Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-20 20:26:58    
Kambi ya siku za joto yawapa watoto na vijana mafunzo ya sheria

cri

    Siku za karibuni, wanafunzi zaidi ya sitini kutoka mji wa Luo he mkoani He Nan walishiriki kwenye kambi ya siku za joto ya mji huo, ambayo kauli mbiu yake ni "kuingia mahakamani, kufahamu sheria na kuacha vitendo vya uhalifu".

    Kambi hiyo iliandaliwa na halmashauri ya mji wa Luo he ya umoja wa vijana wa chama cha kikomunisti cha China, idara ya elimu ya mji huo na mahakama ya wilaya ya Hui yuan. Lengo lake ni kuwapa watoto na vijana mafunzo ya sheria kupitia njia ya kuwapa fursa ya kujifunza kuhusu sheria kwenye mahakama halisi. Katika shughuli za kambi hiyo, mahakimu wa mahakama ya vijana aliwaongoza wanafunzi hao kutembelea mahakama na kuwaonesha zana za mahakama hiyo na kuwaeleza kazi na maisha ya hakimu. Hakimu huyo pia alichagua kesi zinazotokea mara kwa mara na kutoa hukumu hapo papo, ili wanafunzi wasikilize kufanya majadiliano baadaye na wanafunzi hao kuhusu kesi hizo, ili kuinua mwamko wa kisheria wa wanafunzi hao.

    Hakimu huyo pia alichagua kesi halisi iliyohukumiwa na mahakama hiyo ya vijana, na kuwaacha baadhi ya wanafunzi kuvaa nguo za hakimu, na wanafunzi wengine kuwa wahusika wa "mwanasheria", "mshtaki" na "mshtakiwa", na kuigiza shughuli za mahakama ya vijana. Pande mbili za mshtaki na mshtakiwa zilifanya majibizano makali kuhusu makosa yaliyofanywa na mshtakiwa ambayo yanavifikisha vitendo vyake kwenye kiwango cha uhalifu. uigizaji wa kusikiliza kesi ulifanyika vizuri sana, hata walimu na wazazi wa wanafunzi hao waliosikiliza kwenye mahakama hiyo walipiga makofi mara kwa mara.

    Katika shughuli za kambi hiyo, mahakimu 10 wa makahama hiyo waliojitokeza pia walitafuta wanafunzi 10 kila hakimu na mwanafunzi mmoja wakishirikiana kwenye shughuli za kutoa ujuzi kuhusu sheria kwa wanafunzi wengine, na pande mbili zilianzisha utaratibu wa mawasiliano ya mara kwa mara. Mahakimu hao wanawasaidia wanafunzi hao kutatua matatizo ya kisheria katika maisha ya wanafunzi hao ili wanafunzi hao waweze kueneza ujuzi wa sheria kwenye shule. Wanafunzi walioshiriki kambi ya siku za waliapishwa mbele ya bendera ya taifa wamedhamiria kujifunza sheria, kufahamu sheria na kufuata sheria, ili wawe raia wadogo wema.

    Kambi hiyo ya siku za joto ya kutoa elimu ya sheria inakaribishwa sana na jamii. Halmashauri ya mji wa Luo he ya umoja wa vijana wa chama cha kikomunisti cha China imefanya mahakama ya wilaya ya Hui yuan kama ni "kituo cha mafunzo ya utaratibu wa sheria kwa watoto na vijana". Halmashauri ya kazi ya kuwafuatilia watoto na vijana, na idara ya elimu ya mji huo pia zilisifu na kuunga mkono shughuli za kambi hiyo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-07-20