Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-01 20:28:17    
Zaidi ya kilomita laki 2 za barabara za vijijini zitajengwa mwaka huu katika sehemu za kati na magharibi za China

cri

    China itazidi kutilia mkazo ujenzi wa barabara za vijijini. Mwaka huu ujenzi wa barabara za vijijini umefikia kilomita laki 2 na elfu 5, zikiwemo kilomita laki 1 na 65 elfu za barabara zinazojengwa, kilomita elfu 40 za barabara zitakazojengwa.

    Kutokana na maelezo ya mkutano kuhusu ujenzi wa barabara za vijijini katika sehemu za kati na magharibi uliofanyika mjini Wuhan mwezi Juni, mwandishi wetu wa habari alipata kujua kuwa, mwaka 2003, baada ya Wizara ya Mawasiliano ya China kuweka lengo la "kujenga barabara za vijijini kwa makini, ili kuchangia ukuzaji wa miji na kuwawezesha wakulima kutumia barabara za lami na saruji", ujenzi wa barabara za vjijini umeongezewa nguvu, na urefu wa barabara za lami na saruji umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Mwaka huu urefu wa barabara zilizojengwa umefikia kilomita 102 elfu, na uwekezaji ulikuwa yuan bilioni 718. Hadi sasa, mbali na mkoa unaojiendesha wa Tibet, wilaya zote katika sehemu za magharibi zina barabara za lami. Na zaidi ya tarafa elfu 1 katika sehemu za kati na vijiji zaidi ya elfu 23 katika sehemu za mashariki vimeanza kuwa na barabara za lami katika mwaka mmoja.

    Ujenzi wa barabara za vijijini umezifanya barabara za vijijini kuwa na sura mpya, kwani ubora na urefu wa barabara umeongezeka kwa kiasi kikubwa, usafirishaji wa barabarani umepata maendeleo makubwa. Hayo yote yameweka mazingira mazuri kwa mazao ya kilimo na uchumi kubadilika kuwa bidhaa, na kilimo cha kijadi kubadilika kuwa kilimo chenye thamani kubwa kinachofuata mahitaji ya masoko. Ujenzi wa barabara za vijijini umewawezesha wakulima waweze kusafiri kwa urahisi, haraka na kwa usalama. Kuboreshwa kwa mazingira ya maisha ya wakulima, kuongezeka kwa mawasiliano kati ya wakazi wa mijini na vijijini, na kuharakishwa kwa upashanaji habari, si kama tu kumeboresha ubora wa maisha ya wakulima, bali pia kumeinua kiwango cha ustaarabu wa jamii za vijijini.

    Ujenzi wa barabara za vijijini umeungwa mkono kwa dhati na wakulima wote, na umesifiwa kuwa ni "ujenzi unaokidhi mahitaji ya wananchi" na "ujenzi wa kuwanufaisha wananchi". Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali la China vinauzingatia sana ujenzi wa barabara za vijijini, na wakulima wote pia wana matarajio makubwa kuhusu ujenzi huo. Habari zinasema kuwa, mwaka huu China itaanzisha miradi 200 ya ujenzi wa barabara katika wilaya mbalimbali katika sehemu ya magharibi, miradi elfu 1 ya ujenzi wa barabara katika ngazi ya tarafa ya sehemu ya kati na miradi elfu 3 ya ujenzi wa barabara za vijijini katika sehemu ya mashariki.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-01