Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-30 21:30:17    
AIDS (UKIMWI) 09

cri
    Kitu gani kinamfanya mtu mwenye viini vya UKIMWI aanzwe na ugonjwa baada ya kuweza kukaa na viini hivyo mwilini mwake kwa siku nyingi bila matatizo?

    Haijulikani vizuri bado, lakini utafiti ungali unaendelea. Hata hivyo yaelekea kwamba wakati mwingine hali hiyo huenda ikasababishwa na mabadiliko fulanifulani yanayovikumba viini hiyvo vya ugonjwa, na wakati mwingine hali hiyo hutokana na mabadiliko yanayomkuba mtu mwenyewe aliye na viini hivyo?kwa mfano imethibitika kwamba UKIMWI Baridi ya akina mama huweza kubadilika na kuwa UKIMWI Moto mara tu wanapokumbwa na mabadiliko ya kubeba mimba.

    Jambo lingine ambalo huweza pia kutokea na kusababisha hali hiyo ni ikiwa mtu huyo aliyekuwa anaishi na viini vichache vya UKIMWI mwilini mwake bila matatizo, kwa bahati mbaya ataanza bila kujua kuingiza mwilini kwa upya idadi kubwa ya viini vya UKIMWI kwa njia mbalimbali.

    Mama mwenye UKIMWI(AIDS) humwambukizaje mwanae?

    Mama anaweza kumwambukiza mwanae kwa njia zifuatazo:

    1. Kwa kupitia sehemu inayounganisha mama na mtoto katika nyumba ya uzazi, viini vya UKIMWI kutoka damu ya mama vinaweza kumwingia mtoto akiwa bado tumboni, yaani kabla ya kuzaliwa.

    2. wakati wa kujifungua damu (yenye viini vya UKIMWI) inayomtoka mama inaweza kumwingia mtoto.

    3. kwa nadra sana mama anaweza akamwambukiza mwanae wakati wa kunyonyesha, kutokana na viini vya UKIMWI vitakavyoweza kuwemo katika hayo maziwa atakayokuwa ananyonya mtoto wake.

    4. Pia kutokana na uhusiano na ushirikiano wa karibu sana uliopo kati yao, kwa nadra mama asiye mwangalifu anaweza kwa njia ya kujeraha mwilini au kwa njia nyingine za uzembe kusababisha damu au majimaji mengine toka mwilini mwake yamwingie mwanae wakati anapomshika; au wakati anapomwogesha; au anapomlisha; au anapochezacheza naye, n.k.

    Je, ni vizuri watoto wenye UKIMWI Baridi waruhusiwe kukaa shuleni pamoja wa wenzao?

    Hakuna ubaya kufanya hivyo, mradi tu uangalifu mkubwa zaidi uchukuliwe kuhakikisha kwamba endapo watajeruhiwa au kutokwa na damu kwa njia yeyote ile wanapewa haraka huduma kuzuia damu zao zisiwafikie watoto wengine.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-30