Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-02 19:17:14    
Mpunga wa chotara wa China wapandwa katika nchi mbalimbali duniani

cri

    Mtaalamu maarufu wa China wa mpunga chotara Bwana Yang Jubao alisema "Sayansi haina mpaka, wanasayansi wa China wana matumaini kuwa wataweza kutoa mbegu bora kabisa za mpunga chotara kwa wakulima wa dunia nzima",.

    Kutokana na kusaidiwa na serikali ya China, wanasayansi wa kilimo wa China wametoa teknolojia zilizopevuka kuhusu upandaji wa mpunga chotara na kutoa mbegu bora za aina mpya kwa nchi nyingi duniani. Hivi sasa mpunga chotara wa China umepandwa katika sehemu mbalimbali duniani na unachangia katika suala la lishe kwa wananchi wa sehemu kadhaa duniani.

    Bwana Yang Jubao alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Philippines ni mtu wa kwanza mwene shahada ya Udaktari wa somo la mpunga nchini China. Mwaka 1992, Bwana Yang alipelekwa na Wizara ya kilimo ya China kuwa mkuu wa Tawi la Kikundi cha washauri wa mpunga chotara cha Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa nchini Vietnam na pia alikuwa mshauri wa mpunga chotara duniani wa Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa.

    Alipofanya kazi nchini Vietnam, Bwana Yang mara kwa mara alikwenda mashambani kuwaelekeza wakulima wa huko kupanda mpunga aina mpya ya chotara, na alisifiwa kuwa ni ofisa pekee wa Umoja wa Mataifa aliyekwenda mashambani Vietnam.

    Kutokana kuungwa mkono na Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa, Bwana Yang aliingiza mpunga chotara na mbegu bora nyingine kwa ajili ya Vietnam, juhudi zake hizo zilisaidia Vietnam kuwa nchi ya tatu inayouza mchele mwingi zaidi duniani, kutoka kuwa nchi yenye ukosefu mkubwa wa chakula baada ya kufanya bidii kubwa za muda mfupi. Mafanikio hayo ni mfano wa kuigwa katika mradi wa utoaji misaada wa Shirika la kilimo na chakula ambao uliwekezwa kwa kiasi kidogo kabisa lakini ulipata ufanisi mkubwa kabisa. Bwana Yang pia alisifiwa na kupewa nishani iliyotolewa na serikali ya Vietnam kutokana na kazi yake nzuri.

    Mwaka 1974, mwanasayansi wa China Bwana Yuan Longping aliofanikiwa kuotesha aina ya kwanza ya mbegu ya mpunga chotara. Utoaji wa mpunga chotara huwa ni wa juu kwa asilimia 15 hadi 20 kuliko mpunga wa kawaida. Baada ya kufanya juhudi za uenezaji, eneo la upandaji wa mpunga chotara limechukua nusu ya eneo la upandaji wa mpunga nchini China, na utoaji wa kila hekta wa mpunga uliongezeka na kufikia tani 6.2 kutoka tani 3.5.

    Zaidi ya miaka 10 iliyopita, China, Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, Taasisi ya mpunga ya kimataifa, Shirika la mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa na Benki ya maendeleo ya Asia zilitoa misaada mikubwa ya hatua madhubuti kwa utafiti wa uzalishaji wa mpunga chotara katika nchi kadhaa barani Asia, pamoja na kuotesha mbegu za mpunga chotara, kuzalisha mbegu na zana za utafiti.

    Takwimu zimeonesha kuwa, katika mwaka 2003 tu, maeneo ya upandaji wa mpunga chotara yalifikia hekta milioni moja katika nchi za Bangladesh, India, Indonesia, Myanmar, Philippines na Vietnam. Nchini Misri mpunga chotara ulioingizwa kutoka China hata unaweza kukua vizuri kwenye ardhi zenye chumvi na magadi, na utoaji wake huongezeka kwa asilimia 35 kuliko mpunga wa kawaida. Hivi sasa mbegu mpya zilizotengenezwa na China huuzwa kwenye soko la nchini na la nchi za nje kwa wakati mmoja.

    Bwana Yang alisema kuwa, uzalishaji wa mpunga chotara unafanya kazi kubwa kwa nchi zenye upungufu wa mashamba, ongezeko kubwa la idadi ya watu na mapato kidogo ya nguvu kazi, ili kuongeza uzalishaji wa nafaka na kuhakikisha usalama wa nafaka. Hivi sasa mahitaji ya mchele yanaongezeka pia barani Afrika, Latin Amerika na Ulaya. Barani Afrika, hata nchi ya Guinea na nyinginezo ambazo zamani hazikupanda mpunga hivi sasa pia zimeanza kupanda mpunga chotara.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-02