Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-01 21:10:32    
Ubandikaji Karatasi

cri

   

   

    Zhizha maana yake ni taswira zilizobandikwa kwa karatasi, nazo zinatengenezwa kwa karatasi za rangi anuwai, vipande vidogo vya mianzi, matete na seng'enge. Hatua za kutengeneza ni hivi: kwanza kuunda miimo yake kwa vipande vidogo vya mianzi, mabua ya matete na seng'enge, kisha kubandika karatasi za rangi zilizokatwakatwa na kupambwapambwa, mwishowe hutokea taswira mbalimbali za kuvutia. Ikiwa ni taswira ya mtu hufunga kichwa cha udongo, kutia rangi za uso na pia kumshikisha ala za vita mikononi mwake.

    Ukubwa wa zhizha ni tofauti: jumba la ghorofa, jukwaa na hekalu hufika mita kadhaa, mtu mkubwa ni zaidi ya mita 0.67 na aliye mdogo hafiki mita 0.61. Wasanii wanabobea ustadi wa kijadi na umahiri wa kutengeneza taswira mbalimbali zenye maumbo tofauti ya kuvutia.

    Sanaa ya zhizha imekuwa na historia ya zaidi ya miaka 1000 na kuenezwa kwa mapana katika Jimbo la Fujian lililoko pwanipwani ya kusini mashariki mwa China, hasa pande za kusini mwa Fujian desturi na mila za kienyeji na utamaduni jadiia vimeiletea maendeleo mazuri sanaa hiyo. katika maeneo ya Putian, Huian, Zhangzhou na kwengineko kila sikuku ya chipuko, ya taa na sikukuu ya katikati ya majira ya mrao watu huweka majukwaa, milango ya bandia, kuwasha fataki na kutazama taa za rangi, wakati kama huo zhizha ni pambo lisilokosekana. Ikitokea shughuli muhimu, takriba kila familia huwaalika wasanii kuwatengenezea zhizha mbalimbali, kama vile wakisherehekea siku ya kuzaliwa huetengeneza taswira za watu wanaojiunga na karamu na mabanda ya kutakia maisha marefu, watu wakijenga nyumba mpya au kufungua maduka, hutengeneza majukwaa, majumba ya ghorofa na watu wanaoombea baraka, hali ya kuwa kwenye sherehe ya ndoa hutengeneza zhizha maalumu.

    Zhizha huonyesha maudhui kuhusu hadithi jadiia, ngano na mapokeo, wahusika wa opera, maisha ya kawaida ya watu, kasri, jumba la ghorofa ya ngoma saa na majumba ya kuhifadhia misahafu.

   

   

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-01