Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-28 21:58:10    
Usitumie ovyo dawa za kukinga vijidudu (antibacterial )

cri
    Tokea tarehe 1 mwezi Julai mwaka huu, dawa za kukinga vijidudu haziuzwi kwa watu nchini China, hadi uwe na cheti kutoka kwa daktari. Kutolewa kwa kanuni hiyo ya kisheria ni kuzuia matumizi ya ovyo ya dawa ya kukinga vijidudu na kuhakikisha usalama wa matumizi ya dawa. Ni dawa za aina gani zinaweza kumkinga mtu na vijidudu, matumizi ya ovyo ya dawa yana madhara gani na kuna mawazo gani ya makosa katika matumizi ya dawa za kukinga vijidudu ? Mwandishi wetu wa habari aliandaa maswali hayo, na kumtembelea ofisa husika wa ofisi ya masoko ya idara ya usimamizi ya dawa ya mji wa Anshan.

    Ofisa huyu alisema kuwa dawa za kukinga vijidudu ni dawa zinazoua vijidudu au kudhoofisha nguvu zake ikiwa ni pamoja na ya sulfanilamide, imidazole, nitroimidazole na quinoketone ambazo zimetengenezwa kwa vitu vya kemikali. Licha ya dawa hizo, kuna dawa nyingine ya cephaloaporin na erythromycin ambazo tunazifahamu vema, zote ni za kukinga vijidudu. Kwa kawaida, matumizi ya ovyo ya dawa za kukinga vijidudu, yanaweza kuvifanya vijidudu vizoee na kuvumilia dawa na kuongezeka mwilini mwa binadamu, vilevile zinaweza kuongeza uwezekano wa kuathiriwa na sumu ya vitu vya kemikali na vitu vingine, na kufanya wagonjwa kutoweza kutibiwa haraka.

    Hivi sasa, familia nyingi zimejitayarishia vijisanduku vya dawa nyumbani, na watu wengine wana mawazo potofu wakidhani dawa nzuri ni ile ya bei kubwa, ukweli ni kwamba dawa siyo bidhaa za kawaida kwamba bidhaa za bei rahisi ni hafifu, kama unatumia dawa ipasavyo, hata dawa ya bei ya shilingi moja inaweza kukutiobu. Sasa watu wengi hawatumii dawa ipasavyo, wengi wanatibu mafua kwa dawa za kupambana na vijidudu, lakini mtu aliyepatwa mafua ni kuathiriwa na virusi vya mafua, akitumia dawa kiholela anaweza kuleta madhara mengine na kufanya vijidudu kuwa na uwezo wa kuvumilia nguvu ya dawa. Watu wengi baada ya kuugua ugonjwa mkali, wanaweza kutumia dawa kiasi na katika nyakati kutokana na maelezo ya daktari, lakini pindi wakipata nafuu, basi wanatumia dawa wapendavyo. Ujue kuwa nguvu ya dawa ya kukinga vijidudu inategema ujazo wa dawa ndani ya damu. Endapo utatumia dawa bila kufuata maelekezo ya daktari, ujazo wa dawa ndani ya damu utakuwa mdogo, basi si kama tu dawa itashindwa kuua kabisa vijidudu, bali itaweza kufanya vijidudu kuwa na uwezo kuvumilia dawa. Watu wengi wanadhani kuwa dawa yoyote ya kukinga vijidudu, inaweza kuondoa uvimbe, na kuna watu wanaofikiri kuwa wakitumia dawa za aina nyingi, wataweza kupona haraka zaidi. Kosa lao ni kwamba dawa tofauti zinalenga shabaha tofauti. Kwa kufanya hivyo, pamoja na kuwa hawataweza kuona matokeo yanayotarajiwa, bali pia wanaongeza madhara ya dawa na kuathiri afya zao.

    Kamwe dawa za kukinga vijidudu haziwezi kutumiwa ovyo, ujue kuwa kutumia ipasavyo dawa kunaweza kuongeza ufanisi wake. Kwa kawaida dawa za kukinga vijidudu, zinatakiwa kutumiwa saa 1 kabla ya chakula au saa 2 baada ya chakula. Ni kawaida kuwa dawa ya acheomycin na erythromycin zinaweza kutumiwa kabla ya chakula. Aidha, baadhi ya dawa za kukinga vijidudu zinaweza kusababisha maumivu ya matumbo au kuharisha, hivyo wagonjwa wanapaswa kuacha kutumia dawa hizo, baada ya kuona hali hiyo inatokea.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-28