Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-20 14:06:53    
Masoko ya magari nchini China yavutia watu wa nchi mbalimbali

cri

Jumuiya ya sekta ya uzalishaji wa magari ya Ujerumani, ambayo inawakilisha maslahi ya kampuni zaidi ya 500 za magari na vipuri vya magari za nchi hiyo, hivi karibuni ilituma ujumbe nchini China na kuwaonesha wateja wa China magari ya nchi yake. Mkurugenzi mkuu wa jumuiya hiyo profesa Bernd Gottschalk, alisema

    "Sisi tunaongoza duniani katika teknolojia ya magari na mageuzi. Katika siku za baadaye, sekta ya uzalishaji wa magari ya Ujerumani itaongeza haraka shughuli zake za biashara nchini China, na kuendelea kufanya ushirikiano na kuhakikisha kwamba wateja wa China wana haki ya kuendesha magari bora ya kiwango cha juu."

    Lengo la safari ya jumuiya ya magari ya Ujerumani nchini China ni dhahiri kuwa inataka kushirikisha kampuni zote za magari ya Ujerumani, kuwashinda washindani wao waliotoka nchi nyingine kwa nguvu zao za pamoja, na kupanua nafasi zao katika masoko ya magari ya China.

    Magari ya Ujerumani yaliingia China toka miaka mingi iliyopita, na yamepata mafanikio makubwa. Licha ya magari yaliyoagizwa kutoka Ujerumani, magari zaidi ya laki 7 kati ya magari zaidi ya milioni 2 yanayozalishwa nchini China ni ya kijerumani. Kampuni ya BMW, ambayo inajulikana kwa kuzalisha magari madogo ya anasa, ilijenga kiwanda cha ubia pamoja na China, aina 5 za magari yanayozalishwa hivi sasa na kiwanda hicho, yanapendwa sana na watu. Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho cya ubia, Bw. Heinz-Juergen Pressler alisema,

    "Tunatarajia kuwa wafanyabiashara bora kabisa wa magari ya hali ya juu, na tunatarajia kujiimarisha kwa kuambatana na maendeleo ya soko la China."

    Kampuni ya VolksWagen ni nguvu kubwa ya wafanyabiashara wa magari wa Ujerumani hapa nchini. Katika wakati fulani, nusu ya idadi ya magari madogo yaliyozalishwa nchini China, yalitoka kwa viwanda vya ubia vya VolksWagen; Magari madogo ya Audi yalichaguliwa na serikali ya China kuwa ya matumizi ya kiofisi. Hivi karibuni, kampuni ya Daimler Chrysler pia imeshiriki katika mkondo wa uzalishaji wa magari nchini China.

    Katika maonesho ya kimataifa ya magari yaliyofanyika mwezi uliopita hapa Beijing, kampuni ya Ford ya Marekani ilionesha magari 51 ya aina mbalimbali, ambayo yaliwafurahisha sana watazamaji. Hivi sasa meli mbili zinazobeba magari yaliyozalishwa na kampuni ya Ford huko Marekani, zinafika China baada ya kila wiki mbili; mauzo ya magari yaliyozalishwa na viwanda vya ubia hapa nchini pia yanaongezeka mwaka hadi mwaka, hali ambayo inawafurahisha sana viongozi wa kampuni. Naibu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Ford nchini China, Bw. Xu Guozhen alisema,

    "Ford inaendelea vizuri sana nchini China! Kati ya Januari na Aprili mwaka huu, mauzo ya magari yaliongezeka kwa 200%. Tuna imani ya kuwa na maendeleo makubwa mwaka huu."

    Wateja wa China wanayafahamu sana magari ya aina ya Buick yanayotengenezwa na kampuni ya General Motors. Magari ya PSA Peugeot ya Ufaransa, magari ya Honda na Toyota ya Japan na magari ya Hyundai ya Korea ya Kusini yamejenga msingi hapa China. Taarifa moja iliyotolewa hivi karibuni na Jumuiya ya Viwanda vya Magari ya China inasema kuwa kampuni zote muhimu za magari duniani zimeshaingia China, na zinaongeza uwekezaji hatua kwa hatua.. kampuni kubwa za kimataifa zikitumia njia ya kuanzisha viwanda vya ubia, zimechukua 90% ya nafasi ya masoko ya magari madogo ya China. Kwa nini masoko ya magari ya China yanawavutia sana wafanya biashara wa magari duniani? Ongezeko la kasi la uchumi wa China na kuinuka kwa kiwango cha maisha ya watu, kunafanya soko la magari ya China kuhitaji magari mengi. Magari madogo, ambayo katika miaka ya 80 ya karne iliyopita yalichukuliwa kama ni vitu vya anasa vya kuonesha vyeo na hadhi za maofisa, yameingia majumbani kwa watu wa kawaida. Mwaka Jana magari ya binafsi yaliongezeka kwa kiasi cha milioni 1.2. Hivi sasa, wafanya biashara wa kigeni wamejenga viwanda vyao hapa China na kutengeneza magari mapya kila wakati, ambayo yanawapendeza wachina na kuboresha maisha yao. Kutokana na kuwa China ni nchi yenye idadi ya watu bilioni 1.3, ingawa wafanya biashara wa magari wameongezeka sana nchini nchini, lakini bado wanapata faida kubwa kila mwaka.

    Wanaviwanda wa magari nchini waliokuwa na ushirikiano na wafanyabiashara wa magari wa kigeni katika kujenga viwanda vya ubia, pia wanawakaribisha wafanya biashara wa magari wanaotoka nchi za nje, kwani licha ya kupata faida kubwa, wamejisogeza mbele na teknolojia na usimamizi wa kimaendeleo duniani. Kwa mfano kampuni ya magari ya Shenlong, mjini Wuhan ambayo imeanzishwa kwa ubia na kampuni ya magari ya Dongfeng na kampuni ya PSA Peugeot ya Ufaransa, karibu kila mwaka inazalisha aina mpya ya magari madogo ya hali ya wastani, na hivi sasa wachina wanayafahamu sana magari ya Cietron.

    Bw. Guan Wanqiang ni shabiki wa magari, amenunua gari moja la aina ya Volkswagen Bora lililotengenezwa na kiwanda cha magari cha ubia kati ya China na Ujerumani. Yeye ni kama wachina wengine waonavyafanya kuunga mkono maendeleo ya magari yanayozalishwa na viwanda vya ubia. Bw. Guan alisema kuwa bila viwanda hivyo vya ubia, China ingekosa teknolojia mpya ya uzalishaji wa magari. Hivi sasa tofauti ya ubora kati ya magari yanayozalishwa hapa nchini na yale yaliyozalishwa na kampuni kubwa za magari inapungua siku hadi siku.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-20