Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-30 21:35:40    
Wahitimu wa vyuo vikuu vya China wajitafutia ajira mwaka 2004

cri
Mwezi Julai mwaka huu, kikundi kingine cha wanafunzi wa vyuo vikuu wahitimu na kuondoka vyuoni vikuu. Mwaka huu, wanafunzi waliohitimu kutoka vyuo vikuu watafikia milioni 2.8, likiwa ni ongezeko la 30% kuliko mwaka jana. Hivyo, hali ya upatikanaji wa ajira kwa wanafunzi wa mwaka huu si nzuri sana. Wizara ya elimu ya China na vyuo vikuu mbalimbali vya China vilizingatia kazi ya kuwasaidia wanafunzi kutafuta ajira, ambapo vilichukua hatua mbalimbali ili kupunguza ugumu kwa wanafunzi kupata ajira.

    Wang Shuheng ni mwanafunzi aliyehitimu kutoka Shule ya ufundi wa mashine na umeme ya Mkoa wa Henan, katikati ya China. Mwezi Disemba mwaka jana alisaini mkataba wa kazi na Kampuni maalumu ya magari ya China. Mwezi Julai mwaka huu, baada ya kuhitimu kutoka shuleni atakuwa bwana mauzo wa kampuni hiyo. Kuhusu ajira hiyo, Ndugu Wang Shuheng aliridhika sana na ajira hiyo akisema?

    "naona kazi hii ni nzuri. Naipenda kazi hii, kampuni hiyo inaniridhisha, nadhani nitakuwa na maendeleo makubwa."

    Ngudu Wang alimwambia mwandishi wa habari kuwa, alipata ajira hiyo kutokana na msaada wa kituo cha kuwasaidia wanafunzi kupata ajira katika shule yake. Kituo kicho kilifanya mawasiliano na makampuni na mashirika mbali mbali ya serikali ili kupata habari kuhusu nafasi za kazi. Hatimaye, habari hizo zilipelekwa kwa wanafunzi. Mbali na hayo, kituo hicho kilifanya mawasiliano na makampuni mbalimbali na kuwasaidia wanafunzi kuwa na elimu husika kabla ya kuhitimu masomo yao.

    Tokea majira ya baridi mwaka uliopita, shule ya ndugu Wang ilifanya mikutano kadhaa ya kuwasaidia wanafunzi kujitafutia ajira, makampuni mengi maarufu yalihudhuria mikutano hiyo. Mikutano hiyo iliwapitia ajira wanafunzi zaidi ya elfu 4. na Ndugu Wang alipata ajira yake kwenye mikutano hiyo.

    Sasa wanafunzi wengi wa shule ya ufundi wa mashine na umeme ya Henan wamepata ajira. Mkurugenzi wa kituo cha kuwasaidia wanafunzi kupata ajira cha shule hiyo Bw. Li Zengchen alijulisha kuwa:

    " ili kuwasaidia wanafunzi waliohitimu kutoka shuleni kupata ajira, viongozi wa shule walifanya jitihada kubwa. Mwaka huu, zaidi ya wanafunzi 2300 walipata ajira, hadi sasa, 90% ya wanafunzi wameshapata ajira?"

     Bw.Li Zengchen alisema kuwa, shule siku zote inazingatia kazi ya kuwasaidia wanafunzi kupata ajira. Miaka mitano iliyopita, shule ilianzisha kituo cha kuwasaidia wanafunzi kupata ajira. Mbali na hayo, shule hiyo pia ilianzisha "Baraza la mameneja waendeshaji wa shule, makampuni 60 ya China yalikuwa wajumbe wa baraza hilo. Katika miaka mitatu ya masomo, mbali na kuwa shuleni, wanafunzi wanaweza kufanya mazoezi ya kazi katika makampuni mablimbali.

    Kama ilivyofanya shule ya ufundi wa mashine na umeme ya Henan, zaidi ya shule elfu 1 za China zinatilia maanani sana kuwasaidia wanafunzi waliohitimu kupata ajira. Ili kuwasaidia wanafunzi kupata ajira, vyuo vikuu vya Beijing, Chuo Kikuu cha Qinghua, Wuhan na vyuo vikuu vingine vilianzisha kikundi cha kuwasaidia wanafunzi kupata ajira kilichoongozwa na Mkuu wa chuo kikuu. Mbali na hayo, idadi ya wanafunzi waliopata ajira ni kama kigezo cha kupima kazi ya wakuu wa vyuo vikuu; vyuo vikuu kadhaa vilianzisha masomo ya ufundi na kuwaandaa wanafunzi ili kuwaongeza uwezo wa ushindani katika soko la ajira. Wakati huo huo, wizara ya elimu na China na mashirika ya elimu ya sehemu mbalimbali za China yamechukua hatua mbalimbali zenye mafanikio. Mkurugezi wa ofisi ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika wizara ya elimu ya China Bw. Liu Dawei alisema kuwa:

    " tunawatia moyo wanafunzi kufanya kazi katika sehemu ya magharibi ya China, vijijini na sehemu nyingine zinazohitaji wahitimu wa vyuo vikuu, wanatazamiwa kushiriki katika kazi ya uendeshaji wa sehemu ya Magharibi ya China, kukuza ujenzi wa kituo kikongwe cha viwanda cha Kaskazini-Mashariki ya China, kazi ya kuboresha elimu ya msingi ya magharibi ya China, ujenzi wa mfumo wa afya vijijini na miradi mingine mikubwa ya taifa."

    Habari zinasema kuwa, mwaka huu, serikali ya China imeendelea kutekeleza mpango wa kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu wajitolee kufanya kazi katika magharibi ya China. Wanafunzi hao watakapomaliza kufanya kazi katika sehemu ya Magharibi ya China wataweza kuendelea masomo yao ya chuo kikuu au watapewa misaada mbalimbali na serikali.

Idhaa ya kiswahili 2004-06-30