iliyopo kitongoji cha mji wa Huhehaote ni sehemu ya ufugaji wa ng'ombe, ambayo yanatoa maziwa kwa kampuni ya Yili. Katika wilaya hiyo, mwandishi wetu alishuhudia kwamba, nyumba nyekundu za matofali zinapagwa barabara, kila nyumba ina eneo la mita 200 za mraba ikiwa pamoja na mazizi. Mbali na hayo, kila familia ina mashamba ya hekta 0.13 ya kuotesha chakula cha kuwalisha ng'ombe wakati wa siku baridi. Mkulima mmoja alimwambia mwandishi wetu kuwa, miaka mitatu iliyopita, serikali na kampuni ya Yili zilichangia fedha kujenga nyumba hizo zaidi ya 100 kwa ajili ya mifugo ya ng'ombe. Wakulima wakikosa fedha za kununua nyumba, waliweza kuomba mitaji ya miaka mitatu bila riba kutoka benkini, na kampuni ya Yili pia ilisaidia mitaji ya dola za kimarekani 550 kwa kila ng'ombe.

    Bw. Ren Peiping mwenye umri wa miaka 40 mwaka huu ni mkulima mmoja anayeshughulikia mifugo ya ng'ombe kwenye wilaya hiyo. Miaka mitatu iliyopita, akitegemea mitaji ya dola za kimarekani 11,000 kutoka serikali na kampuni pamoja na akiba yake mwenyewe, alinunua nyumba mbili na ng'ombe 28, akajishughulikia mifugo. Hivi sasa, amekuwa na ng'ombe zaidi ya 40. Alisema, "Inaendelea vizuri katika miaka hiyo. Sasa ng'ombe wapatao 15, 16 wanazaa maziwa jumla ya zaidi ya tani 300 kila siku, hivyo napata faida ya dola za kimarekani 1220 kwa mwezi."

    Bw. Ren aliongeza kusema kuwa, tokea baba yake, familia yake ilikuwa imejishughulikia mifugo. Hapo mwanzoni, kutokana na ukosefu wa mitaji, ilikuwa utajiri mkubwa kwa familia yenye ng'ombe kadhaa. Lakini hivi sasa, Bw. Ren anafuga ng'ombe zaidi ya 40, mbali na hayo, hana wasiwasi juu ya kuuza maziwa. Kwa vile, kuna kituo cha kutoza maziwa kwenye eneo hilo la mifugo ya ng'ombe, ambacho kinashughulikia kununua maziwa kutoka wakulima.

    Bw. Zhan Yongkuan wa kampuni ya Yili alieleza kuwa, ili kulinda maslahi ya wakulima wanaofuga ng'ombe, kampuni hiyo imesaini mikataba na wakulima.

    "Sisi na wakulima tumetilia sahihi mikataba, na tunanunua maziwa yote ya ng'ombe kutoka kwa wakulima hao. Ili kuhakikisha mapato ya haki ya wakulima, katika miaka hiyo tunadumisha bei ya maziwa katika kiwango fulani, na kila mwezi tunaweka fedha kwenye akounti za wakulima benkini kwa wakati. Aidha, tunawasaidia wakulima katika shughuli nyingine za ufugaji bora na karantini."

    Kutokana na ulinzi wa mikataba na huduma bora, wakulima wanafurahia sana kujishughulikia mifugo ya ng'ombe. Takwimu zinaonesha kuwa, katika eneo karibu na mji wa Huhehaote, mwaka 1992, kulikuwepo ng'ombe wasiozidi elfu 18, idadi ambayo imefikia laki 3 na elfu 50 kwa hivi sasa, ambapo wakulima karibu laki moja wameondokana na umaskini na kupata pesa. Mwaka jana, nusu ya mapato ya wakulima katika eneo hilo yalitokana na mifugo ya ng'ombe.

    Maisha ya wakulima yamebadilika sana kutokana na mifugo ya ng'ombe. Tukichukua mfano wa Bw. Ren Peiping, pamoja na kufuga ng'ombe, familia yake pia inaotesha mahidi ya hekta 4 kama chakula cha ng'ombe. Kwa ajili ya kusafirisha chakula cha ng'ombe, alinunua gari dogo la uchukuzi kwa dola za kimarekani 1,200. Bw. Ren alisema kuwa, kutokana na mifugo ya ng'ombe, maisha ya familia yake yameinuka kwa kiasi kikubwa. "Hapo mwanzoni viazi vilikuwa chakula muhimu kwenye familia yangu, ambapo mboga zilikuwa nadra kuonekana. Sasa tunakula mara kwa mara mboga za aina mbalimbali, nyama na samaki. Mwanzoni ilikuwa hakuwepo vitu vyovyote vya umeme nyumbani kwangu, lakini sasa nina vitu vyote vya umeme, motokaa, na nilinunua komputa mwaka huu, sasa napenda kutafuta habari za mifugo ya ng'ombe kwenye mtandao wa Internet."

    Ng'ombe wa Bw. Ren wanazaa ndama zaidi ya 10 kila mwaka. Mwandishi wetu alipotembelea zizi lake la ng'ombe, aliona ng'ombe mmoja mwenye mimba. Bw. Ren alisema na furaha kuwa, ndama mmoja anauzwa kwa dola za kimarekani 600. Hata hivyo, hana mpango wa kuuza ndama wote, bali anataka kupanua shughuli zake za mifugo ya ng'ombe.

    Aliongeza kusema kuwa, kampuni ya Yili inajenga eneo la kisasa la mifugo ili kuinua ukubwa na ubora wa shughuli za mifugo ya ng'ombe. Mkulima mwenye ng'ombe 50 na mitaji fulani angeweza kuhamia kwenye eneo hilo la kisasa. Bw. Ren akiwa na imani kubwa alimwambia mwandishi wetu kwamba, katika miaka miwili au mitatu, hakika ataweza kutimiza lengo la kuingia kwenye eneo la kisasa la mifugo, ambapo atapata maendeleo makubwa zaidi.

Idhaa ya Kiswhaili 2004-06-17