Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-20 13:34:35    
Barua za wasikilizaji 20/7/2004

cri
    Msikilizaji wetu Bwana Kaziro Dutwa wa S.L.P 209 Songea Ruvuma-Tanzania ametuletea barua akisema kuwa, yeye ni mzima na anafurahi kuwasiliana nasi tena.

    Anasema amefurahishwa sana na moyo wetu wa upendo kwa wasikilizaji, kuwaandalia bahasha ambazo ni maalum zikiwa zimelipiwa gharama za posta. Hii ni kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano, anasema hakika huu ni ukarimu wa ajabu ulioje. Hata hivyo pamoja na juhudi zetu hizi anasema kwa upande wake anasikitika hajaweza kufaidi matunda haya kwani hizi bahasha zetu bado zinakataliwa hukoo Songea na kila barua yake ni lazima ibandikwe stempu vinginevyo hurejeshwa kwake. Hata hivyo anasema anatumai kuwa ufumbuzi utapatatikana katika siku si nying.

    Lingine ni kuhusu tovuti yetu, anasema kwa kweli ilimvutia sana tangu siku ile ya kwanza alipofuangua ukurasa wetu kwenye uso wa Kompyuta. Alisoma makala kadha wa kadha zenye kuvutia nakuona picha za watangazaji wa idhaa ya kiswahili. Dhamira yake ilisutwa sana na picha za kwenye mtandao hasa picha za watangazaji na mwalimu maarufu wa kiswahili Shao Chen.

    Anasema, picha iliyokuwepo akilini mwake ni tofauti kabisa na picha iliyokuwa akiiona kwenye Kompyuta. Hata hivyo Kompyuta haikuweza kujali. Hivyo dhamira ilikuwa haina jinsi ila kukiri picha iliyokuwa kwenye ukurasa wa Kompyuta kuwa ni ya kweli. Kuna picha moja alipiga akiwa kwenye mbuga za wanyama bila shaka ni Afrika ya mashariki, je ni wapi hapo?

    Kuhusu hii tunapaswa kuomba radhi kwa wasikilizaji wetu. Tulipoweka picha hizo hatukuweka maelezo, lakini kutokana na mapendekezo na maswali yenu tutasahihisha. Kuhusu picha hizo wasikilizaji wetu kadhaa wametuandikia barua wakiuliza suali kama hilo. Mwaka jana tulipokwenda Kisii Kenya kukutana na wasikilizaji wetu, njiani tulipita mbuga ya Masaimara, sehemu hiyo ilikuwa karibu na mpaka kati ya Kenya na Tanzania, nadhani mkiona picha hiyo mtaona karibu na mama Chen wapo walinzi kadhaa.

    Bwana Dutwa anasema, anatupongeza sana kwa juhudi zetu kuweza kufanikisha idhaa ya kiswahili kuwa na tovuti yake na bila shaka itaboreshwa zaidi kadri siku zinavyosonga mbele, anatuombea kwa Mungu atubariki katika kazi yetu hii ngumu atupe uwezo ili tiweze kuwaelemisha na kuwaburudisha zaidi wasikilizaji wetu.

    Tunamshukuru sana msikilizaji wetu maarufu Kaziro Dutwa kwa barua yake ya kututia moyo tuendelee na juhudi za kuboresha zaidi tovuti yetu. Ni matumaini yetu kuwa wasikilizaji wetu wengine wakipata nafasi watatembelea mara kwa mara tovuti yetu na kutuletea maoni na mapendekezo.

    Msikilizaji wetu Ras Franz Manko Ngogo, wa Klabu ya wasikilizaji wa Radio China Kimataifa Kemogemba, Sanduku la Barua 71 Tarime mara-Tanzania anasema katika barua yake kuwa, anapenda kuendelea kutuletea maoni yake kuhusu vipindi vyetu maalum vya maadhimisho ya mika 40 ya uhusianio wa kibalozi kati ya China na Tanzania. Tarehe 28/4/04 kama kawaida mahojiano baina ya watanzania ama wachina wazielewazo nchi hizi mbili yaliendelea.

    Mara hii yalimuhusu Bw Hirari Bujiku ambaye ni mpiga picha wa waziri mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Frederick Sumaye. Bw Bujiku akieleza maoni yake jinsi alivyoona China na wakazi maendeleo na maisha yake hadi vijijini aliibuka na wazo ama pendekezo moja la maana, alisema watanzania nao wangepanga uzazi ili kuwa na mwanya wa maendeleo sawa na China.

    Anasema ana hakika, maoni hayo yalimweka katika wazo jipya la maisha. Hakika mfululizo huu umevutia na kuwapa changamoto kubwa wasikilizaji wa idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa.

    Tarehe 29/4/2004 maelezo ya mwisho ya jinsi uhusiano wa uendeshaji wa kiwanda cha urafiki maelezo yaliyohusisha sana wasikilizaji wote wale waliosikiliza mfulilizo wa vipindi maalum vya maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa Kibalozi kati ya China na Tanzania.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-20