Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-24 17:45:53    
Mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia ya peninsula ya Korea

cri

    Duru la tatu la Mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia ya peninsula ya Korea yanafanyika kuanzia tarehe 23 hadi 26 hapa Beijing.

    Kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2002, suala la nyuklia la peninsula la Korea lilionekana kuwa ni tatizo kubwa ambalo liliathiri vibaya amani na utulivu wa peninsula ya Korea na sehemu ya kaskazini mashariki ya Asia. Ili kusukuma mbele utatuzi wa suala hilo, kuanzia mwezi Marchi mwaka 2003, serikali ya China ilifanya usuluhishi kati ya pande mbalimbali, na mwezi Aprili mwaka huo huo China ilifanikiwa kuanzisha mazungumzo ya pande tatu za China, Korea ya kaskazini na Marekani hapa Beijing. Baada ya hapo, na baada ya kufanya mashauriano na usawazishaji kati ya China, Korea ya kaskazini, Korea ya kusini, Marekani, Japan, na Russia, Duru la kwanza la mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea yalifanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka 2003. Pande mbalimbali zilizoshiriki katika mazungumzo hayo zilipata maoni ya pamoja na kuthibitisha kanuni kuhusu kufanya mazungumzo ili kutatua kwa njia ya amani suala la nyuklia la peninsula ya Korea.

    Baada ya mashauriano na usawazishaji wa mara kwa mara kati ya China na Korea ya kaskazini, Marekani na pande nyingine mbalimbali, Duru la pili la Mazungumzo ya pande 6 lilifanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 25 hadi 28 Februari mwaka 2004. Mazungumzo hayo yalipata matokeo makubwa, kupitisha Taarifa ya mwenyekiti na kupata maoni ya pamoja kuhusu kuanzisha Kikundi cha utekelezaji wa mazungumzo hayo, ambapo pande mbalimbali zilikubaliana kufanyika kwa duru la tatu la mazungumzo hayo mwishoni mwa mwezi Juni hapa Beijing.

    Tokea kumalizika kwa duru la pili la mazungumzo hayo, China ilipitia njia mbalimbali kudumisha mawasiliano na majadiliano na pande mbalimbali, imefanya ipasavyo kazi ya usawazishaji, na pande mbalimbali pia zimeahidi kuendelea na juhudi za kuongeza maoni ya pamoja na kuaminiana zaidi. Kutokana na juhudi zilizofanywa na pande mbalimbali, mkutano wa kwanza wa Kikundi cha utekelezaji wa mazungumzo ya pande 6 ulifanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 12 hadi 22 Mei, ambapo pande mbalimbali zilibadilishana maoni kwa unyoofu na kufuata hali halisi kuhusu utatuzi wa suala la nyuklia la peninsula ya Korea, na kuthibitisha kufanyika kwa duru la tatu la mazungumzo ya pande 6 mwishoni mwa mwezi Juni kutokana na mpango uliowekwa. Baada ya kufanya mashauriano kati ya pande mbalimbali, Mkutano wa pili wa Kikundi cha kazi ya mazungumzo ya pande 6 ulifanyika tarehe 21 na 22 Juni hapa Beijing. Baada ya kumalizika kwa mkutano huo, ujumbe wa China, Korea ya kaskazini, Marekani, Korea ya kusini, Russia na Japan uliamua kufanya Duru la tatu la Mazungumzo ya pande 6 kuanzia tarehe 23 hadi 26 katika Jumba la wageni wa taifa la Diaoyutai la Beijing.

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Zhang Qiyue alipohojiwa na waandishi wa habari alisema kuwa, kadiri masuala halisi yanavyojadiliwa kwa kina zaidi, ndivyo migongano kati ya pande mbalimbali inavyoonekana kuwa wazi zaidi, na taabu zitakuwa nyingi zaidi. Huu ni ukwelil wa mambo. Lakini alisema kuwa, China itaendelea na juhudi za usuluhishi ili kusukuma mbele maendeleo ya mazungumzo hayo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-24