Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-08 17:48:42    
Mkazi Mzee wa Beijing Anayependa Kukata Ukataji Kisanii

cri

    Katika kichochoro kimoja cha mtaa wa Beixinqiao, mashariki ya Beijing, anaishi bibi mzee anayependa ukataji wa kisanii. Si kama tu anapenda kukata ukataji wa kisanii wenye sanamu za wanyama, pia anapenda kuonesha hisia zake kwa maisha na matukio muhimu kwa njia ya ukataji wa kisanii. Kabla ya mwaka mmoja na zaidi uliopita, wakati katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Kofi Annan alipotembelea China, mke wake Bibi Nane Lagergren alitembelea hadi nyumbani kwake na kupewa ukataji wa kisanii kadhaa alioupenda sana.

    Bibi mzee huyo anayependa kukata ukataji wa kisanii anaitwa Miao Xiufang, ana umri wa miaka 87 mwaka huu. Anajulikana sana kwa ukataji wake wa kisanii wenye sanamu murua za wanyama. Tofauti na watu wengine, mzee Miao hapendi kutazama TV au kucheza karata, kila alipokuwa na wakati , yeye hupenda kukata wanyama wa aina mbalimbali kwa kisu na karatasi nyekundu. Katika miaka kumi kadha iliyopita, amekata wanyama wengi wasiohesabika, na wanyama hao wanaonekana kama ni wanyama hai wanaotaka kuruka kutoka karatasi. Kama vile, ukataji wake wa kisanii wa Jogoo, manyoya yao yanaonekana yakipeperuka wakati wakipiga makelele; ukataji wa kisanii wa panya uliobandikwa kwenye dirisha humvuta paka kuzunguka mara kwa mara karibu naye. Nyumbani kwa bibi mzee Miao, mapambo yanayopendeza zaidi ndiyo ukataji wa kisanii wenye sanamu za wanyama mbalimbali.

    Ukataji wake wa kisanii unapata tuzo karibu kila mwaka katika maonyesho ya aina mbalimbali, lakini hauuzi hata mmoja, watu wakipenda na kuomba, huwa anawapa bure. Mwezi Octoba mwaka 2002, mke wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bibi Nane Lagergren alitembelea hadi nyumbani kwake. Bibi mzee Miao alijua kuwa, Umoja wa Mataifa umefanya mchango mkubwa kwa amani ya dunia nzima, na Bibi Annan pia amefanya kazi nyingi kwa nchi zinazoendelea, hivyo Mzee Miao alikuwa na heshima kubwa kwa Bibi Annan, na kumpa ukataji wa kisanii kadhaa zilizo nzuri kabisa. Alikumbuka kuwa, wageni wengi wanapenda wanyama wa dragoni na finiksi ambao ni wanyama waliobuniwa katika hadithi za agano za China, hivyo pia alimpa Bibi Annan ukataji wa kisanii wa dragoni na finiksi. Kwa kuwa mwaka ule ni mwaka wa mbuzi nchini China, hivyo alimpa pia ukataji wa kisanii wenye sanamu za mbuzi na maua.

    Bibi Annan aliupenda sana ukataji wa kisanii aliopewa na Mzee Miao, alisema atamwonesha ukataji huo kwa Bwana Kofi Annan. Siku ya pili, picha za Mzee Miao na Bibi Annan zilichapishwa kwenye ukurasa wa kwanza wa magazeti mengi nchini China. Katika mwaka mmoja na zaidi uliopita, Mzee Miao mara kwa mara alimkumbuka Bibi Annan. Kwa kalenda ya China, mwaka huu ni mwaka wa kima, moyoni mwa wachina, kima ni ishara ya busara, baraka na furaha, mzee Miao alikata ukataji mingi wenye sanamu ya kima, anatumaini kumpa Bibi Annan ukataji kadhaa wenye kima ili kumtakia heri na baraka katika mwaka huu wa kima. Kwa sababu bibi Annan hatafika China mwaka huu, hivyo mzee Miao anautuma ukataji wa kisanii kwa njia ya posta,katika barua yake alisema:

    "Mheshimiwa Bibi Annan, mimi ni mzee mwenye umri wa miaka 87 kutoka Beijing, China. Tarehe 14 Octoba mwaka 2002, ulitembelea mtaa nilioishi, nilikuwa na bahati ya kukupatia ukataji wangu wa kisanii wenye sanamu za dragoni na finiksi. Leo nakutuma picha moja zetu ili kueleza hisia zangu kwako wewe. Mwaka huu ni mwaka wa kima nchini China,wachina wanawapenda na kuwaheshimu sana kima , kwa kuwa kima ni busara sana, tena ni wanyama wenye uhai mkubwa, hivyo nitakutuma ukataji wangu wa kisanii wenye sanamu ya kima , kama ni heri na baraka zangu kwako wewe."

    Mzee Miao hapendi kutazama TV, lakini anapenda sana kusoma magazeti, hivyo anajua mambo mengi ya nchini China na ya kimataifa. Anajaribu kuonesha mambo muhimu kwa ukataji wake wa kisanii, kama vile, mwaka 1997,serikali ya China ilirudisha mamlaka ya Hongkong, mzee miao alikata ukataji wa kisanii wenye maua ya zijinghua, ambayo ni maua ya mji wa Hongkong; mwaka wa 1999, China iliporudisha mamlaka ya Macao, mzee Miao pia alikata ukataji wa kisanii wenye maua ya mji wa Macao na kuubandika ukutani. Mwaka jana, mtaa wa Beixinjiao aliokaa ulifanya uchaguzi, wakazi wa mtaa huo walipiga kura kuwachagua viongozi wa mtaa huo. Mzee Miao aliposikia habari hiyo alijipamba na kujiunga na upigaji kura bila kujali umri wake mkubwa, na kupeleka ukataji mingi wa kisanii ili kuonesha uungaji mkono wake. Siku ya pili, picha za mzee Miao kujiunga na upigaji kura na ukataji wake wa kisanii zilichapishwa kwenye ukurasa wa kwanza wa magazeti mengi.

    Japokuwa mzee Miao ana umri mkubwa sana, lakini ana afya nzuri, anaishi kwa furaha. Sasa jambo pekee linalomsumbua ni kwamba,yeye amezeeka siku hadi siku, lakini watoto na wajukuu wake hawapendi kujifunza ukataji wa kisanii, kwa sababu ukataji wa kisanii ni kazi inayohitaji subira na umakini. Binti yake wa pili mwenye umri wa miaka 55 mwaka huu Jia Yandie alisema kuwa, japokuwa hawapendi kujifunza ukataji wa kisanii, lakini watahifadhi kwa makini ukataji wa kisanii wa mama yao:

    "Ukataji wa kisanii mama alionipa nimehifadhi vizuri, kwa kuwa ukataji wa kisanii ukibandikwa mlangoni, ukutani au dirishani, ni rahisi kutoa rangi yake nyekundu, pia ni vigumu kuutoa tena. Hivyo nafikiri kuzitengeneza kwa njia umaalum ili kuhifadhi daima."

    Ukataji wa kisanii wa mzee Miao ni usanii wa kienyeji wenye thamani kubwa sana, hivyo tunatumaini kuwa, ukataji wake wa kisanii utaweza kuhifadhiwa vizuri na watu waliokuwa nao pamoja na Bibi Annan.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-08