Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-02 21:53:41    
Mvumbuzi wa michongo ya mng'arisho juu ya vyombo vya kauri

cri

    Joka kubwa anaruka angani, mwili wake nusu unaonekana nusu umejificha mawinguni, macho yake yanang'ara kifahari, pembe za kichwani, magamba ya mwilini na kucha za miguuni, vyote vinaonekana kuwa ni vigumu na vyenye nguvu. Mnyama huyu wa kishani na anayeonekana kama hai, si mnyama anayeruka angani wala anayeogelea baharini, bali ni mchongo juu ya sahani kubwa na nyeusi ya kauri uliochongwa na Bw. Zhai Jiucheng kwa ustadi wa kioekee.

    Zhai Jiucheng alivumbua ustadi mpya wa michongo ya mng'arisho juu ya vyombo vya kauri.

    Sifa za ustadi huo ni nyingi sana. Kwenye tabaka la mng'arisho lenye unene usiozidi mm 1 juu ya vyombo vya kauri, msanii anachonga michongo mbalimbali kwa mbinu tofauti. Akitumia sifa za nguvu, kuakisi mwanga na tabia ya fizikia anaonyesha matokeo ya kisanii yenye rangi nyeusi, nyeupe na yakijivujivu kama vile sanamu za jasi, picha za watu, michongo ya mawe, vyombo vya shaba nyeusi, michoro iliyochapishwa kwa mabamba yaliyochongwa nakshi na michoro ya kumwagia wino mweusi. Kadhalika, michoro hiyo haidhuriwi na usafishaji kwa maji ya kawaida na hata maji mbalimbali yenye kemikali.

    Michongo ya Zhai Jiucheng ilisifiwa sana na wasanii wa nchini na nchi za nje katika maonyesho ya kwanza ya sanaa ya China yaliyofanyika huko Guangzhou, mwaka 1993. Picha ya Mao Zedong iliyochongwa na Zhai kwa hisia nyingi za heshima inaonyesha kikamilifu sura tukufu ya kiongozi huyu marehemu na sasa picha hii inahifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho ya Mapinduzi ya China. Picha ya vichwa vya Samaranchi na mkewe iliyochongwa na Zhai kwa hisia ya upendo inaonyesha kutoka pande zote sura halisi za watu hawa maarufu na ilisifiwa sana na wao wenyewe.

    Baada ya kupata hataza ya uvumbuzi huo, Zhai Jiucheng anaanza utafiti mpya wa michongo ya mng'arisho wa rangi juu ya vyombo vya kauri. "Kufuatilia sanaa isiyo na mwisho kwa kutumia maisha yenye kikomo" ndio nia ya Zhai Jiucheng katika maisha yake.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-02