Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-07-21 16:06:24    
Mahojiano na wanafunzi wa Kenya mjini Beijing

cri
    Mwandishi: Ni kwanini ulichagua kuja kusoma China?    

Glory

    Glory: Mimi binafsi sikuchagua kuja kusoma hapa China ,sababu iliyonifanya nije ni kutokana na mzazi wangu kuchaguliwa kufanya kazi hapa nchini China ndio maana nilikuja ,pia nilipofika China niliyapenda sana mazingira yake kwa ujumla ndio maana nikaamua kusoma hapa hapa wala sikujali ugumu wa lugha ya kichina ,pia sikupenda kwenda kusoma nchi nyingine zaidi ya China.

    Sandra:Mimi nilichagua kuoma hapa kwasababu napenda changamoto yaani napenda vitu vilivyo vigumu.

    Mhandishi:Tukiangalia mazingira ya elimu ya kule Afrika ya mashariki labda nianze na wewe Glory; mazingira ya shule na au vyuo ya kule Tanzania ukilinganisha na China unaona kuna kufanana au kuna tofauti yoyote?

    Glory; Ukilinganisha vyuo vya hapa na vya pale nyumbani ninaona kwa kweli mazingira ni tofauti sana kwasababu vyuo vya hapa kuna vitu vingi ambavyo kule kwetu hatuna,Pia kuna changamoto sana kwa wanafunzi ambapo sisi kule nyumbani hatuna,pia wanafunzi wa kichina wana sehemu nyingi nzuri ambazo wanafanyia michezo na pia katika madarasa ambayo hapa china tunayasomea kuna vyombo vingi vya kitaalamu ambavyo vinawasaidia wanafunzi kuweza kuelewa zaidi ambapo wakati wa mazoezi (practical) tunafanya kwa kutumia vyombo vyenye utaalamu wa juu ukilinganisha na Tanzania. Hivyo mimi naona mazingira ya China yako katika hali ya juu kuliko ya kwetu.

    Mhandishi; Je Sandra ukilinganisha mazingira ya Kenya na hapa China unaona kuna tofauti au ni sawa.

    Sandra; Ndiyo kuna tofauti kubwa sana ,kwanza lugha kule Kenya tunasoma kwa kingereza na huku ni kwa kichina hivyo ni tofauti kubwa sana maana huku ni lazima usome kila wakati ukilinganisha na kule Kenya ,na gharama ya kuishi huku China ni kubwa kuliko Kenya mfano bei ya vyakula ni tofauti sana.

    Mhandishi; Labda tuzungumzie tatizo la lugha kwasababu umegusia lugha.Nianze na wewe Glory kule Tanzania watu wanaamini kuwa kichina ni moja ya lugha ngumu na wanafunzi wengi kidogo wanakwepa kwepa kuja China kwa sababu ya kuogopa kujifunza kichina,sasa wewe ilikuwaje ukajifunza lugha inayosadikiwa kuwa ni ngumu sana?

    Glory; Kwa upande wangu mimi naona kichina sio kigumu na wanafunzi wengi kutoka Tanzania au nchi mbalimbali huwa wanakwepa sana hii lugha ya kichina, lakini mimi naona unapoamua kuisoma ni kiasi cha kujifunza kwa bidii kwasababu katika kusoma hakuna kitu ambacho ni kirahisi ,lakini ukijifunza utaona ni rahisi .pia ukilinganisha nyumbani huwa hatuandiki kwa kutumia character ila kwa hapa China ni lazima uandike kwa kutumia chinese character ambapo nyumbani tunatumia herufi.Na kitu ambacho wanafunzi wengi wanakiogopa ni ile kuandika kwa kichina,lakini ukiwa na moyo wa kutaka kujua ni rahisi sana hivyo nawashauri wanafunzi wenzangu walioko nyumbani ambao wanataka kuja kusoma hapa China wasikate tamaa wala wasisikilize maneno ya watu kwasababu lugha ya kichina ni kama lugha nyingine kama ilivyo kiswahili, kwa hiyo sioni kama kuna ugumu wowote kwangu mimi.

     Mhandishi; Labda nikuulize wewe Sandra tangu umefika hapa wewe na Glory tayari mnaweza kuongea kichina na mnaweza kusoma na kuandika.

    Sandra; Ndio tumaweza kuongea ,kusoma na kuandika vyote tunaweza.

    Mhandishi; Kwa mfano sasa hivi mkienda kule Tanzania mnafikiri mnaweza kuandika kichina mnaweza labda mkawafundisha watu kuandika na kusoma kwa kichina?

    Sandra; Ndio tunaweza maana tayari tumeshakuwa na uzoefu wa hii lugha.

    Mhandishi; Mnafikiri ugumu wa kujifunza lugha ya kichina uko wapi

    Sandra; Hamna ugumu ni kama kujifunza lugha nyingine kama kifaransa ,kijerumani n.k kwanza naona kifaransa ni kigumu kuliko kichina kwasababu sijui ni kwanini mimi naona kichina ni rahisi kwangu kuliko hata kingereza na kiswahili.

    Mhandishi; Labda niongee kitu kimoja unafikiri wachina wanafahamu waafrika vizuri au hawawafahamu vizuri;

    Sandra; Wachina hawawafahamu waafrika vizuri, kwa mfano juzi nilimuuliza mchina mmoja unafahamu Kenya akasema hapana akafikiri namuuliza Canada .Lakini wanajua bara la Afrika lakini hawajui nchi zilizo ndani ya bara hilo .ila ukisema Afrika kusini wanajua maana kulikuwa na wazungu wengi wengi kule lakini nchi nyingine hawajui.

    Mhandishi; Ina maana wanafahamu kuwa wewe ni mwafrika lakini hawajui wa sehemu gani

    Sandra; Ndiyo.

    Mhandishi; Glory na wewe ulishawahi kukutana na kitu kama hicho ambapo unaona wachina hawana ufahamu wa Afrika?

Glory; kwa upande China kuijua Afrika wapo wachina wengi wanaijua Afrika vizuri na wengine hawaijui. Na wachina ambao hawaijui Afrika ni wale waliotoka vijijini ,lakini wachina ambao wako mijini na wana elimu wanajua vizuri sana jinsi Afrika ilivyo na mazingira yake.Na wengi wao wanapenda sana kusoma na kuijua Afrika ilivyo hata marafiki zangu wa kichina ambao nimekuwa nao shuleni huwa wananiuliza Tanzania iko wapi lakini nilipowaonesha kwenye ramani waliweza kujua na kuwa na uelewa wa haraka kwamba Afrika ina nchi ngapi na Afrika ikoje ,kwa hiyo kuna baadhi sio kwamba ni wachina wote hawaijui Afrika.

Idhaa ya kiswahili 2004-07-21