Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-21 21:13:58    
Namna ya kupima uzito wa mwanaanga akiwa anga ya juu

cri

   Mwanaanga mmoja akikula chocolate

    Kupima uzito wa mwili ni jambo rahisi kabisa kwetu sisi, lakini katika mazingira ya anga ya juu, ambayo uzito wa vitu huonekana kuwa mdogo mno, uzito wa mwanaanga unapimwa kwa namna gani?

    Mwanaanga akiwa katika kituo cha angani na kufanya kazi kwa muda mrefu, anatakiwa kupimwa afya yake na uzito wa mwili. Mtaalamu wa kituo cha udhibiti wa safari za anga ya juu cha Russia Bw. Runjin alisema kuwa kutokana na kuwa uzito wa mwanaanga anayekuwa anga ya juu, unaonekana kama haupo kabisa, hivyo njia ya upimaji wa uzito wa mwili kwenye anga ya juu ni tofauti kabisa na ile inayotumika hapa ardhini. Wakati mwanaanga anapopimwa uzito wa mwili, anapaswa asimame kwenye kibao kilichowekwa katika upande mmoja wa nyenzo, na kufanya spring moja iliyowekwa chini ya kibao kukandamizwa chini, kisha kufungua spring hiyo kwa spana moja maalumu, na kuifanya ifyatuke. Kupima nafasi iliyofyatuka kwa zana maalumu, kunaweza kutambulisha uzito wa mwanaanga huyo.

    Zana za aina hiyo za kupima uzito wa mwili, zilivumbuliwa na wataalamu wa Russia ili kupima uzito wa mwili wa wanaanga wanaofanya kazi kwenye anga ya juu. Hata katika mwaka 1974, wanaanga wa Urusi ya zamani walipofanya kazi katika kituo cha anga ya juu kilichojulikana kwa "Salute-3", walipimwa uzito wa mwili kwa njia hiyo.

    Kwa kawaida uzito wa mwili wa wanaanga hupungua kwa kilo 2 hadi 4 baada ya kufanya kazi kwenye anga ya juu, kutokana na kutumia nguvu nyingi za mwili. Lakini wanaanga wawili walioko katika kituo cha kimataifa cha anga ya juu, tarehe 1 Julai, walipopimwa uzito wa miili yao baada ya kutembea nje ya kituo, uzito wa miili yao ulikuwa sawa na ule waliokuwa nao kabla ya kutembea kwenye anga ya juu.

    Wanaanga hao wawili walipokuwa nje ya kituo cha anga ya juu, wakitumia saa 5 na dakika 40, walifaulu kukarabati gurudumu tuzi (gyro) iliyoko nje ya kituo. Baada ya kufanya kazi kubwa katika anga ya juu, hivi sasa wanaanga hao wawili wanapumzika na kutumia nafasi hiyo wanafanya kazi za kuweka usafi kwenye vyumba vya kituo cha anga ya juu.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-19