Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-06 09:22:19    
Tangazo kuhusu mashindano ya chemsha bongo

cri
    Idhaa ya Kiswahili inataka kuwaarifu wasikilizaji wetu kuwa, Mashindano ya chemsha bongo ya mwaka jana kuhusu utamaduni na utalii wa eneo la magharibi la China, yalifanyika mwezi Agosti hadi Desemba mwaka jana kupitia matangazo ya lugha 43 za Radio China ya kimataifa na tovuti za lugha za kigeni kwenye mtandao wa internet yamemalizika rasmi.

    Mashindano hayo yalilenga kufahamisha ujuzi kuhusu mazingira ya kimaumbile, vivutio vya utali, historia na utamaduni wa makabila madogomadogo ya China katika sehemu ya magharibi ya China. Mashindano hayo yalipata majibu kutoka kwa wasikilizaji zaidi ya laki 4 kutoka nchi na sehemu 134.

    Wasikilizaji 10 kutoka nchi za Australia, Nepal, India, Sri Lanka, Vietnam, Iran, Hungary, Colombia, Benin na Malaysia walishinda katika mashindano hayo na wamepata tuzo maalum. Tarehe 2 Juni, naibu spika wa Bunge la umma la China Bwana Xu Jialu alikutana na washindi hao 10 na kuwatia moyo waendelee kuimarisha urafiki na wananchi wa China.

    Idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa imepata jumla ya majibu 80, wengi wa waliotoa majibu, walijibu kwa usahihi maswali 9.

    Bwana Ras Franz Manko Ngogo wa P.O.Box 71 Tarime, Mara Tanzania alituletea jibu zuri na makala iliyoandikwa vizuri, tulifanya juhudi kumsaidia kugombea tuzo maalum na apate Ushindi, lakini kutokana na hali halisi ya majibu mazuri na makala ya kuvutia zaidi zilizoandikwa na wasikilizaji wa idhaa nyingine, uamuzi wa mwisho wa Kamati ya uchaguzi ya CRI ni kuwa, Bwana Ngogo amekuwa mshindi wa kupata nafasi ya kwanza. Hakupata ushindi wa nafasi maalum.Na msikilizaji wetu mwingine Xavier L. Telly Wambwa wa P.O.Box 2287 Bungoma Kenya amechaguliwa kuwa mshindi wa nafasi ya tatu.

    Kutokana na kiasi cha majibu tuliyopata kutoka kwa wasikilizaji wetu, ni asilimia chache tu ya wasikilizaji waliweza kupewa nafasi. Wengine wote walioshiriki katika mashindano hayo watapata kadi ya kumbukumbu.

    Ni matumaini yetu kuwa wasikilizaji wetu hamtakata tamaa, kwani mashindano ya chemsha bongo yanayoandaliwa kila mwaka na CRI yamesifiwa na kuungwa mkono na idara nyingine husika. Tumeahidiwa kuwa, katika mashindano yatakayoandaliwa mwaka huu, washindi wa tuzo maalum wataongezeka zaidi, huenda wasikilizaji kutoka kila sehemu watapata nafasi ya kuchaguliwa. Hivi sasa mashindano hayo yanakaribia kuandaliwa tayari, tumeambiwa kuwa mashindano ya chemsha bongo ya mwaka huu yataanzishwa rasmi mwezi ujao, tukipata habari tutawaarifu rasmi wasikilizaji wetu.

    Na idhaa ya kiswahili ya CRI pia imeanza kuandaa mashindano madogo ya kuandika makala kuhusu "Mila za China", au unaweza kuandika makala kuhusu mila za nchi yenu au mila za kabila lako, na ututumie. Kila atakayeandika atapaka zawadi ndogondogo, na makala hizo zitatangazwa kwenye vipindi vyetu na kuwekwa kwenye tovuti yetu yenye anuani ya cri.cn. Karibuni.

    Ni matumaini yetu kuwa wasikilizaji wetu watashiriki kwa juhudi katika mashindano ya chemsha bongo ya mwaka huu yatakayoanzishwa mwezi ujao, na kushiriki katika uandikaji wa makala kuhusu mila za makabila mbalimbali .

2004-07-06