Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-14 21:03:33    
Wachina wazingatia kunvywa maziwa kila siku

cri
Maziwa ni chakula chenye virutubisho vingi, maziwa yanaweza kutoa vitu vingi vizuri kwa mwili wa binadamu. Hivyo, watu wanayasifu maziwa kuwa ni "damu nyeupe". Na sasa nchi nyingi zinachukulia kiwango cha matumizi ya maziwa kuwa kigezo cha maisha ya watu. Lakini maoni mazuri ya wachina kuhusu maziwa na bidhaa za maziwa yalipatikana baada ya muda mrefu. Hivi sasa wachina wanapendelea siku hadi siku kutumia maziwa na vyakula vilivyotengenezwa kwa maziwa. Leo tunawaletea maelezo kuhusu jambo hilo.

" maziwa ni matamu sana, mama yangu aliniambia maziwa ni mazuri sana, yanasaidia watoto kujenga afy, hivyo nakunywa maziwa kila siku."

Sasa watoto wengi wa China wanakunywa maziwa kila siku. Lakini kabla ya mwaka 1978, wakati China bado haijatekeleza mageuzi ya uchumi ya ufunguaji mlango, wachina walikuwa wanakunywa maziwa kidogo sana. Katika wakati huo, kunywa maziwa lilikuwa ni jambo la anasa. Sababu muhimu ni kwamba, katika miaka ya 70 na 80, viwanda vya utengenezaji wa maziwa vilikuwa si vizuri, kulikuwa na viwanda vichache tu vya maziwa katika miji mikubwa, na utoaji wa kila mwaka haukuweza kufikia tani milioni moja. Sababu nyingine ni kuwa, wachina wengi hawakuwa na desturi ya kunywa maziwa tangu zamani.

Katika miaka 20 iliyopita, kutokana na maendeleo makubwa ya uchumi nchini China, wachina walianza kuzingatia suala la afya. lakini tangu zamani mfumo wa chakula wa wachina ulitegemea sana mchele, hivyo ulikuwa siyo mzuri sana. Watu wengi walikuwa na matatizo ya ukosefu wa Vitamin na Calcium, na ubora wa protein haukuwa mzuri sana, mambo hayo yaliathiri vibaya afya za watu.

Wanasayansi wanaona kwamba, maziwa na chakula kilichotengenezwa kwa maziwa kinawasaidia wachina kutatua matatizo hayo. Mkurugenzi wa Kamati ya viwanda vya chakula cha maziwa ya China Bw. Song Kungang alisema kuwa, ni muhimu sana kuwahimiza wachina kunywa maziwa.

" maziwa na chakula kilichotengenezwa kwa maziwa vinatuleta afya njema, maisha yetu yanatiwa nguvu, hivyo tunapaswa kuwasaidia watu kuwa na desturi ya kunywa maziwa, na kuongeza chakula cha maziwa katika maisha yao. Hii ni muhimu katika kuongeza ubora wa maisha ya watu wa China."

Bw.Song Kungang alisema kuwa, watu wengi wa China bado wana mawazo potofu kuhusu matumizi ya maziwa, kwa mfano, watu kadhaa wanaona kuwa, maziwa ni chakula kizuri, ambacho kinawafaa watoto na wazee tu, vijana hawahitaji maziwa. Wachina wana tatizo la upungufu wa madini ya Calcium, lakini watu wengi hawajui kwamba, maziwa yana Calcium nyingi.

Ili kuwawezesha watu wengi zaidi kutambua umuhimu wa maziwa, Kamati ya viwanda vya chakula cha maziwa ya China ilifanya shughuli nyingi kuhamasisha unywaji wa maziwa. Mbali na hayo, magezeti mengi ya China hutangaza ripoti na makala kuhusu umuhimu wa maziwa.

Wakati huo huo, kazi ya ufugaji na utengenezaji wa chakula cha maziwa nchini China inaendelea haraka. Hadi kufikia mwaka 2003, makampuni ya utengenezaji wa vyakula cha maziwa nchini China yalifikia 560, na utoaji wa chakula cha maziwa ulifikia tani milioni 160.

Sasa bila kujali uko kwenye duka gani, unaweza kupata chakula cha maziwa, kama vile, unga wa maziwa, siagi, ice cream.

Wang Fangfang ni muuzaduka, alimwambia mwandishi wa habari:

"bidhaa za maziwa za duka letu zinauzwa vizuri sana. Kwa mfano, watu wananunua maziwa kwa maboksi, na mtindi pia unauzwa vizuri sana. Sasa hali ya hewa ni joto sana, hivyo ice cream zinanunuliwa sana na watu."

Sasa maziwa na bidhaa za maziwa ni chakula cha lazima katika maisha ya wachina. Bibi Pan Peilei ni mfanyakazi katika idara moja ya serikali ya Beijing, kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita amekuwa akinywa maziwa kila siku. Alitoa maoni yake kwa mwandishi wa habari maoni yake, akisema:

" katika miaka ya hivi karibuni, nimekuwa nikinywa maziwa wakati wa chakula cha mchana. Siku hadi siku, afya yangu inakuwa nzuri sana. Watu wengi wana ugonjwa wa osteoporosis, lakini mimi sina. Nafikiri sababu muhimu ni kwamba, nashikilia kunywa maziwa kila siku."

Ingawa wachina wengi wanaona umuhimu mkubwa wa maziwa kwa afya za binadamu, na wachina wengi zaidi wameanza kunywa maziwa kila siku, Lakini likilinganishwa na kigezo cha kimataifa, China bado iko nyuma. Hasa katika miji midogo, wilaya na vijiji, kiwango cha matumizi ya bidhaa za maziwa bado ni kidogo.

Kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa Kamati ya viwanda vya bidhaa za maziwa ya China Bw. Song Kungang alisema kuwa, katika siku za baadaye, kamati hiyo itashirikiana na mashirika mengine ya China, kuchukua hatua mbalimabli, kueneza elimu ya umuhimu wa maziwa kwa watu, ili kuwawezesha watu wengi zaidi kuchagua bidhaa za maziwa.

Idhaa ya kiswahili 2004-07-14