Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-07 15:57:00    
Sayansi na teknolojia zainua kiwango cha maisha

cri

    Piano inaweza kupiga muziki wa kupendeza, na mtu anaweza kudhibiti friji yake ya nyumbani hata akiwa umbali wa kilomita elfu 1 kutoka nyumbani kwake. Miujiza hiyo ilitokea hivi karibuni katika maonesho ya sayansi na teknolojia, ambayo katika siku ya kwanza yalivutia wakazi wa Beijing zaidi ya 2000 kwenda kuyaangalia bila kujali mvua iliyokuwa ikinyesha. Hivi sasa, wachina wanaona kuwa sayansi na teknolojia zimekuwa na uhusiano mkubwa zaidi na maisha yao.

    Ili kueneza elimu ya kisayansi na kuendeleza teknolojia ya kisayansi miongoni mwa umma na kuinua kiwango cha elimu yao ya sayansi na teknolojia, idara husika za serikali ya China kila mwaka zinafanya shughuli za wiki ya sayansi na teknolojia zinazolenga kueneza elimu hiyo miongoni mwa jamii. Katika wiki ya sayansi na teknolojia ya mwaka huu, mambo yaliyofuatiliwa zaidi na watu ni namna ya kuunganisha maisha yao na elimu ya sayansi na teknolojia. Katika maonesho yaliyofanyika mwaka huu mjini Beijing ambayo yalijulikana kwa "familia yenye maisha mazuri", watazamaji waliona kuwa piano ambayo kwa kawaida inapigwa na mwanamuziki kwa mikono, iliunganishwa na mashine moja yenye software, na inapiga muziki yenyewe.

    Licha ya hayo, watazamaji waliona kuwa endapo mwenyewe akiunganisha kampyuta yake na mtandao wa Internet, hata akiwa safarini anaweza kutumia friji na micro-wave oven, kutumia mfumo wa ulinzi wa usalama nyumbani ambao utatoa onyo pindi mtu wa nje akiingia katika nyumba yake. Miujiza hiyo iliwafurahisha watazamaji, hususan watazamaji vijana. Mwanafunzi kutoka shule ya msingi ya Cuiwei, Beijing He Yuchen aliporejea nyumbani baada ya kuangalia maonesho hayo, bado alifurahi sana, akisema,

     "Kitu kilichonipendeza zaidi ni choo ambacho nikikisogelea karibu, kinafungua kifuniko chake chenyewe. Kwa kudhibitiwa na kompyuta, choo kile kinaweza kukadiria kiasi cha maji yanayotumika kutokana na hali ya matumizi, kutoa harufu nzuri ya kunukia na kumaliza kazi ya kusafisha. Ninataka sana familia yangu kuwa na choo cha namna ile."

    Mwanafunzi He Yuchen alisema kuwa katika maonesho yale kulikuwa na vitu vingi vya kustaajabisha watu ambavyo ni pamoja na mapazia ya madirisha yanayoweza kujifunga na kujifungua yenyewe, roboti iliyoweza kuongea, jiko la umeme linaloweza kupika wali lenyewe katika saa ile iliyotegwa, vitu hivyo alidhani viko tu katika hadithi, lakini hivi sasa alivishuhudia, tena familia yake itaweza kuvitumia vitu hivyo vya ajabu katika siku chache za baadaye.

    Kama alivyo mwanafunzi huyo wachina walio wengi wanatarajia sayansi na teknolojia kuinua kiwango cha maisha yao. Matarajio yao hayo yatakuwa mambo ya kweli hatua kwa hatua. Katika miaka 15 ijayo, China itakabiliwa jukumu la kujenga kwa pande zote jamii yenye kiwanago cha maisha mazuri. Tukitaka kufanikisha jukumu hilo, tunapaswa kuwa na msimamo wa kutoa kipaumbele kwa manufaa ya umma na kuwa na mtazamo wa kisayansi wa kuwania maendeleo ya pande zote, yenye uwiano na endelevu. Mwanakamati ya mambo ya taifa Bw. Chen Zhili alisema kuwa kutokana na harakati za kueneza sayansi na teknolojia za umma ambazo zinaambatana na hali halisi, Maisha ya watu na yenye mvuto, ari ya uvumbizi ya watu katika sekta mbalimbali za jamii yatahamasishwa, na itakuwa ni nguvu ya kujenga jamii yenye kiwango cha maisha bora. Bibi huyo alisema,

    "Katika siku za baadaye, iko haja kubwa kwa China kuuchukulia uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia kuwa nguvu ya kuendeleza viwanda vya kisasa na kuwa na maendeleo ya uchumi wenye kiwango cha juu cha sayansi na teknolojia, ufanisi mkubwa, matumizi madogo ya rasilimali, uchafuzi mdogo wa mazingira ya asili na kutumia viliivyo ubora wa nguvu-kazi."

    Katika mji wa Shanghai, ulio umbali wa kilomita zaidi ya 1000 kutoka Beijing, wanamji walishiriki shughuli zaidi ya 300 za kisayansi na kiteknolojia. Katika wiki ya harakati za sayansi na teknolojia, kulikuwa na maonesho ya kimataifa yaliyoandaliwa na Japan na Norway, semina ya kimataifa ya kueneza sayansi na teknolojia ambayo yalihudhuriwa na wanamji zaidi ya milioni 3. Mwalimu mwanmke wa sekondari ya chuo kikuu cha Fudan, Shanghai, bibi Li Qiu alisema,

    "Kitu kilichonipendeza zaidi katika maonesho hayo ni kutumia kwa mara nyingine tena vitu vilivyokwishatumiwa. Baada ya kurejea nyumbani, nitamtengenezea mtoto wangu, nembo moja ya karatasi, ambayo itaimarisha wazo lake la kuhifadhi mazingira ya asili na kupunguza matumizi ya rasilimali. Ninatumaini kuwa mtoto wangu atakuwa na wazo moja la kuvumbua zana zinazoweza kusafisha hewa au roboti ya mimea, itaweza kulinda misitu, hizi zitakuwa kazi nzuri sana."

    Hivi sasa, China inajitahidi kutekeleza mkakati wa maendeleo endelevu, hivyo watu wa China wanatakiwa kubadilisha mawazo yao, waboreshe maisha yao kwa teknolojia ya kisayansi na isiyoleta uchafuzi kwa mazingra na kujenga familia za wachina zenye maisha bora. Kuhusu suala hilo, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Wuhan Chang Bao alipendekeza kuwa idara za serikali ya China zinapaswa kuimarisha uenezi wa elimu ya sayansi na teknolojia na kuongeza kwa haraka sifa za wachina za elimu ya sayansi na teknolojia.

    Alisema kuwa hivi sasa anaona sayansi na teknolojia ziko karibu na familia za watu, ambao wanatumia vitu vingi vya teknolojia ya kisayansi. Hivyo anaona kuwa kuna haja ya kueneza zaidi elimu ya sayansi na teknolojia, hususan zile zinazonufaisha maisha ya watu, na kufanya watu kuona kuwa sayansi na teknolojia ziko katika maisha yetu.

   

Idhaa ya kiswahili 2004-07-07