Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-18 18:23:30    
Maonyesho ya saba ya biashara na uwekezaji ya China

cri
    Maonyesho ya saba ya biashara na uwekezaji ya China yalifungwa hivi karibuni huko Xiamen, mji mkuu wa pwani ya kusini mashariki ya China. Maonesho hayo yaliwavutia wafanya biashara zaidi ya elfu 11 wa nchi na sehemu 102. Wataalamu husika wamesema kuwa mafanikio ya maonesho ya 7 ya biashara yamebainisha kuwa hatakati za uwekezaji zimeanzishwa upya baada ya ugonjwa wa SARS kuthibitiwa ipasavyo.

    Maonesho ya biashara na uwekezaji ya China ambayo huandaliwa na wizara ya biashara ni shughuli pekee za China katika kuhimiza uwekezaji wa vitega uchumi ikiwa ni pamoja na uwekezaji biashara ujulishaji wa sera za China na utafiti wa biashara. Maonesho hayo hutoa mialiko kwa mashirika ya umma na serikali pamoja na makampuni na viwanda vya aina mbalimbali vinavyotafuta ushirikiano wa uwekezaji.

    Kuanzia mwaka 1997 maonesho ya biashara na uwekezaji ya China hufanyika mwezi september kila mwaka mjini Xiamen. Katika maonesho 6 yaliyopita thamani ya mikataba ya biashara iliyosainiwa kati ya China na nchi za nje ilifikia karibu dola za kimarekani bilion 70. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya wizara ya biashara Bw. Wen Zai-xing alisema

    Ikiwa ni hatua muhimu ya mkakati wa China katika ufunguaji mlango kwa nje maonesho ya biashara na uwekezaji ya China yamekuwa kama daraja la kuingiza mitaji ya nje na pia ni daraja kwa viwanda na makampuni ya China kuwekeza katika nchi za nje .

    Kampuni ya kompyuta ya Dell ya Marekani ambayo ni maarufu sana ulimwenguni, ilikuwa na mazungumzo na serikali ya China tangu maonyesho ya kwanza ya biashara na uwekezaji, hatimaye iliamua kujenga kituo cha kudumu kwa wateja wa China mjini Xiamen ambacho kilianza kutoa huduma mwaka 1998. Katika miaka mitano iliyopita kampuni ya Dell ilikuwa na maendeleo makubwa na kuwa na ongezeko la wastani wa 70% kwa mwaka. Hivi sasa kampuni ya Dell sio kama tu imejiimarisha katika nafasi ya soko la kompyuta nchini China, bali imechukuwa nafasi ya 6 ya soko la kompyuta la China na kuwa kampuni ya tatu ya kompyuta kwa ukubwa nchini China. Katika orodha ya makampuni 200 makubwa nchini China yaliyosafirisha bidhaa zake nchi za nje mwaka 2002, thamani ya bidhaa zilizosafirishwa kwa nchi za nje na kampuni ya Dell inakaribia dola za kimarekani bilioni 1. 2 ikichukuwa nafasi ya kwanza miongoni mwa makampuni ya nchi za nje ya uzalishaji wa zana za upashanaji habari yalioko nchini China. Bw. Li Yuan-jun wa kituo cha kudumu ya wateja cha kampuni ya Dell nchini China alifurahia maendeleo yake hayo akiona kwamba mafanikio yayo yametokana na soko kubwa la China na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji.

    Sababu ya sisi kuwekeza hapa Xiamen ni kutokana na rasmali nyingi ya nguvu kazi mazingira bora ya uwekezaji na uungaji mkono wa serikali ya China. Hii ndiyo sababu muhimu ya sisi kuwekeza hapa na kujenga kampuni inayotengeneza bidhaa kwa sehemu ya Asia ya kaskazini mashariki.

    Hali halisi ni kwamba maonesho ya biashara na uwekezaji ya China yamekuwa yakitoa fursa kwa wafanya biashara wa nchi za nje kufahamu mambo ya China. lakini sasa yanabadilika na kuelekea kuwa harakati kubwa ya uwekezaji ulimwenguni. Mashirika ya kilimwengu yalioshiriki katika maandalizi ya maonesho ya 7, mbali na mashirika ya kuhimiza biashara ulimwenguni, kuna baraza la biashara na maendeleo la umoja wa mataifa nchini na sehemu 58 zikiwemo Canada, Marekani, Japani, New-zealand, Ujerumani na Australia zilishiriki katika maonesho hayo, ambapo Uingereza, Canada. sehemu Caribbean na Hong Kong ziliweka siku maalum za maonesho yao zikiwafahamisha wafanya biashara sera na mazingira ya uwekezaji katika nchi zao ili kuwavutia kuwekeza huko. Aidha maonesho ya 7 pia yalikuwa na majadiliano juu ya baadhi ya maswala ya kilimwengu hatua ambayo imehimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi mbalimbali.

    Shughuli nyingine iliyopewa kipaumbele ni kuvutia wafanya biashara wa nchi za nje kuwekeza hapa china na kuhumiza viwanda na makampuni ya China kwenda kuwekeza katika nchi za nje. Hapo zamani waandaji walizingatia kuwavutia wafanya biashara wa nchi za nje kuja kuwekeza hapa nchini, lakini katika maonesho ya 7 wafanyabiashara wa China wamekuwa na wazo la kwenda kuwekeza katika nchi za nje. Mazungumzo ya utafiti wa uwekezaji yanahusu nchi na sehemu makumi kadhaa zikiwemo nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki, sehemu ya Carribbean, Uingereza, Marekani na Hong Kong ya China. Mazungumzo hayo yamefuatiliwa na washiriki wa maonesho hayo na kutoa fursa nzuri kwa wafanya biashara wa China kufahamu hali ya mitaji, masoko, sera na mazingira ya uwekezaji nchi za nje. Benki ya watu wa China na idara za serikali zimepunguza masharti ya kuwekeza katika nchi za nje kwa viwanda na makampuni ya China, ili kuvisaidia katika mambo ya sera. Baadhi ya viwanda na makampuni ya China yamekuwa na shauku kubwa ya kwenda kuwekeza katika nchi za nje ili kukwepa vikwazo vya biashara vilivyowekwa na nchi za nje. Kiongozi wa idara ya mitaji ya kigeni ya wizara ya biashara ya China , Bw Hu Jing-yan alisema

    Sifa moja muhimu ya maonesho ya biashara na uwekezaji ya Xianmenni kuvutia uwekezaji wa nje na kuhimiza uwekezaji wa China katika nchi za nje. Licha ya kuvutia uwekezaji vitega uchumi wa nchi za nje, pia sisi tunahimiza baadhi ya makampuni na viwanda vyenye uwezo unaotakiwa kuwekeza katika nchi za nje. Hii inaambatanisha na sera za China.

    Ofisa wa wizara ya biashara ya China alisema kuwa katika siku za baadaye, China itaendelea kuhimiza viwanda na makampuni ya China kuwekeza katika nchi za nje.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-18