Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-08 16:15:50    
Kutengeneza Mashamba Kwenye Jangwa Kubwa la Pili Duniani

cri

    Mzee Alemas mwenye umri wa miaka 80 mwaka huu anaishi katika mahali penye umbali wa kilomita moja tu kutoka pembezoni mwa jangwa kubwa la pili la dunia Taklamagan. Lakini yeye na wenzake wameboresha maisha yao karibu na jangwa hilo kwa kupanda ukanda wa miti wa kuzuia upepo, kutengeneza mashamba na kulima mahindi.

     Baada ya kuishi kwa miaka 30 hivi katika chemchem ya Chele iliyopo jangwani kwenye mkoa ujiendeshao wa Xinjiang, mzee Alemas na wenzake wamepambana na jangwa na kusukuma mbele chemchem hiyo kwa kilomita moja. Hivi sasa watoto na wajukuu wao wanaendelea na kazi ya kuongeza mashamba kutoka kwenye jangwa.

    Chemchem ya Chele iko katika bonde la Talimu mkoani Xinjiang, karibu na milima ya Kunlun, ambapo upepo wenye mchanga unaovumwa kutoka jangwa la Taklamagan kaskazini, siku zote unashambulia chemchem hiyo. Kwa mujibu wa takwimu, vilima vya mchanga pembezoni mwa jangwa kila mwaka vinahama kwa mita 150 hivi kuelekea kwenye chemchem, na vimekuwa tishio kubwa kwa chemchem hiyo. Katika chemchem ya Chele, kila mwaka kuna siku 200 na zaidi za kuwepo na vumbi, ambapo siku 20 hadi 30 zina dhoruba ya mchanga. Ukosefu wa maji na maafa ya upepo na mchanga yameathiri sana maendeleo ya hapo.

     Mkuu wa wilaya ya Chele Abdula Kurban alisema kuwa, ili kuzuia mchanga, kila mwaka wanapanda miti katika mashamba yenye hekta elfu kadhaa kwenye mstari wa pembezoni mwa jangwa wenye umbali wa kilomita 17. Chemchem ya Chele imeongezeka mbele kwa kilomita 7 kwa ujumla ndani ya jangwa, mashamba kati ya kanda za miti za kuzuia upepo yamekuwa mashamba mazuri ya kilimo. Alisema kuwa, kutokana na ujenzi wa Bwawa la Shengli milimani, kutengeneza mfereji wa maji na kueneza matumizi ya kisasa ya umwagiliaji maji, rasilimali nyingi za maji zitaokolewa, na kuweka hali nzuri ya kujenga mashamba mengi zaidi katika jangwa.

    Hivi sasa, chemchem za Chele, Yutian,Minfeng na Hetian zilizoko kusini mwa jangwa la Taklamagan zote ziko mbioni kutengeneza msitu kwenye mchanga, kanda za miti zinazoungana pamoja kwenye jangwa zimefaulu kuzuia upepo wa machanga.

    Msemaji wa Taasisi ya Viumbe na Jiografia ya Xinjiang ya chuo cha Sayansi ya China Bwana Hu Wenkan alisema kuwa, ukanda wa miti kwa upande mmoja unafanya ufanisi mkubwa wa kiumbe na kijamii, kwa upande mwingine unahitaji mitaji mikubwa. Wanasayansi wanafanya utafiti kuhusu jinsi ya kuinua ufanisi wa kiuchumi wa ukanda wa miti wa kuzuia upepo.

    Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, Taasisi ya Viumbe na Jiografia ya Xinjiang ya chuo cha Sayansi ya China ilianzisha kituo cha kuondoa hali ya jangwa katika chemchem ya Chele, kufanya utafiti na majaribio ya kuzuia na kuondoa hali ya jangwa. Kutokana na kipindi kirefu cha hali ya mchanga kuvamia mashamba na kutoweka kwa makazi ya binadamu, ardhi zenye miti na mimea katika ukanda wa mpito kati ya jangwa na chemchem haikuzidi asilimia 3. Sasa wataalamu wamefaulu kuchunguza mtindo wa kupanda miti wakati wa majira ya joto, yaani kutumia maji ya mafuriko kuotesha mbegu za miti, majira ya kuchipua ya mwaka wa pili yenye ukame sana inapofika, miche hiyo imeshakua na yenye uwezo wa kupambana na ukame.

     Kuanzishwa kwa mfumo wa kuondoa hali ya jangwa kumezuia kwa ufanisi mashambulizi ya mchanga dhidi ya chemchem, Mafanikio hayo yamepewa tuzo ya shirika la UNEP, na kuwa mfano bora wa kudhibiti hali ya jangwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-08