Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-24 19:29:09    
Wachina wafurahia kupashana habari kwa simu za mkononi

cri
    Bw. Wu Qinggang ni kijina, mwenye umri wa miaka 25, na ni mhadisi wa kampuni ya moja ya teknolojia ya hali ya juu hapa jijini Beijing. Siku moja miezi sita iliyopita majira ya saa 2 usiku alikuwa anasoma tovuti moja iliyotangaza habari za kutafuta marafiki ambapo Bw Wu alivutiwa na jina moja lililosajuliwa kama "mwezi wa kale" pamoja na nambari ya simu yake ya mkononi. Wakati huo huo kijana mmoja alikuwa na wazo moja kwamba anaweza kumsalimia kwa kumpelekea ujumbe kupitia simu ya mkononi. Muda si mrefu baadaye Bw Wu alipata majibu kutoka kwa rafiki huyo asiye mfahamu hata kidogo. Akiwa ndani ya basi kuelekea nyumbani walianza mazungumzo kupitia ujumbe wa viselula ambapo bw Wu aliona kuwa safari ya saa moja kuelekea nyumbani ilionekana imefupishwa na alihisi kuburudika kwa kiasi baada ya kazi ya siku moja. Wasikilizaji wapendwa hadithi hiyo haikuishia hapo tu bali Wu na rafiki huyo anayejiita "mwezi wa kale" wakawa mume na mke baada ya miezi sita.

    Bw Wu ananiambia kuwa, kuanzia siku hiyo walikuwa wanawasiliana mara kwa mara kupitia ujumbe wa viselula, kiazi kwamba mazungumzo hayo maalumu yaliendelea hadi usiku wa manane baadhi ya wakati. Anasema:

    Tulikuwa tunavutiana katika mazungumzo, ingawa haikupita muda mrefu, lakini tuliona kuwa tumekuwa karibu sana. Katika kipindi hiki, nilikuwa natuma ujumbe zaidi ya 100 kwa wastani wa kila siku.

    Kwa kupitia ujumbe wa viselula, Bw Wu alifahamishwa kwamba, mtu huyo anayejiita "mwezi wa kale" ni msichana na jina lake la kweli ni Qinyue. Anaishi katika mji wa Taiyuan, umbali wa kilomita 500 kutoka Beijing, anapokaa Bw Wu, wiki mbili baadaye , walikutana katika kituo cha treni cha mji wa Taiyuan, ambapo walipendana papo hapo.

    Kwa vile wanaishi katika miji tofauti, wanashindwa kukutana kila siku, gharama ya simu ya masafa marefu ni kubwa, hvyo ujumbe wa viselulaukawa njia mwafaka ya mawasilianokwa wapenzi hao, kutokana na sifa zake za kutuma na kupokea mara moja pamoja na gharama nafuu. Bw Wu anakumbusha kwamba, alikuwa anakwenda msalani akiwa na kiselula chake.

    Qinyue ni msichana mwangalifu sana, alinakili ujumbe wao mmoja baada ya mwingine kwenye daftari, na katika kipindi cha nusu mwaka, amekuwa na daftari tatu kubwa. Anaeleza kuwa katika siku zile alikwenda na kiselula, daftari na kalamu popote, anasema kuwa hizo ni alama zake za mapenzi. kiselula kina ukubwa wa kiasi wa kuhifadhi ujumbe, iwapo ukubwa huo umejaa, unapaswa kufuta baadhi kwa ajili ya kupokea mwingine. Naona kila ujumbe anaotuma ni mzuri na kuthaminika. Mapenzi yanatutia moyo ambapo baadhi ya maneno hatuwezi kuyapata kimawazo katika hali ya kawaida lakini tunaweza kuongea kupitia ujumbe wa viselula.

    Vijina hao wawili wamefunga ndoa kutokana na ujumbe wa viselula ingawa matukio ya namna hii ni machache sana, lakini katika China ya hivi leo, ujumbe wa viselula hutumika sana na watu katika kuwasiliana na kusalimiana. Mathalan, katika sikukuu ya spring, ambayo ni mwaka mpya wa kalenda ya kichina, idadi ya ujumbe iliwahi kifikia milion 100 kwa siku. Takwimu inaonesha kuwa , mwaka jana jumla ya ujumbe wa viselula ilikuwa bilion 90, na idadi hiyo itazidi bilion 150 mwaka huu. Tunaweza kusema kuwa takriban kila mteja wa kiselula wa china amepeleka au kupokea ujumbe.

    Hali hii imetokana na hali ya viselula kupatikana nchini kote. Tukitembea mijini hapa nchini tunashuhudia watu wengi wenye viselula, kiasi kwamba baadhi ya watu wanaofuatilia mitindo wamebadilisha viselula vyao mara kadhaa. Ujumbe ukiwa aina moja ya huduma za viselula sasa umegeuka kuwa njia ya mawasiliano inayopendwa na watu wengi

    Katika hali hii, makampuni ya simu ya China yametoa huduma mbalimbali za ujumbe. Hivi karibuni m-zone ndiyo inayojulikana hapa nchini, ambapo mteja hulipa Renminbi Yuan 20 tu kwa mwezi, sawa na dola 2 za kimarekani, anaweza kupeleka ujumbe 300. Hivyo kwa awali gharama yake ilikuwa centi 10 au 15.

    Bw Gao Ran ni miongoni mwa wapenzi wa huduma hiyo, anaeleza maoni yake, akisema, (sauti3) sasa natumia kadi ya " m-zone" naweza kupeleka ujumbe wakati wowote . Nikipata hadithi, vichekesho na habari mpya nawatumia marafiki na jamaa zangu kwa wakati . kwamfano wanafunzi wenzangu wanakaa katika sehemu tofauti hapa nchini. Nikiwapigia simu ni gharama kubwa. Kuwapelekea ujumbe wa viselula kunagharimu centi 7 tu, lakini naweza kuwasalimia licha ya umbali kati yetu, naweza kuwapata. Ujumbe wa viselulaunafanya kazi kubwa zaidi kuliko njia nyingine za mawasiliano.

    Ujumbe wa viselula pia umetoa nafasi ya mawasilianao kati ya watu wasiofahamiana . Bibi Wang Fan ni mwandishi wa habari alieleza mafanikio yake alipoweza kumhoji mwimbaji maarufu kwa kupiitia ujumbe wa viselula. Baada ya kupata nambari ya simu ya kiselula ya mwimbaji huyo, Bibi Wang alimpelekea ujumbekupitia viselula. (sauti4) Niliona siwezi kumpigia simu mara moja sitaki kumsumbua pia hata pokea simu yangu kwa vile hatambui nambari yangu, kwa hiyo nilimpelekea ujumbe kupitia viselula. Katika ujumbe huo, nilijitambulisha na kumweleza program yangu na maswali niliyotaka kumhoji pamoja na namna ya kunipata. Baada ya saa mbili alinipigia simu na kusema amekubali mahijiano.

    Hivi sasa ujumbe wa viselula umekuwa njia rahisi ya mawasiliano kati ya wachina, mbali na hayo umeingia katika maeneo mbalimbali ya maisha. Katika siku za baadaye labda tutaweza kuutumia katika kununua tikiti za filamu na maua kulipia ada za simu maji na umeme katika enzi hii ambapo sayansi na teknolojia huendelezwa kila wakati je kuna kitu kisichowezekana?

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-24