Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-18 18:59:45    
Wachina waishio Zanzibar

cri

    Katika karne zilizopita, wachina wengi waliondoka nyumbani, wakavuka bahari hadi kufika pwani ya sehemu nyingine ili kutafuta maisha bora. Mwandishi wetu wa habari alipotembelea Tanzania aliwatembelea wachina waishio Unguja. Katika kipindi hiki cha leo,tumewaandalia maelezo kuhusu historia ya wachina waishio Unguja, na maisha yao ya hivi sasa yalivyo.

    Bi. Chen Lijun alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alielezea historia ya wachina waliofika Zanzibar akasema kwamba, katika miaka ya 20 ya karne iliyopita, kikundi cha wachina vijana kilifika katika sehemu ya pwani ya Tanzania na Kenya wakipelekwa na kampuni moja ya Hongkong ili kutafuta majogoo ya baharini. Wengine walikwenda Pemba, Lamu, Mombasa, na Malindi, vijana 9 walifika Unguja. Hawa vijana baada ya kuishi Unguja kwa miaka kadhaa, waliipenda sana Unguja na kuamua kuishi huko. Walirudi China kutafuta wake na kwenda kuishi pamoja nao Unguja.

    Kwa mfano, baba ya Bi. Chen Lijun alikuwa mmoja kati ya watu waliotangulia kufika Unguja, baada ya miaka kadha, alirudi China kuoa na kwenda pamoja na mke wake Unguja na wakazaa watoto 7. Bi. Chen Lijun ambaye ni kitindamimba alizaliwa mwaka 1955. hali kadhalika na familia nyingine. Hivyo watoto wa kizazi cha pili cha wachina waishio Unguja wamekuwa wengi.

    Nyumbani kwa Bi. Chen Lijun kuna picha iliyopigwa mwaka 1968. Japokuwa picha hiyo ni ya zamani, lakini imeonyesha hali ya wakati ule ya wachina waliokuwa wakiishi Unguja. Kwenye picha hiyo kuna mkusanyiko wa watu wapatao 35 wa familia tisa walioishi huko Unguja.

    Lakini kwa sababu Unguja ni sehemu ndogo, hawawezi kupata elimu ipasavyo na hakuna nafasi nyingi nzuri za kazi, hivyo watoto wengi baada ya kumaliza shule ya msingi walipelekwa ng'ambo kusoma na kutafuta kazi, na kuishi kule kule. sasa wengi wamesambaa katika nchi za marekani, uingereza na nchi nyingine za ulaya, na australia. kama mimi nina ndugu saba, lakini watano wako nje, ni mimi na ndugu mwingine tu tuliobaki hapa. watatu wako marekani, mmoja yuko australia, na mwingine yuko Dar.

    Bibi Chen lijun alisema, sasa hivi familia yake imekuwa ya kizazi cha nne, mama yake amerudi china, na yeye mwenyewe ana watoto watatu, na hata amepata mjukuu, yaani kizazi cha nne.

    Japokuwa wameishi ng'ambo kwa miaka mingi, hawajui kuandika na kusoma kichina, lakini wanatilia maanani sana uhusiano na china. Bi chen alisema kwamba, karibu kila mwaka yeye na mume wake huwa wanarudi China kuwatembelea jamaa zake, na kutembelea hapa na pale huku china. Anasema walipoona maendeleo na mabadiliko makubwa yametokea nchini China katika miaka ya hivi karibuni, wanalifurahi sana.

    Ili kuwaeleimisha watoto wao ujuzi kuhusu China, waliwapeleka watoto wote 3 kusoma huko Hongkong walipomaliza tu shule ya msingi huko Unguja. Sasa watoto wake wote wameshakua, mtoto wa kwanza amerudi Unguja kuendesha mkahawa wa chakula cha kichina uitwo Pagoda. Mtoto wa kiki amemaliza masomo huko australia na kupata kazi yake huko, mtoto wa mwisho bado anasoma ng'ambo.

    Kuhusu maisha yao ya Unguja, Bi Chen Lijun alisema kuwa, kwa ujumla, maisha ya Unguja ni mazuri. Zamani walifanya biashara ya majogoo ya baharini, tambi n.k. Sasa biashara ya majogoo imekuwa sio nzuri tena, kwa sababu, zamani wenyeji walikuwa hawajui majogoo ni kitu gani, na kina thamani gani, lakini katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na Tanzania na Zanzibar kufungua mlango kwa nje, tena bei ya majogoo imepanda sana, wafanyabiashara wengi kutoka nje wamekwenda Unguja kununua majogoo, na wenyeji wakaambiwa kuokota majogoo. Kwa kuwa wenyeji hawajui kuhifadhi wale wadogo, hivyo sasa kiasi cha majogoo kimepungua sana. Bi. Chen na bwana yake wameanza kuzeeka, hivyo wameamua kuacha biashara ya majogoo, na kuanzisha mkahabwa wa chakula cha kichina. Kwa kuwa, sasa watalii wengi wanamiminikia Zanzibar, hivyo biashara yao ya mkahawa imekuwa mzuri sana.

    Licha ya mkahawa wa chakula cha kichina, pia wanashughulika na tambi ya unga, kila asubuhi wanatengeneza tambi, halafu kuzisambaza Unguja, pemba hata Dar es Salaam na Mombasa. Mpaka sasa wanajitosheleza sana katika maisha yao. Lakini kwa sababu Zanzibar ni sehemu ndogo, isiyo na hali nzuri ya kiuchumi, hivyo siyo rahisi kwao kufanya biashara kubwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-18