Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-07 16:01:23    
China yatengeneza meli ya kisasa ya uchunguzi wa kisayansi

cri
    Habari kutoka katika sherehe za kuadhimisha miaka 40 ya kuanzishwa kwa idara ya elimu ya sauti ya taasisi ya taifa ya sayansi zinasema kuwa, meli hiyo ya uchunguzi inayogharimiwa na taasisiya taifa ya sayansi ina uwezo wa kubeba tani 2,500, sehemu ya chini ya meli hiyo iko katika kina cha mita 6.5, kasi yake kubwa kabisa ni 9 notikmaili 15, na inaweza kusafiri notikmeili 8,000 kwa mfululizo. Meli hiyo yenye sehemu mbili zinazoungana, inaweza kusafiri kwa usalama wakati upepo wa nyuzi 11 unapovuma. Meli hiyo inatarajiwa kuanza kutumika mwaka 2005. Hivi sasa, zabuni ya usanifu wa meli hiyo imekwisha tolewa, idara husika ya usanifu ikombiono kukamilisha kazi hiyo.

    Meli hiyo yenye sehemu mbili zinazounganishwa pamoja ambayo sehemu yake ya chini haiingiisana katika maji, ni ya kiwango cha juu cha teknolojia. Meli hiyo inaweza kusafiri hata katika mawimbi makubwa, na watu walioko katika meli hiyo wasisikie sana kizunguzungu. Hivyo meli ya aina hiyo inapendwa na wachunguzi wa sayansi ya bahari na ina matumizi mengi katika uchunguzi na utafiti wa baharini. Katika miaka ya karibuni, nchi nyingine zikiwemo Marekani, Japani na Korea ya kusini, zilitenga fedha kutengeneza meli za uchunguzi za aina hiyo.

    Meli hiyo inatengenezwa na idara ya elimu ya sauti ya taasisi ya sayansi ya taifa kwa kusaidiwa na idara ya bahari ya kusini na idara ya mitambo inayojiendesha ya Shenyang, kutokana na mpango wa maendeleo ya kipindi cha muda mrefu na wastani pamoja na mahitaji ya idara zinazohusika na bahari za taasisi ya sayansi ya taifa. Meli hiyo itatumika kwa utafiti na majaribio ya fizikia ya sauti ya maji, uhandisi wa sauti ya maji na maroboti ya chini ya maji ya bahari, na kuwa sehemu moja ya mifumo ya upimaji wa mazingira na upashanaji habari. Meli hiyo inaweza kufanya uchunguzi wa sayansi wa elimu za aina nyingi zikiwemo za sauti ya maji na bahari kwenye bahari ya karibu na bahari ya mbali.

    Meli za uchunguzi wa sayansi ya bahari za China, hususan za idara ya bahari ya taifa, taasisi ya sayansi ya China na wizara ya elimu, mbili zinafanya uchunguzi kwenye ncha za dunia, meli nyingine zaidi ya 10 zinafanya utafiti wa kisayansi kwenye bahari ya mbali, pamoja na nyingine ndogo zinafanya uchunguzi kwenye bahari ya karibu. Meli hizo karibu zote zilitengenezwa au kurekebishwa kuwa za uchunguzi katika miaka ya 70 au 80 ya karne iliyopita. Taasisi ya sayansi ya China hivi sasa ina meli 4 za uchunguzi, ambazo zote zina umri wa zaidi ya miaka 20 na zimeanza kuchakaa. Kama China haitatengeneza meli nyingine mpya za utafiti wa kisayansi, basi itakabiliwa hali ya upungufu wa meli ya uchunguzi.

2004-07-07