Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-25 18:07:31    
"Mpango wa chipukizi" wasaidia watoto elfu 110 wa kike kurudia shuleni

cri
    Kutokana na juhudi za pamoja za ngazi mbalimbali za umoja wa wanawake nchini China, "Mpango wa chipukizi" umetekelezwa vizuri katika miji 18 na wilaya 158 mkoani He nan. Mpaka sasa mpango huo umefanikiwa kukusanya fedha za misaada kiasi cha yuani milioni 25, kuanzisha madarasa zaidi ya 60 ya watoto wa kike, kujenga shule 11, na kuwasaidia watoto wa kike walioshindwa kuendelea na masomo na wanafunzi wa kike wa chuo kikuu wenye matatizo ya kiuchumi kutimiza azma yao ya kuendelea na shule.

    "Mpango wa chipukizi" ni harakati moja ya kunufaisha umma iliyoanzishwa na kutekelezwa kwa pamoja na Umoja wa Wanawake wa China na mfuko wa watoto wa China, kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike wanaoshindwa kuendelea na masomo kwenye sehemu maskini kuendelea na shule. Mpango huo ulianzishwa rasmi mkoani He nan mwaka 1994. Miaka 10 iliyopita, ili kutekeleza mpango huo, ngazi zote za Umoja wa Wanawake wa mkoa wa He nan zilifanya utafiti vijijini na kuandaa orodha ya watoto wa kike wanaotoka familia zenye matatizo ya kiuchumi. Pia zilisawazisha raslimali ya jamii, kuwawezesha watoto wa kike wenye matatizo ya kiuchumi kusaidiwa na watu maalum na kuwatafutia mama wasaidizi, na kuanzisha shughuli za kuwatunza watoto wa kike wa familia zenye matatizo ya kiuchumi. Katika miaka ya karibuni, Umoja wa Wanawake wa mkoa wa He nan umekusanya fedha zaidi ya yuan milioni 9 na kuwasaidia maelfu ya watoto wa kike. Mwaka 2003, Umoja wa Wanawake wa mkoa huo ulifanya juhudi za kuongeza na kupanua wigo wa wanaosaidiwa, harakati moja ya dharura ya utoaji misaada kwa wanafunzi wa kike wa chuo kikuu wenye matatizo ya kiuchumi iitwayo "harakati ya Da He Chun Hua" ilianzishwa kwenye jamii nzima na kuwanufaisha wanafunzi wapatao 150 wa chuo kikuu wenye matatizo makubwa ya kiuchumi.

    Katika mchakato wa kutekeleza mpango huo, Umoja wa Wanawake wa mkoa wa He nan pia unaendelea bila ya kusita kusitawisha shughuli za mpango huo na kuongeza mafunzo ya ufundi wa kivitendo kwenye masomo ya madarasa ya watoto wa kike ya mpango huo. Ngazi mbalimbali za Umoja wa Wanawake pia zinawasaidia wanawake masikini mijini na vijijini na kuhamasisha mashirika kushiriki kwenye mpango huo. Njia ya kuwasaidia watoto wa kike wa familia zenye matatizo ya kiuchumi kurudia shuleni kwa kupitia kusaidia familia zao na kuongeza uwezo wao wa kuondokana na umaskini imefanikiwa vizuri. Hata watoto wengi wa kike walikuwa wa huko walitangulia kuondokana na umaskini na kujitajirisha.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-25