Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-06 17:39:45    
Mavuno yatakuwa mazuri kwa kushughulikiwa na waziri mkuu

cri

    Tarehe 5 Julai katika kijiji cha An Fuzhen mkoani Hubei nchini China, ngano ilikuwa imekomaa tayari kuvunwa. Katika siku hiyo mkulima Zeng Xianghua aliamka mapema na alitundika kitambaa kirefu uani kilichosomeka, "Waziri mkuu tufuatilia, wanasayansi wanatuletea mbolea". Wanakijiji walikwenda na kujaa uani baada ya kusikia habari hiyo.

    Wataalamu wa kituo cha kueneza teknolojia ya kilimo cha Wizara ya Kilimo ya China walikwenda nyumbani kwake na mbolea yenye mchanganyiko kisayansi kilo 1000, mkulima Zeng Xianhua alifarijika na kusema, "Nashukuru sana Chama, tukiwa tunashughulikiwa na waziri mkuu, mavuno yetu mazuri mwaka huu hayatakuwa ndoto."

    Kutokana na maelezo ya mwanakijiji huyo kisa chenyewe ni hiki: Tarehe 9 Juni, alipokuwa akifanya kazi shambani kwa bahati alikuta waziri mkuu Wen Jiabao aliyekuja kijijini kufanya ukaguzi. Waziri mkuu alipozungumza naye kuhusu hali ya maisha yake, alimwuliza shida aliyo nayo, Zeng Xianhua alitoa ombi lake kuwa kama wataalamu wa kilimo wangekuja kijijini na kupima udongo ili tujue elementi gani inakosekana mashambani, kwa kufanya hivyo tungeweza kutia mbolea kwa uhakika. Waziri mkuu mara akamwahidi kuwa atamsaidia kutatua tatizo hilo. Siku ya pili tu wataalamu wa kilimo walikuja nyumbani kwake na kuuliza mbolea alizotumia. Kutokana na kuwa ameweka mbolea siku chache zilizopita, matokeo ya upimaji wa udongo hayataweza kuwa ya kweli, wataalamu walimwambia, watakuja tena mwishoni mwa mwezi huo.

    Mtaalamu wa kilimo kutoka Ofisi ya Kilimo katika mkoa wa Hubei Bw. Xu Nenghai alituambia, tarehe 30 Juni wataalamu wa shirika la mbolea mkoani walikuja kijijini, walipima udongo wa mashamba yote kijijini hekta 267, wakagundua kuwa mashamba yanakosa potassium. Shirika hilo likaanza kuzalisha mbolea yenye mchanganyiko wa nitrogen, phosphorus na potassium kwa uwiano wa 22, 10 na 20.

    "Mashamba yangu je?" "Uwiano gani utafaa katika mbolea ya mashamba yangu?" Wanakijiji walikuwa wanauliza na Bw. Xu Nenghai aliwaambia, wako katika uchambuzi na watawaletea matokeo, aliwaambia kuwa Idara ya Kilimo mkoani imechagua mashamba ya kijiji hicho kuwa kituo cha kupima hali ya udongo kwa ajili ya kufahamu hali ya udongo mashambani mkoani kote na itatoa huduma siku zote." Kusikia maneno hayo, wanakijiji walifurahi sana. Bw. Xu aliwaambiaa waandishi wa habari kuwa idara hiyo imekwisha pima mashamba hekta laki 6.7 na imedhamiria kupima mashamba yote mkoani yenye hekta milioni 3.4 katika miaka minne hivi.

    Naibu mkurugenzi wa Kituo cha Kueneza Teknolojia ya Kilimo mkoani Hubei Bw. Su Tieshen alisema, "Ombi la mkulima Zeng Xianhua ni ombi la wakulima wote wa China, licha ya kuwa inatupasa tutatue tatizo lake binafsi pia tunapaswa kutatua matatizo ya wakulima wote na kuhakikishwa kwa mfumo, na tuwe na fikra za kuwahudumia wakulima daima."

    Mkulima Zeng Xianghua alimshika mkono wa mwandishi wa habari akisema, "nyumbani kwangu kuna mashamba nusu hekta, kila mwaka natumia yuan 1,700 kununua mbolea za chumvi, lakini kutokana na kutofahamu mbolea ya aina gani inahitajika mashambani, mbolea nyingi zilitumika bila haja, ni sawa na kutumia dawa bila kufahamu ugonjwa wenyewe, pesa zilitumika bure." Aliongeza kusema kuwa "Tukiwa tunasaidiwa na mbolea zinazofaa pamoja na sera nzuri za serikali, sisi wakulima tunajawa na matumaini makubwa."

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-06